Endelea kujifunza

Umeshaingia
Jisajili sasa kwenye jukwaa la Taa ili uanze kujifunza, na fuatialia maendeleo yako, na kukusanya pointi, na uingie kwenye mashindano.Baada ya kujisajili, utapata cheti cha kielektroniki katika mada ambazo utajifunza.

Sehemu ya sasa:

Somo Swala zinazopendekezwa.

Swala za faradhi za mchana na usiku ni tano tu, lakini kuna swala ambazo inapendekezwa kwa Muislamu kuzitekeleza ili aongeze ukaribu wake kwa Mwenyezi Mungu, Mtukufu aliye juu. Katika somo hili, utajifunza kuhusu swala muhimu zaidi kati ya hizo zinazopendekezwa.

  • Kujifunza kuhusu Swala za sunna zilizoteuliwa.
  • Kujifunza kuhusu swala ya mvua.
  • Kujifunza kuhusu swala ya Istikhara.
  • Kujifunza kuhusu swala ya Dhuha.
  • Kujifunza kuhusu swala ya kupatwa jua.

Kila mchana na usiku, Mwislamu analazimika kuswali swala tano tu. Hata hivyo, sheria inamtaka Mwislamu kuswali swala zilizopendekezwa ambazo zitakuwa sababu ya Mwenyezi Mungu kumpenda mja, na zitakamilisha mapungufu ya swala zake za faradhi. Imesimuliwa kutoka kwa Abu Huraira, Mwenyezi Mungu amwiye radhi, kwamba Nabii - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - alisema, “Hakika, kitu cha kwanza ambacho watu watafanyiwa hesabu juu yake katika matendo yao Siku ya Kiyama ni Swala. Akasema: Mola wetu Mlezi Mtukufu Mwenye Nguvu atawaambia Malaika wake, na Yeye ndiye anayejua zaidi: Tazameni swala ya mja wangu, je, aliikamilisha au hakuikamilisha? Kwa hivyo, ikiwa ilikamilika, anaandikiwa swala kamili. Na kama hakikukamilika kitu kwayo, atasema, "Je, mja wangu ana swalah za kujitolea? Kama anazo swala za hiari, atasema, “Mtimizie mja wangu Swalah zake za faradhi kutoka katika Swala zake za hiari, kisha matendo mengine yote yatafanywa hivyo.” (Sunan Abi Dawud 864)

Swala maalumu za sunna

Zinaitwa hivyo kwa sababu haziachani na swala za faradhi, na zinafungamana nazo. Tena kwa sababu Mwislamu anashikamana nazo mara kwa mara.

Amesema Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, “Hakuna mja Mwislamu ambaye anamswalia Mwenyezi Mungu kila siku rakaa kumi na mbili kwa hiari yake, ambazo si za wajibu, isipokuwa Mwenyezi Mungu humjengea nyumba Peponi.” (Muslim 728)

Swala maalumu za sunna

١
Rakaa mbili kabla ya swala ya alfajiri
٢
Rakaa nne kabla ya swala ya adhuhuri, na atatoa salamu baada ya kila rakaa mbili, kisha rakaa mbili baada ya Swala ya Dhuhr.
٣
Rakaa mbili baada ya Swala ya Maghrib
٤
Rakaa mbili baada ya swala ya Isha

Witr

Swala hii inaitwa hivyo kwa sababu idadi ya rakaa zake haigawanyiki. Ni miongoni mwa Swala za sunna iliyo bora kabisa. Amesema Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, “Enyi watu wa Qur-ani, swalini Witr.” (Tirmidhi 453, Ibn Majah 1170)

Wakati wake mzuri zaidi ni masaa ya mwisho ya usiku. Lakini Mwislamu anaweza kuiswali wakati wowote kuanzia baada ya swala ya Isha hadi kuchomoza kwa alfajiri.

Idadi ya rakaa za swala ya Witr

Rakaa za chini zaidi za swala ya Witr ni rakaa moja. Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alikuwa akiswali Witr rakaa tatu, tano, saba, tisa na kumi na moja.

Namna ya kuswali Swala ya Witr

Idadi kamilifu zaidi ya Swala ya Witr ni rakaa tatu. Basi Mwislamu ataswali rakaa mbili na atoe salamu. Kisha ataswali rakaa moja kisha atoe salamu. Na inaruhusiwa kwake kisheria katika rakaa ya mwisho - kabla au baada ya rukuu, - kuinua mikono yake juu kufikia kwenye kifua chake kisha aombe dua ya Qunut.

Swala ya istisqaa (kuomba mvua inyeshe)

Ni swala iliyoamrishwa na Mwenyezi Mungu wakati ardhi inapokauka, na watu wakapatwa na madhara kwa sababu ya ukosefu wa mvua. Inaruhusiwa kisheria kuiswalia viwanja na mahali wazi ikiwezekana. Pia inaruhusika kuiswalia msikitini.

Inaruhusika kwa wale wanaoiswali watoke kuiendea kwa unyenyekevu, na kumlilia Mwenyezi Mungu huku wakitubia, na wanapaswa kuwa walifanya mambo ambayo yatawaletea rehema ya Mwenyezi Mungu, kama vile kuomba msamaha, kurudisha kilichochukuliwa kwa dhuluma, kutoa sadaka, kuwafanyia watu wema na mengineyo.

Namna ya kuswali Swala ya Istisqaa

Swala ya Istisqaa kama swala ya Idi, ni rakaa mbili ambazo imamu atasoma Qur-ani ndani yake kwa sauti kubwa. Inaruhisiwa kuongeza takbira mwanzoni mwa kila rakaa. Kwa hivyo atatoa takbira sita katika rakaa ya kwanza kabla ya kusoma, kando na takbira ya kufungulia swala (Takbiratul-Ihram), na takbira tano katika rakaa ya pili, kando na takbira ya kusimama kutoka kwenye sijda. Kisha atatoa khutba mbili ambamo ataomba msamaha kwa wingi, na kukakamia kumwomba Mwenyezi Mungu.

Swala ya Istikhara

Ni swala anayoruhusiwa Mwislamu anapotaka kufanya jambo linaloruhusiwa lakini hajui ikiwa kuna heri ndani yake au la.

Kukubalika kwake kisheria

Mwislamu anapoazimia kufanya jambo linaloruhusiwa lakini hajui ikiwa kuna heri ndani yake au la, basi inapendekezwa aswali rakaa mbili, kisha aombe baada yake dua iliyopendekezwa ambayo Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - aliwafundisha maswahaba wake, ambayo ni, “Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninakuomba muelekezo kwa elimu yako, na ninakuomba uniwezeshe kwa uwezo wako, na ninakuomba fadhila zako kubwa. Hakika wewe unaweza, nami siwezi. Nawe unajua, nami sijui. Nawe ndiye ajuaye zaidi wa yaliofichikana. Ewe Mwenyezi Mungu, iwapo jambo hili kutokana na elimu yako - (na alitaje jambo lake lenyewe) - lina heri kwangu katika dini yangu na maisha yangu na mwisho wa jambo langu, - au alisema karibu au mbali katika mambo yangu, - basi ninakuomba uniwezeshe nilipate. Na iwapo unajua kwamba jambo hili ni ovu kwangu katika dini yangu na maisha yangu na mwisho wa jambo langu - au alisema karibu au mbali katika mambo yangu, - basi liepushe na mimi, nami niepushe nalo, na nipangie jambo jingine lenye heri nami popote lilipo, kisha niridhishe kwalo.” (Al-Bukhari 6382)

Dua ya Swala ya Istikhara

Swala ya Dhuha

Ni miongoni mwa Swala zilizopendekezwa, ambazo zina malipo makubwa. Rakaa zake chache zaidi ni rakaa mbili, na wakati wake ni kuanzia jua linapoinuka baada ya kuchomoza kwake kwa kiasi cha mkuki, mpaka muda mfupi kabla ya jua kupindukia katikati ya mbingu muda mchache, kabla ya kuingia wakati wa swala ya Dhuhr.

Swala ya Kusuf (kupatwa jua na mwezi)

Kusuf ni hali ya kiulimwengu isiyo ya kawaida, ambapo mwanga wa jua au mwezi au sehemu yake hupunguka kabisa. Ni moja ya ishara za Mwenyezi Mungu zinazoonyesha uwezo wake na ufalme wake. Hali hii inamtanabahisha mtu na kumwamsha kutoka katika kughafilika kwake ili ahofu adhabu ya Mwenyezi Mungu na ataraji malipo yake.

Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, “Hakika, jua na mwezi havipatwi kwa kufa mtu yeyote katika watu, bali ni ishara mbili za Mwenyezi Mungu. Basi mkiziona, simameni na mswali.” (Bukhari 1041)

Namna ya kuswali swala ya Kusuf

Swala ya kupatwa jua au mwezi ni rakaa mbili, lakini imeruhusiwa kufanya rukuu mara mbili ndani yake. Kwa hivyo, baada ya mwenye kuswali kuinuka kutoka kwenye rukuu katika rakaa ya kwanza, atasoma tena Al-Fatiha na chochote kinachokuwa chepesi kwake katika Qur-ani, kisha atarukuu, kisha atainuka kutoka kwenye rukuu, kisha atasujudu sijda mbili. Na hii ni rakaa kamili. Baada ya kuinuka kutoka kwenye sijda, atafanya katika rakaa ya pili kama alivyofanya katika rakaa ya kwanza.

Umemaliza somo kwa ufanisi


Anza mtihani