Endelea kujifunza

Umeshaingia
Jisajili sasa kwenye jukwaa la Taa ili uanze kujifunza, na fuatialia maendeleo yako, na kukusanya pointi, na uingie kwenye mashindano.Baada ya kujisajili, utapata cheti cha kielektroniki katika mada ambazo utajifunza.

Sehemu ya sasa:

Somo Kumjua Nabii - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake

Mwenyezi Mungu alimtuma Mtume wetu Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, - kwa watu wote kwa jinsia zao zote na jamii zao zote. Katika somo hili, kuna ufafanuzi mfupi wa Nabii - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake.

  • Kuyajua kwa ufupi maisha ya Nabii Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake.
  • Kujua cheo cha Nabii - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake.

Jina la Nabii wetu - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake

Jina lake ni Muhammad bin Abdullah bin Abdul Muttalib bin Hashim Al-Qurashi. Naye ndiye mbora wa Waarabu kwa nasaba, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake.

Ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa watu wote

Mwenyezi Mungu alimtuma Mtume wetu Muhammad, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, kwa watu wote, jinsia zao zote, na jamii zao zote, na akawajibisha kwa watu wote kumwamini, na kumtii. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema,"Sema: Enyi watu! Hakika, mimi ni Mtume Mwenyezi Mungu kwenu nyinyi nyote."(Al-A’raf: 158)

Qur-ani iliteremshwa kwake

Mwenyezi Mungu aliteremshia Muhammad, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, Kitabu chake kitukufu zaidi, ambacho ni Qur-ani, ambayo haijiwi na upotovu wowote mbele yake wala nyuma yake.

Mwisho wa Manabii na Mitume

Mwenyezi Mungu alimtuma Muhammad, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, kama mwisho wa Manabii, basi hakuna Nabii yeyote atakayekuja baada yake. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu, "Bali ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na mwisho wa Manabii. (Al-Ahzab: 40)

1- Kuzaliwa kwake - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake

Alizaliwa Makka katika Mwaka wa Tembo (571 AD), akiwa yatima wa baba. Na alimpoteza mama yake katika umri mdogo, hivyo basi akalelewa chini ya uangalizi wa babu yake, Abdul-Muttalib, kisha baada yake katika uangalizi wa ami yake, Abu Talib ambaye alimlinda na kumtetea.

2- Maisha yake na malezi yake - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake

Aliishi katika kabila lake la Quraish kwa muda wa miaka arobaini kabla ya Unabii, (571-611 AD) ambapo alikuwa mfano mzuri wa maadili na akapigiwa mfano katika kunyooka na kuwa wa kipekee. Jina lake la utani mashuhuri miongoni mwao lilikuwa ni As-Sadiq Al-Amin (mkweli, mwaminifu). Na alikuwa akifanya kazi ya kuwachunga wanyama, kisha akafanya biashara. Mtume wa Mwenyezi Mungu kabla ya Uislamu alikuwa mnyoofu akimwabudu Mwenyezi Mungu kwa mila ya Ibrahim, na anakataa ibada ya masanamu na matendo ya kipagani.

3- Kutumwa kwake - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake

Baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - kukamilisha miaka arobaini katika umri wake, na alipokuwa akitafakari na kumuabudu Mwenyezi Mungu katika pango la Hira katika Jabal An-Nur, ulimjia Wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Na Qur-ani ikaanza kuteremka kwake. Na lilikuwa jambo la kwanza lililoteremka kwake katika Qur-ani ni kauli yake Mwenyezi Mungu, "Soma kwa jina la Mola wako Mlezi ambaye aliumba." (Al-Alaq: 1). Ili kutangaza kwamba kutumwa huku tangu mwanzo wake ni zama mpya ya elimu, na kusoma, na nuru na mwongozo kwa watu. Kisha Qur-ani ikaendelea kuteremshwa kwake kwa muda wa miaka ishirini na mitatu.

4- Mwanzo wa kulingania kwake - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake

Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - aliilingania dini ya Mwenyezi Mungu kwa siri kwa muda wa miaka mitatu, kisha akaudhihirisha mwito huo na kuuweka hadharani kwa muda wa miaka kumi mingine. Mtume wa Mwenyezi Mungu na maswahaba zake walipata ndani yake aina kali zaidi za mateso na dhuluma kutoka kwa kabila lake la Qureshi. Kwa hivyo, akaupeleka Uislamu kwa makabila yanayokuja kuhiji, kwa hivyo watu wa Madina wakaukubali, na kuhama kwa Waislamu kukaanza kidogo kidogo.

5-Kuhama kwake - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake

Nabii - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - alihamia Madina iliyotiwa nuru, ambayo wakati huo iliitwa Yathrib, mwaka wa 622 AD alipokuwa na umri wa miaka hamsini na mitatu, baada ya kufanyiwa njama na viongozi wa Maquraishi miongoni mwa wale walioupinga wito wake na wakafanya juhudi kumuua. Aliishi huko kwa muda wa miaka kumi, akiulingania Uislamu, na akaamrisha Swala, na Zaka, na sheria nyinginezo za Uislamu.

6- Kuieneza kwake - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake Uislamu

Mtume wa Mwenyezi Mungu aliasisi kiini cha ustaarabu wa Kiislamu kule Madina baada ya kuhama kwake (622 AD), na akaimarisha sifa za umma wa Kiislamu. Basi akaondoa utetezi batili wa kikabila wa kijahilia, na akaeneza elimu. Na akaimarisha kanuni za uadilifu, unyoofu, undugu, na ushirikiano juu ya wema na uchamungu. Baadhi ya makabila yalijaribu kuuondoa Uislamu, kwa hivyo vita na matukio kadhaa yakatokea, na Mwenyezi Mungu akaipatia ushindi dini yake na Mtume wake. Kisha watu kukaendelea kuingia kwa watu katika Uislamu. Kwa hivyo, Makka na aghalabu ya miji na makabila katika Bara Arabu wakaingia katika Uislamu kwa hiari, wakiwa wameridhika na dini hii kubwa.

7- Kifo chake - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake

Katika Safar mwaka wa 11 wa kuhama kwa Mtume, na baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu kufikisha ujumbe na kutekeleza amana, na Mwenyezi Mungu akakamilisha baraka zake juu ya watu kwa kukamilisha dini. Nabii - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - alipatwa na homa, na maradhi yakamlemea mpaka alipokufa, - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, - mchana wa siku ya Jumatatu, tarehe kumi na mbili Rabi' al-Awwal mnamo mwaka wa 11 Hijiria sambamba na (8/ 6/632 AD), hali ya kuwa ametimiza miaka sitini na mitatu. Na alizikwa katika chumba cha 'Aisha Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, kwenye upande wa Msikiti wa Mtume.

Umemaliza somo kwa ufanisi


Anza mtihani