Endelea kujifunza

Umeshaingia
Jisajili sasa kwenye jukwaa la Taa ili uanze kujifunza, na fuatialia maendeleo yako, na kukusanya pointi, na uingie kwenye mashindano.Baada ya kujisajili, utapata cheti cha kielektroniki katika mada ambazo utajifunza.

Sehemu ya sasa:

Somo Mali ambazo Zaka inalazimika kutolewa kwazo

Zaka ilifaradhishwa katika vitu maalumu miongoni mwa mali ili kuvisafisha. Katika somo hili, utajifunza kuhusu mali ambazo Zaka inalazimika kutolewa kutoka kwazo.

  • Kujua mali ambazo Zaka inalazimika kutolewa kutoka kwazo.

Ni mali gani ambazo Zaka inalazimika kutolewa kwazo?

Zaka siyo wajibu katika kile ambacho Muislamu anamiliki kwa ajili ya kujinufaisha mwenyewe, kama vile nyumba yake anayoishi hata kama itakuwa ghali kiasi gani, au gari lake analotumia, hata kama ni la kifahari namna gani, na vile vile nguo zake, chakula chake na kinywaji chake.

Mwenyezi Mungu aliwajibisha Zaka katika aina fulani za mali ambazo katika sifa zake ni kukua na kuongezeka, ambazo ni:

1. Dhahabu na fedha, ambazo hazitumiwi katika mavazi na mapambo

Zaka siyo wajibu katika hizo isipokuwa ikiwa zitafikia kiwango maalumu cha kisheria (yaani, Nisab), na mwaka mzima wa mzunguko wa mwezi ukapita hali ya kuwa ziko katika miliki yake, nazo ni siku 354.

Nisab ya Zaka ya dhahabu na fedha ni kama ifuatavyo:

١
Dhahabu ni kilogramu 85 takriban.
٢
Fedha ni kilogramu 595.

Basi ikiwa Mwislamu atamiliki kiasi hiki - au zaidi - cha dhahabu au fedha, na mwaka mmoja ukapita, basi atatoa zaka yake kwa kiasi cha asilimia 2.5% ya thamani yake.

2. Mali mbalimbali

Zinajumuisha mali za hela taslimu kama vile sarafu za kila aina, ziwe ziko mkononi mwake au aliziweka katika benki.

Jinsi ya kutoa Zaka ya mali mbalimbali

Muislamu atahesabu Nisab ya mali na sarafu kwa kiasi kinacholingana cha dhahabu. Kwa hivyo, ikiwa ana mali sawa na Nisab ya dhahabu, ambayo ni takriban gramu 85, au zaidi yake wakati wa ulazima wa kutoa zaka, na ikawa kwamba mali hizo zimepitiwa na mwaka mmoja wa mzunguko wa mwezi hali ya kuwa ziko katika milki yake, basi atatoa kwazo asilimia 2.5% ya thamani yake.

Mfano wa kuhesabu Nisab ya Zaka ya mali:

Ikiwa tutachukulia kwamba bei ya gramu moja ya dhahabu wakati wa ulazima wa kutoa zaka ni sawa na dola ishirini na tano (USD 25), basi inakuwa Nisab ya zaka ni kama ifuatavyo: dola ishirini na tano (USD 25) (bei ya gramu moja ya dhahabu, ambayo inabadilikabadilika) x 85 (idadi ya gramu, ambayo haibadilikibadiliki) = dola elfu mbili mia moja na ishirini na tano (USD 2125).

3. Bidhaa za biashara

Nazo ni mali zote zilizoandaliwa kwa ajili ya biashara, kama vile mali isiyohamishika, majengo au bidhaa kama vile vyakula na vitu vya kutumia.

Jinsi ya kutoa Zaka ya bidhaa za kibiashara

Mtu atahesabu thamani ya vitu vyote alivyo navyo kwa ajili ya biashara vinapopitwa na mwaka mmoja, kisha atapima thamani yake kulingana na bei iliyoko sokoni katika siku ambayo anataka kutoa Zaka. Kwa hivyo, ikiwa itafikia Nisab ya mali, atatoa zaka kiasi cha robo ya ushuri, yaani, (2.5%) ya thamani yake.

4. Vitu vinavyotoka katika ardhi kama vile mazao, matunda na nafaka:

Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema, "Enyi mlioamini, toeni katika vile vizuri mlivyovichuma, na katika vile tulivyowatolea katika ardhi." (Al-Baqarah: 267)

Zaka ni lazima katika aina fulani za mazao, ilimradi yamefikia kiwango fulani cha kisheria (Nisab).

Inatofautishwa katika kiwango cha zaka kati ya kile kinachonyweshwa maji na mvua na mito, na kile kinachonyweshwa kwa kumwagiliwa na mwenyewe. Hii ni kwa ajili ya kuzingatia hali mbalimbali za watu.

Masharti ya Zaka kuwa wajibu katika mazao na matunda

1. Mavuno kufikia Nisab

Nabii - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - aliweka kiwango ambacho Zaka ni wajibu ndani yake, na haiwi wajibu katika kilicho chini ya hicho. Alisema, "Hakuna sadaka katika kilicho chini ya Wasaq tano za tende." (Al-Bukhari 1459, Muslim 980) Nacho ni kipimo cha kupima wingi, lakini pia kinaweza kukadiriwa kiuzito katika ngano na mchele mzito kwa kilogramu 612, na hakuna Zaka katika kilicho chini ya kilogramu hizo.

2. Ni lazima mazao yawe ya aina ambayo Zaka inatolewa ndani yake.

Zaka si lazima isipokuwa katika mazao ya kilimo ambayo yanaweza kuwekwa akiba kwa muda na kuhifadhiwa bila kuharibika, kama vile ngano, shayiri, zabibu, tende, mchele na mahindi. Ama aina mbalimbali za matunda na mboga ambazo haziwezi kuwekwa akiba, basi Zaka si lazima katika hizo, kama vile tikiti maji, komamanga, saladi, viazi, na mengineyo.

3. Kwamba mazao hayo yavunwe.

Zaka ni lazima katika mazao na matunda yanapovunwa na kukusanywa, wala hayahusiani na kupita kwa mwaka mzima. Kwa hivyo, ikiwa mazao yatavunwa mara mbili kwa mwaka, basi Zaka itakuwa ni lazima katika kila mavuno hayo. Na ikiwa atatoa Zaka ya mavuno fulani kisha akayahifadhi na kuyaweka akiba kwa miaka, basi haimlazimu Zaka katika miaka hiyo.

5.Rasilimali ya Mifugo

Rasilimali ya mifugo inamaanisha kile ambacho mwanadamu anafaidika kwacho miongoni mwa wanyama wa nyumbani. Kame vile ngamia, ng'ombe, mbuzi na kondoo peke yao.

Mwenyezi Mungu amewaneemesha waja wake kwa kuwaumbia wanyama hoa ili wale katika nyama zao, wavae sufu zao, wawabebe wao na mizigo yao katika safari zao na kuhama kwao. Akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Na wanyama hoa amewaumbia. Katika hao mna vifaa vya kutia joto, na manufaa mengineyo, na baadhi yao mnawala. Na wanawapa furaha pale mnapowarudisha jioni na mnapowapeleka malishoni asubuhi. Na hubeba mizigo yenu kupeleka kwenye miji msiyoweza kuifikia isipokuwa kwa mashaka ya nafsi. Hakika Mola wenu Mlezi ni Mpole, Mwingi wa kurehemu." (Al-Nahl: 5- 7)

Masharti ya jumla ya Zaka ya wanyama hoa

١
Ni lazima wanyama hoa hao wafikie kiwango cha kisheria (Nisab); kwa sababu haiwalazimu kutoa Zaka katika hao isipokuwa matajiri tu. Na wale ambao wana idadi ndogo ya mifugo kwa ajili ya mahitaji yao, hawalazimiki kutoa zaka ya mifugo. Na idadi ya chini zaidi ya zaka ya ngamia ni ngamia watano, na kondoo au mbuzi ni arobaini, na ng'ombe ni thelathini, na hakuna zaka katika kilicho chini ya hao.
٢
Kwamba mwaka mmoja wa mzunguko wa mwezi upite ilhali mifugo hoa wako katika miliki ya mmiliki wao.
٣
Kwamba wawe mifugo hoa hao wanakula nyasi huru katika malisho, na wala mmiliki wao asiwe analazimika kuwapa malisho katika sehemu kubwa ya mwaka.
٤
Kwamba wasiwe wa kufanyia kazi, kama vile katika kulima ardhi, kusafirisha bidhaa, au kubeba mizigo. Hawa hakuna Zaka ndani yao.

Umemaliza somo kwa ufanisi


Anza mtihani