Endelea kujifunza

Umeshaingia
Jisajili sasa kwenye jukwaa la Taa ili uanze kujifunza, na fuatialia maendeleo yako, na kukusanya pointi, na uingie kwenye mashindano.Baada ya kujisajili, utapata cheti cha kielektroniki katika mada ambazo utajifunza.

Sehemu ya sasa:

Somo Kushuhudia kwamba Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu

Kushuhudia kwamba, “Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu,” ndiyo sehemu ya pili ya shahada mbili. Katika somo hili, utajifunza maana yake na matakwa yake.

  • Kujifunza maana ya kushuhudia kwamba, “Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu.”

Maana ya kushuhudia kwamba, Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- ni Mtume wa Mwenyezi Mungu

Maana yake ni kuzisadiki habari zake, kutekeleza maamrisho yake, kujiepusha na makatazo yake, na kwamba tumuabudu Mwenyezi Mungu kwa mujibu wa yale aliyotuwekea Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, na akatufundisha. Na hilo linajumuisha yafuatayo:

1- Kuamini habari ambazo Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alitujulisha kuhusiana na nyanja zote, miongoni mwake ikiwa ni:

١
Mambo ya ghaibu, Siku ya Mwisho, Pepo na neema zake, na Moto na adhabu zake.
٢
Yale yatakayokuwa miongoni mwa matukio ya Siku ya Kiyama na alama zake, na yale yatakayokuwa katika zama za mwisho.
٣
Habari za wa mwanzo na wale waliotangulia, na yale yaliyotokea baina ya Manabii amani iwe juu yao na kaumu zao.

2- Kufuata maamrisho na makatazo yake, rehema na amani zimshukie, ambazo ni pamoja na:

١
Kutekeleza yale aliyotuamrisha yeye - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, - miongoni mwa ibada mbalimbali, matendo mema na maadili mema.
٢
Kujiepusha na yale aliyotukataza miongoni mwa yale yaliyoharamishwa kama vile maadili mabaya, tabia mbaya, vitendo vyenye madhara, na kuamini kwamba kutuzuia maharamisho hayo ni kwa sababu ya hekima tu aliyoitaka Mwenyezi Mungu, na kwa masilahi yetu, hata kama hekima hiyo inaweza kufichikana kwetu wakati mwingine.
٣
Kuwa na yakini kuwa yeye hasemi kwa matamanio yake, bali ni ufunuo kutoka kwa Mwenyezi Mungu, Mwenye Nguvu, Mtukufu. Kama alivyosema Mtukufu, "Mwenye kumtii Mtume, basi hakika amemtii Mwenyezi Mungu." (An-Nisa: 80)
٤
Kuamini kwamba mwenye kukiuka amri ya Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, anastahiki adhabu chungu. Kama alivyosema Mtukufu, "Basi, na wajihadhari wale wanaokwenda kinyume na amri yake isije ikawapata fitina au ikawapata adhabu chungu." (An-Nur: 63)

3- Kwamba tusimwabudu Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa mujibu wa yale aliyotuwekea Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. Na hilo linajumuisha mambo kadhaa ambayo ni lazima yatiliwe mkazo:

Kumfuata Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake

Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, ndiye kiigizo chetu. Na mja humkaribia Mola wake Mlezi, na daraja zake hupanda kwa Mola wake Mlezi kila anavyofuata mwongozo wa Nabii na Sunna zake kwa wingi, pamoja na kila kilicho ndani yake miongoni mwa maneno, na matendo, na kuafikiana naye na kukiri kila kitu. Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema, "Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu, basi nifuateni mimi, Mwenyezi Mungu atawapenda na atawafutia madhambi yenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta madhambi, Mwenye kurehemu." (Al-Imran: 31)

Sheria imekamilika.

Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, - aliifikisha dini na sheria zote kwa ukamilifu bila ya upungufu wowote. Kwa hivyo, hairuhusiki kwa yeyote kuzua ibada ambayo Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, hakutuwekea kama sheria.

Sheria ya Mwenyezi Mungu ni nzuri kwa kila wakati na mahali.

Hukumu za dini na sheria zilizokuja katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah za Mtume wa Mwenyezi Mungu, - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - ni nzuri kwa kila wakati na mahali. Basi hakuna mwenye kuyajua zaidi masilahi ya wanadamu kuliko yule aliyewaumba baada ya kwamba hawakuwepo.

Kuafikiana na Sunnah

Ili ibada ikubaliwe, ni lazima mtu amkusudie tu Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kwamba ibada hiyo iwe kulingana na yale aliyotuwekea Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - katika sheria. Kama alivyosema Mtukufu, "Kwa hivyo, mwenye kutaraji kukutana na Mola wake Mlezi, basi na atende matendo mema, wala asimshirikishe yeyote katika ibada ya Mola wake Mlezi." (Al-Kahf: 110) Na maana ya "mema" ni matendo sahihi na yanayokubaliana na Sunna ya Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake.

Kuharamisha kuzua

Mwenye kuzua ibada isiyotokana na Sunnah ya Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, na akataka kumwabudu Mwenyezi Mungu kwayo, kama vile mtu anayezua Swala ambayo si kwa namna yake ya kisheria, basi amekiuka amri ya Nabii rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, na anapata dhambi kwa hilo tendo, na atarudishiwa tendo lake hilo. Amesema rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, "Basi na watahadhari wale wanaohalifu amri yake, isije ikawapata fitina au ikawapata adhabu chungu." (An-Nur: 63). Na akasema Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: “Mwenye kuzua katika jambo letu hili yale yasiyokuwamo, basi hilo litakataliwa.” (Bukhari 2697, Muslim 1718)

Kumpenda yeye - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake

Katika yale yanayolazimiana na kumwamini Nabii rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, ni kwamba awe Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndio vipenzi zaidi kwa Muumini kuliko kila kitu. Kama alivyosema Nabii rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, “Haamini mmoja wenu mpaka niwe kipenzi zaidi kwake kuliko baba yake, na mwanawe, na watu wote.” (Bukhari 15, Muslim 44)

Umemaliza somo kwa ufanisi


Anza mtihani