Njia za kujifunza
Jukwaa la Taa lina Njia mbalimbali za kujifunza. Kila njia ina masomo yaliyochaguliwa kutoka vitengo mbalimbali vya tovuti ili kusaidia kujenga maarifa ya kisheria ya mwanafunzi kulingana na mahitaji yake.
Mambo ambayo Mwislamu hapaswi kutojua
Sheria ilikuja na hukumu zinazowapasa Waislamu wote kujifunza na kuzifanyia kazi. Hukumu hizi ni nyepesi na zilirahisishwa. Kwani, Sheria ya Kiislamu imejengwa juu ya kuleta masilahi na kuzuia maovu. Vile vile, hukumu hizi zinatofautiana na zinginezo kwa sababu chanzo chake ni cha kimungu, cha kimola, na kwamba yule aliyezibainisha kwa watu ndiye mjuzi zaidi wa watu, mfansaha zaidi wa lugha na mwenye kunasihi zaidi kwa umma wake, ambaye ni Nabii Muhammad, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. Katika njia hii, kuna kundi la masomo yaliyochaguliwa, ambayo yanamfunza Mwislamu hukumu mbalimbali za kisheria ambazo hawezikosa kuzihitaji kuzijua na kuzifanyia kazi.
Mwislamu mpya
Kwa kuingia katika Uislamu, mtu huanza safari katika maisha haya ya dunia ambayo ni tofauti na kila kitu kilichopita katika umri wake. Katika safari hii, atahitaji idadi kubwa ya maarifa na elimu ili aweze kusahihisha kwayo imani yake na kuihifadhi, kutekeleza majukumu ambayo Mwenyezi Mungu amemfaradhishia na kupanda katika daraja za imani na Uislamu kidogo kidogo. Tayari tumeshamkusanyia katika njia hii yale yanayofikia lengo hili, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.
Miamala ya kimali
Dini ya Uislamu ni Dini inayojumuisha nyanja zote za maisha. Kwani, ni dini ya ibada na pia ni ya miamala. Waja wanahitaji kile kinachowaongoza kujua hukumu za sheria ya Kiislamu katika hayo yote, ili matendo yao yawe kulingana na yale ambayo Mwenyezi Mungu anayapenda na anayaridhia. Qur-ani Tukufu imejumuisha maelezo ya kina yanayohusiana na miamala na mikataba. Naye Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, aliwabainishia umma wake kile wanachohitaji katika hukumu za mauziano na miamala mingine ya kimali. Tutaeleza baadhi ya hayo katika njia hii.
Familia ya Kiislamu
Uislamu uliipa familia mazingatio makubwa na uangalizi kamili. Kwani, Sheria imejengeka juu ya kuwaongoza waja kwenye masilahi ya maisha haya na ya akhera. Jamii haiwezi kutengenea isipokuwa kwa kutengenea kwa familia ambazo inajengeka kwazo. Sheria ilikuja na hukumu za kina, adabu za juu, na mfumo bora sana unaojenga familia na kuzihifadhi. Kwa hivyo, sheria hii ilibainisha wajibu wa kila mwanafamilia kama vile ilivyobainisha haki zake.
Mwanamke wa Kiislamu
Sheria ya Kiislamu ilikuja kwa ajili ya kuwatukuza wanawake, na ushahidi wa hilo ulioko katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu na maisha ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, ni nyingi sana. Katika kumtukuza mwanamke katika Uislamu ni kwamba Uislamu umemuwekea hukumu za kisheria ambazo zinazingatia sifa zake na mambo yake mahususi, kuhifadhi haki zake, kumlinda kutokana na mambo machafu, na matamanio ya wenye nia mbaya na wale wenye magonjwa mioyoni mwao.