Matukio mbalimbali
Uislamu ni dini yenye kujumuisha kila kitu ambacho ni kizuri kwa mwanadamu, na ni ujumbe wa jumla kwa mwanadamu popote alipo na wakati wowote ule. Kama vile ni yenye kujumuisha na ya jumla, basi ni nzuri katika kila mahali na wakati. Sehemu hii inajumuisha mada zilizochaguliwa ambazo Waislamu wanazihitaji katika hali za matukio mbalimbali.
mada ndogo ndogo
Sheria mbalimbali za msimu wa baridi
Uislamu ni dini yenye kujumuisha na inafanya maisha yote kufungamana na Muumba wake, yenye malengo ya juu sana, yenye hekima katika sheria zake mbalimbali. Ndiyo maana Muumini ana ibada inayomuongoza kufikia hilo katika kila wakati. Msimu wa baridi ni msimu ambao hauwezi kukosa hukumu mbalimbali za kisheria zinazohusiana na milango kadhaa, katika usafi, swala, mavazi, mvua na mengineyo. Katika mlango huu, tutashughulikia kwa idhini ya Mwenyezi Mungu baadhi ya hukumu zake.
Hukumu za Safari
Uislamu ni dini ya maisha; kwani inafungamana na hali zote za mwanadamu, katika kukaa kwake nyumbani na kusafiri kwake, katika kutulia kwake na harakati zake, katika hali ya utani na hali isiyokuwa na utani. Na safari ni miongoni mwa maisha haya ya kijamii. Nazo hazikosi hukumu za vitu ambavyo Mwenyezi Mungu Mtukufu anataka tuvikumbuke na kuvifanya, au mambo ambayo Mwenyezi Mungu anataka tuyaepuke na tuyaache. Mwenyezi Mungu akipenda, tutajifunza katika sehemu hii baadhi ya hukumu za safari.
Mlipuko wa magonjwa na ugonjwa wa kawaida
Janga la magonjwa ni moja ya majaliwa ya Mwenyezi Mungu yanayoteremka juu ya watu, Waislamu wao na makafiri wao. Lakini hali ya Muislamu anapokuwa katika balaa (janga) si sawa na ile ya wengineo; kwani yeye huamiliana nayo kwa yale ambayo Mola wake Mlezi Mtukufu aliamuru, kama vile kuwa na subira na kufanya sababu za kisheria za kuizuia kabla ya kutokea kwake, na kutafuta tiba baada ya kushikiwa nayo.