Itikadi
Uislamu ni Itikadi na Sheria. Na Itikadi ndio msingi ambao dini inasimama juu yake. Itikadi ya Kiislamu ni itikadi iliyo wazi na nyepesi, inayoafikiana na akili timamu na umbile la asili lililo salama.
mada ndogo ndogo
Shahada mbili
Uislamu ulilipa neno la Tauhidi (yaani, kusema kwamba hakuna mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu), cheo kikuu na kitukufu zaidi. Huo ndio wajibu wa kwanza wa Muislamu. Kwa hivyo, anayetaka kuingia katika Uislamu, ni lazima aliamini neno hili na alitamke. Na mwenye kulisema akiwa na yakini nalo, akitafuta kwalo uso wa Mwenyezi Mungu, litakuwa ni sababu ya kuokoka kwake kutokana na Moto. Kama alivyosema Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: “Kwani hakika, Mwenyezi Mungu alimharamishia Moto yeyote mwenye kusema: "Laa ilaaha illa Llah" (yaani, hakuna mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu) akitafuta kwa hilo uso wa Mwenyezi Mungu.” (Bukhari 415)
Imani
Jumbe zote za Manabii kwa kaumu zao zilikubaliana juu ya kumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake bila mshirika, na kukufuru vyote vinavyoabudiwa badala ya Mwenyezi Mungu. Na huu ndio uhakika wa maana ya neno la Tauhid. Nalo ni neno ambalo mtu huingia kwalo katika dini ya Mwenyezi Mungu.
Ibada
Ibada ni utiifu wa kila aina kwa Mwenyezi Mungu, kwa upendo, utukufu, na kunyenyekea. Nayo ni haki ya Mwenyezi Mungu juu ya waja wake, na ni mahsusi kwake pekee. Ibada inajumuisha kila kitu ambacho Mwenyezi Mungu anakipenda na anachoridhia miongoni mwa maneno na vitendo alivyoviamrisha na akawaamrisha watu kufanya, sawa yawe ni katika matendo ya dhahiri kama vile swala, zaka, na Hija, au katika matendo ya ndani kama vile kumdhukuru Mwenyezi Mungu kimoyomoyo, kumhofu, kumtegemea, kumuomba msaada na mengineyo.