Endelea kujifunza

Umeshaingia
Jisajili sasa kwenye jukwaa la Taa ili uanze kujifunza, na fuatialia maendeleo yako, na kukusanya pointi, na uingie kwenye mashindano.Baada ya kujisajili, utapata cheti cha kielektroniki katika mada ambazo utajifunza.

Sehemu ya sasa:

Somo Kuunga jamaa

Katika somo hili, tutajifunza kuhusu maana ya kuunga jamaa katika Uislamu, na baadhi ya masuala yanayohusiana na hilo.

  • Kujifunza kuhusu maana ya kuunga jamaa katika Uislamu.
  • Kubainisha umuhimu wa kuunga jamaa na kutahadharisha dhidi ya kuwakata.
  • Kubainisha baadhi ya njia za kuunga jamaa.
  • Kubainisha baadhi ya fadhila za kuunga jamaa.

Maana ya kuunga jamaa

Ni kuwashirikisha jamaa katika matendo mema, kuwafanyia wema, kuwahurumia, kuwafanyia upole, kuwatembelea, kuwajulia hali zao na kuwapa matumizi wanaohitaji miongoni mwao.

Maandiko ya Qur-ani Tukufu na Sunna za Mtume yalikuja yakisisitiza suala la kuunga jamaa na kukataza kuwakata jamaa. Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema akiwaelezea makafiri, "Wale wanaovunja ahadi ya Mwenyezi Mungu baada ya kwisha kuifunga, na wakayakata yale aliyoamrisha Mwenyezi Mungu kuungwa, na wakafanya uharibifu katika nchi; hao ndio wenye hasara. [Al-Baqarah: 27] Pia alisema, "Basi yanayotarajiwa kwenu mkitawala ndiyo mtafanya uharibifu katika nchi na muwatupe jamaa zenu?" [Muhammad: 22]

Nabii - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - alisema, "Yeyote anayemuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho, na aunge jamaa zake." (Al-Bukhari 6138) Pia alisema, "Hakika Mwenyezi Mungu aliumba viumbe, mpaka alipokamilisha uumbaji wake, tumbo la uzazi likasema, 'Hapa ni mahali pa yule anayejilinda kwako kutokana kukatwa.' Akasema, "Ndiyo. Je, huridhii kwamba nimuunge mwenye kukuunga, na nimkate mwenye kukukata?" Likasema, "Ndiyo, ewe Mola Mlezi" Akasema, "Basi hilo ni lako." Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - alisema, "Basi someni mkitaka: Basi je, yanayotarajiwa kwenu mkitawala ndiyo mtafanya uharibifu katika nchi na mwatupe jamaa zenu?" [Muhammad: 22] (Al-Bukhari 5987, Muslim 2554)

Sheri'a iliamuru kuunga jamaa kulingana na ukoo na uhusiano.

Kuunga jamaa kwa wajibu

Ni kuunga jamaa, kama vile wazazi, wana wa kiume na mabinti, kaka na dada, ami, wajomba, shangazi na dada ya mama.

Kuunga jamaa kunakopendekezwa

Ni kuunga jamaa wasiokuwa maharimu, kama vile wana wa ami na wana wa dada ya mama.

Jinsi ya kuunga jamaa

Kuunga jamaa kunakuwa kwa kuwafanyia heri iwezekanavyo, na kuwazuilia uovu iwezekanavyo kulingana na uwezo wa mtu. Inaweza kuwa kwa kutoa salamu na hata kwa kuzungumza, au kwa mali na kutoa msaada unapohitajika, au kuzuilia madhara, au kuwa mchangamfu usoni, au kuwaombea dua, au mengineyo.

Mifano ya kuunga jamaa

١
Kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi kwa simu au kupitia programu za intaneti.
٢
Kutoa mali kwa ajili ya matumizi ya wajibu au kuwapa Zaka wale ambao si majukumu ya mtu huyu kuwalea, au kwa kuwapa sadaka, au zawadi, au kuwalea, au kuwaandikia wasia.
٣
Kushirikiana nao katika mambo ya furaha, na kuwafariji katika huzuni
٤
Kuwatembelea
٥
Kuitikia mwaliko
٦
Kumtembelea mgonjwa
٧
Kufuata jeneza ya mmoja wao
٨
Kutengeneza mahusiano kati yao

Miongoni mwa fadhila za kuunga jamaa

١
Ni sababu ya kuwapenda jamaa na kuimarisha uhusiano wa kifamilia kati yao.
٢
Kunapanua riziki na kunaongeza umri.
٣
Kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu humuunga mwenye kuunga jamaa.
٤
Kwamba ni sababu ya kuingia Peponi.
٥
Kwamba ndani yake kuna kumtii Mwenyezi Mungu, na kupata ridhaa yake.

1- Ni sababu ya jamaa kupendana na kuimarisha uhusiano wa kifamilia

Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - alisema, "Jifunzeni katika nasaba zenu kile mtakachounga kwacho jamaa zenu. Kwani kuunga jamaa kunaleta upendo katika familia, kunazidisha mali, kunarefusha athari za mtu." (Tirmidhi 1979)

2- Kupanua maisha na kuongeza umri

Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - amesema, “Anayefurahishwa kwamba apanuliwe katika riziki yake, au arefushiwe katika athari zake, basi na awaunge jamaa zake.” (Al-Bukhari 2067, Muslim 2557)

3. Kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu humuunga mwenye kuunga jamaa

Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - amesema, "Hakika Mwenyezi Mungu aliumba viumbe, mpaka alipokamilisha uumbaji wake, tumbo la uzazi likasema, 'Hapa nipo katika mahali pa anayejilinda na Wewe kutokana na kukatwa.' Akasema, 'Ndiyo. Je, huridhii kwamba nimuunge mwenye kukuunga, na nimkate mwenye kukukata?" Tumbo la uzazi likasema, 'Ndiyo, Mola Mlezi.' Akasema, 'Basi unalo hilo.'"(Al-Bukhari 5987, Muslim 2554)

4- Kuunga jamaa ni sababu ya kuingia Peponi

Mwanamume mmoja alimuuliza Nabii - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - kuhusu matendo ambayo yatamuingiza Peponi, naye akamwambia, "Umuabudu Mwenyezi Mungu na usimshirikishe na chochote, na usimamishe Swala, utoe Zaka, na uunge jamaa." (Al-Bukhari 1396, Muslim 13)

Umemaliza somo kwa ufanisi


Anza mtihani