Jisajili sasa kwenye jukwaa la Taa ili uanze kujifunza, na fuatialia maendeleo yako, na kukusanya pointi, na uingie kwenye mashindano.Baada ya kujisajili, utapata cheti cha kielektroniki katika mada ambazo utajifunza.
Kutafuta elimu ni miongoni mwa ibada kubwa kabisa, na kujiondolea ujinga ni miongoni mwa faradhi za lazima. Na kupata ufahamu katika dini ni miongoni mwa matendo yanayomridhisha Mola Mlezi wa walimwengu wote. Amesema Nabii - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - , "Kutafuta elimu ni wajibu kwa kila Muislamu". (Ilipokewa na Imam Ahmad). Na akasema Nabii - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, "Yule ambaye Mwenyezi Mungu anamtakia heri, humpa ufahamu katika dini." (Ilipokewa na Muslim). Na kwenye jukwaa la Taa, utapata uzoefu wa kipekee, rahisi, na wa kufurahisha wa kujifunza unaokuwezesha kupata maarifa mengi ya kisheria yatakayokufaidi wewe hapa duniani na Akhera.