Sehemu ya sasa:
Somo Swala ya msafiri na mgonjwa
Swala ni lazima kwa Muislamu katika hali zake zote maadamu ana akili na ufahamu wake, lakini Uislamu unazingatia hali na mahitaji tofauti ya watu, kama vile magonjwa na kusafiri.
Ni sunna kwa msafiri katika hali ya kusafiri kwake na kusita kwake katika safari kwa muda ulio chini ya siku nne, kufupisha swala za rakaa nne hadi rakaa mbili. Kwa hivyo, ataswali Dhuhr na Ishaa rakaa mbili mbili badala ya nne nne, isipokuwa ikiwa ataziswali pamoja na imamu asiyekuwa safarini, basi atamfuata katika swala yake na aswali rakaa nne kama yeye.
Msafiri anaruhusiwa kuacha Swala za sunna maalumu (sunan rawatib) isipokuwa zile rakaa mbili za sunna za kabla ya Swalatul-fajr. Na pia anaruhusiwa kudumisha swala ya Witr na Tahajjud.
Anaruhusiwa kuunganisha kati ya Dhuhr na Asr, na kati ya Maghrib na Isha katika wakati wa moja yake, haswa akiwa katika hali ya kusafiri kwake. Huu ni wepesishaji kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na rehema na kuondoa ugumu.
Kusimama kunakuwa si lazima kwa mgonjwa ambaye hawezi kusimama, au ikiwa kusimama ni kugumu kwake au kunaweza fanya asipone haraka, kwa hivyo anaweza swali akiwa amekaa. Na ikiwa hawezi, basi kwa ubavu wake. Amesema Mtume rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, "Swali ukiwa umesimama. Na ikiwa huwezi, basi kama umeketi. Na ikiwa huwezi, basi kwa ubavu." (Al-Bukhari 1117)