Sehemu ya sasa:
Somo Fadhila za Makka na Msikiti Mtakatifu
Fadhila za Makka takatifu: Mji huu mzuri una mahali pakubwa na fadhila nyingi, na miongoni mwake ni:
Abdullah bin 'Adiy bin al-Hamra, Mwenyezi Mungu amridhie, alisema: Nilimwona Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, amesimama juu ya al-Hazura na akasema, "Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu, hakika wewe ndiyo nchi ya Mwenyezi Mungu iliyo bora zaidi, na ardhi ya Mwenyezi Mungu pendwa zaidi kwa Mwenyezi Mungu. Na kama nisingetolewa kutoka ndani yako, nisingetoka." (Tirmidhi 3925) Na katika riwaya nyingine: "Na ardhi ya Mwenyezi Mungu ambayo ndiyo pendwa zaidi kwangu." (Ibn Majah 3108)
2. Ni patakatifu (haram) pa Mwenyezi Mungu
Mwenyezi Mungu ameharamisha juu ya viumbe vyake kumwaga damu ndani yake, au kumdhulumu yeyote ndani yake, au kuwinda mawindo ndani yake, au kukata miti yake na nyasi zake.
Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, alisema: “Hakika Makka ameiharamisha Mwenyezi Mungu na wala siyo watu walioiharamisha. Kwa hivyo, si halali kwa mtu yeyote anayemwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho kumwaga damu ndani yake wala kukata mti humo." (Bukhari 104, Muslim 1354)
Alisema swahaba mtukufu Abu Dharr al-Ghafari, Mwenyezi Mungu amridhie, kwamba: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Ni msikiti gani uliwekwa katika ardhi wa kwanza? Akasema: "Mskikiti mtakatifu." Nikasema: Halafu upi? Akasema: "Msikiti wa Al-Aqsa." Nikasema: Ni muda gani ulikuwa kati yake? Akasema: "Miaka arobaini. Na popote itakapokupata swala, basi wewe swalia hapo, kwani hapo ni msikiti." (Bukhari 3366, Muslim 520)
2. Kwamba kuna Ka'aba tukufu ndani yake:
Ka'aba ni jengo la umbo la mche mraba ambayo iko katikati ya ua la Msikiti mtakatifu. Hii ndiyo kibla ambayo Waislamu huelekea, mashariki na magharibi mwa dunia katika swala zao zote. Ilijengwa na Ibrahim, mwandani wa Mwenyezi Mungu na mwanawe Ismail, rehema na amani ziwe juu yao, kwa amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, kisha ikarekebishwa mara kwa mara. Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema, "Na kumbukeni Ibrahim na Ismail walipoinyanyua misingi ya ile Nyumba, wakaomba: "Ewe Mola wetu Mlezi, tukubalie! Hakika Wewe ndiye Msikizi, Ajuaye zaidi." [Al-Baqarah: 127] Na Maquraishi walikubali kwamba Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, ndiye anayefailia kuliweka lile jiwe jeusi mahali pake walipoijenga upya.
3. Kuongezwa maradufu malipo ya kuswalia ndani yake:
Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie alisema: “Swala katika msikiti wangu ni bora kuliko swala elfu moja katika misikiti mingineyo, isipokuwa Msikiti Mtakatifu. Na swala katika Msikiti mtakatifu ni bora kuliko swala laki moja katika misikiti mingineyo."(Ibn Majah 1406, Ahmad 14694)
4. Kwamba Mwenyezi Mungu aliwajibisha kwenda Hija kwenye Nyumba yake takatifu kwa mwenye uwezo wa kuifikia:
Ibrahim, amani imshukie, aliwanadi watu kwamba wahiji. Kwa hivyo watu wakamjia kutoka kila mahali, na manabii, amani iwashukie pia wakahiji huko. Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alisema: Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema akijulisha alivyomuamrisha Ibrahim, "Na watangazie watu Hijja; watakujia kwa miguu na juu ya kila ngamia aliyekonda, wakija kutoka katika kila njia ya mbali." (Al-Hajj: 27)