Shahada mbili
Uislamu ulilipa neno la Tauhidi (yaani, kusema kwamba hakuna mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu), cheo kikuu na kitukufu zaidi. Huo ndio wajibu wa kwanza wa Muislamu. Kwa hivyo, anayetaka kuingia katika Uislamu, ni lazima aliamini neno hili na alitamke. Na mwenye kulisema akiwa na yakini nalo, akitafuta kwalo uso wa Mwenyezi Mungu, litakuwa ni sababu ya kuokoka kwake kutokana na Moto. Kama alivyosema Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: “Kwani hakika, Mwenyezi Mungu alimharamishia Moto yeyote mwenye kusema: "Laa ilaaha illa Llah" (yaani, hakuna mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu) akitafuta kwa hilo uso wa Mwenyezi Mungu.” (Bukhari 415)