Zaka
Zaka ni nguzo ya tatu ya Uislamu. Mwenyezi Mungu aliifaradhisha ili imtakase na kumsafisha mtoaji na mchukuaji. Ingawa inaonekana kwa dhahiri kwamba ni kupunguza kiwango cha mali, lakini katika athari zake ni kuongezeka kwa baraka katika mali, kuongezeka kwa kiasi chake na kuongezeka kwa imani katika moyo wa mwenye kuitoa.