Ibada mbalimbali
Tawi hili linalenga kusimamisha misingi ya ibada na kuiimarisha, na kufungamanisha ibada na hukumu zake na Kitabu kitukufu na Sunna za Mtume zilizo safi. Linajumuisha ufahamu wa kina wa ibada (Fiqhi) na hukumu za ibada alizoamrishwa mwanadamu kwa kuzibainisha na kuzieleza, kama zilivyopokewa kutoka kwa Nabii Muhammad, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, na kutoka kwa maswahaba wake, Mwenyezi Mungu awe radhi nao wote.
mada ndogo ndogo
Twahara
Swala ndiyo nguzo ya pili ya Uislamu baada ya shahada mbili. Na kwa vile swala haikubaliki bila ya twahara, ikawa inafaa zaidi kwa mwanafunzi kujifunza kwanza hukumu za twahara ili swala yake iwe sahihi.
Swala
Swala ndiyo msingi wa dini na ndiyo ibada muhimu sana ambayo mtu lazima aanze nayo katika kujifunza kwake. Ni nguzo ya pili ya dini ya Kiislamu baada ya Shahada, na Uislamu wa mtu haukamiliki isipokuwa kwa kuitekeleza.
Zaka
Zaka ni nguzo ya tatu ya Uislamu. Mwenyezi Mungu aliifaradhisha ili imtakase na kumsafisha mtoaji na mchukuaji. Ingawa inaonekana kwa dhahiri kwamba ni kupunguza kiwango cha mali, lakini katika athari zake ni kuongezeka kwa baraka katika mali, kuongezeka kwa kiasi chake na kuongezeka kwa imani katika moyo wa mwenye kuitoa.
Kufunga saumu
Kufunga saumu katika Ramadhani ni nguzo ya nne ya Uislamu. Na kufunga saumu ni ibada ya heshima aliyoifaradhisha Mwenyezi Mungu juu ya waislamu, kama alivyoifaradhisha juu ya umma waliotangulia ili kufikia uchamungu, ambao ndio ufunguo wa heri yote.
Hijja
Hijja ni nguzo ya tano ya Uislamu. Muislamu mzima mwenye uwezo analazimika kuhiji mara moja maishani mwake.
Kifo na mazishi
Kifo siyo mwisho wa jambo la maisha, bali ni awamu mpya kwa mtu na mwanzo wa maisha kamili ya akhera. Kama vile Uislamu ulivyokuwa na nia ya kulinda haki mbalimbali tangu kuzaliwa, pia ulisisitiza juu ya hukumu zinazohifadhi haki za maiti na kuzingatia hali ya familia yake na jamaa zake.