Sehemu ya sasa:
Somo Adabu ya ndoa
Mbali na hukumu za kisheria zinazohusiana na ndoa, ambazo baadhi yake huwa kabla ya mkataba wa ndoa, na baadhi yake huwa wakati wa mkataba, na baadhi yake huwa baada yake, Uislamu umeizunguka ndoa kwa mkusanyiko wa adabu ambazo kila mmoja wa wanandoa anapaswa kudumisha; ili kupata thawabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kwa matumaini ya kuhifadhi nguvu na uimara wa uhusiano wa kindoa.
1. Nia
Niya ina nafasi kubwa katika Uislamu, kama inavyothibitishwa na hadithi hii maarufu, "Hakika matendo yanategemea niya tu, na hakika kila mtu atapata kile alichokusudia." (Al-Bukhari 1, na Muslim 1907) Kwa hivyo wanandoa wanapaswa kuwa na niya njema katika ndoa. Bali katika ufahamu mzuri ni kwamba wazidishe niya nzuri ili wazidishe thawabu zao. Na katika niya njema katika ndoa ni kuonyesha moja ya ishara za Mwenyezi Mungu, kufuata amri za kisheria zinazotakwa katika ndoa, kutumaini kwamba uzao mzuri utaibuka kutoka kwao ambao watampwekesha na kumuabudu Mwenyezi Mungu, kila mmoja wa wanandoa kumuweka safi mwenzake na kumlinda kutokana na majaribio, na mambo mengineyo.
2- Kufuata Sunna katika usiku wa kukutana kwa wanandoa
Karamu ya ndoa ni sunna iliyosisitizwa, kwa mujibu wa kauli yake Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, akimwambia ʻAbdur-Rahman bin ʻAwf, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, alipooa, “Fanya karamu walau kwa kondoo mmoja.” (Al-Bukhari 2048, Muslim 1427)
Kinachopasa kuzingatiwa kwenye karamu
4- Wanawake kuimba kwenye harusi
Inaruhusiwa kwa wanawake tu kuimba kwa maneno mazuri ambayo yanaruhusiwa na kupiga ngoma huku wakiwa mbali na wanaume, na bila ya kutumia vyombo vya muziki. Kwa maana, kuonyesha furaha katika hafla hii nzuri inaruhusiwa katika Uislamu.
5. Kuishi pamoja kwa wema
Miongoni mwa adabu za ndoa zinazosisitizwa ni kuishi pamoja kwa wema; ili udumu upendo, ambao wanandoa hao wataishi kwa huo maisha ya furaha, Mwenyezi Mungu Mtukufu akipenda. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Na kaeni nao kwa wema." (An-Nisaa: 19)