Sehemu ya sasa:
Somo Adabu za posa
Posa ni mwanamume kumjulisha mlezi wa mwanamke kwamba anataka kumuoa kwa mujibu wa Sunna ya Mwenyezi Mungu, na Sunnah ya Mtume wake - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake.
Miongoni mwa neema za Mwenyezi Mungu Mtukufu ni kwamba aliiwekea posa adabu ambazo kwazo inapatikana ridhaa na uchaguzi mzuri na utulivu, na zinasaidia kila mmoja wao kupatana na kukubaliana na mwenzake.
Miongoni mwa adabu za posa
1- Muislamu asipose juu ya posa ya Muislamu mwingine. Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - alisema, "Mtu asiuze juu ya mauzo ya ndugu yake, wala asipose juu ya posa ya ndugu yake, isipokuwa ikiwa atampa ruhusa." (Al-Bukhari 5142, Muslim 1412)
2- Kumtazama aliyechumbiwa kwa njia itakayomfanya amuowe. Mtume rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie alimwambia Mughira bin Shu'bah alipotaka kuposa, "Mwangalie. Kwani hilo linasaidia zaidi katika kuwafanya kupendana zaidi."(Tirmidhi 1087) Kumtazama mchumba pia ni haki ya wanawake. Bali baadhi ya wanazuoni walidai kwamba mwanamke ndiye anayestahili zaidi kufanya hivyo. Na maana ya kudumu baina yenu ni, mapenzi kuendelea kati yao.
Imesimuliwa kutoka kwa Jabir bin Abdullah kuwa alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - alisema, "Mmoja wenu anapomposa mwanamke, ikiwa anaweza kuangalia kinachoitia kumuoa, basi na afanye hivyo." Alisema: Basi nikamposa msichana mmoja, kwa hivyo nikawa ninamuangalia kisiri hadi nikaona kwake kilichoniitia kumuoa, kwa hivyo nikamuoa. (Abu Dawud 2082)
Miongoni mwa adabu za kumtazama yule anayetaka kuposwa
3. Miongoni mwa maadili muhimu zaidi ya posa ni kwamba kila mmoja wao: mwanaume na mwanamke afanye uchaguzi wake vizuri, na wategemee misingi sahihi ambayo itaanzisha nyumba yenye utulivu mwingi kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.
4. Miongoni mwa adabu za posa ni kwamba mwanamume afanye bidii kumuoa mwanamke mwenye kuzaa sana ili wazidishe uzao mwema. Kama alivyosema Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie: - "Oeni wapendezao, wanaozaa sana. Kwa maana, mimi nitazidi umma nyingine kwa wingi wenu." (Abu Dawud 2050)
5. Kutafuta ushauri wa watu, na ushauri wa Mwenyezi Mungu, na dua. Kwa maana, Muislamu anamuomba Mola wake Mlezi ushauri na anamuomba dua, na anatafuta ushauri wa watu wenye ufahamu na uelekezi mzuri katika mambo yote. Uamuzi wa kuoa ni uamuzi muhimu katika maisha ya binadamu, na hilo linafailia zaidi kutanguliwa na suala la kutafuta ushauri unaofaa, na kumuomba Mwenyezi Mungu umuamulie.
6. Wahusika hao wawili lazima wawe katika kiwango cha juu cha uwazi na ukweli katika kuelezea mambo na hali zote, bila kuficha kasoro yoyote, au kudanganya kwa makusudi au kuficha ukweli katika mambo yatakayoathiri uhusiano kati ya wahusika hawa wawili katika siku zijazo baada ya kuoana.
7. Kuzingatia hukumu za kisheria na mambo ya kisheria yanayodhibiti posa. Kwani hiyo ni kutoa ahadi tu ya kuoa, na siyo kuoa kwenyewe. Kwa hivyo hairuhusiwi kusalimiana mikononi, wala kukaa faraghani, wala kuzungumza kwa njia ya uvunjifu au kutia manukato na kujipamba kwa ajili ya anayeposa.