Endelea kujifunza

Umeshaingia
Jisajili sasa kwenye jukwaa la Taa ili uanze kujifunza, na fuatialia maendeleo yako, na kukusanya pointi, na uingie kwenye mashindano.Baada ya kujisajili, utapata cheti cha kielektroniki katika mada ambazo utajifunza.

Sehemu ya sasa:

Somo Makatazo ya Ihram

Yatakiwa kwa mwenye kuhiji au kufanya umra akiwa ndani ya ihram yake aepuke makatazo fulani. Utajifunza kuhusu hayo katika somo hili.

  • Kujifunza makatazo ya ihram.
  • Kujua hukumu zinazotokana na kufanya makatazo haya.

Makatazo ya Ihram

Ni kile ambacho mtu katika ihram amekatazwa kufanya kwa sababu ya Hija au Umra.

Makatazo ya ihram yamegawanyika katika sehemu tatu.

١
Baadhi yake yameharamishwa kwa wanaume na wanawake.
٢
Baadhi yake yameharamishwa kwa wanaume pekee.
٣
Baadhi yake yameharamishwa kwa wanawake pekee.

Miongoni mwa makatazo ya ihram kwa wanaume na wanawake:

١
Kunyoa au kupunguza nywele, pamoja na kukata kucha.
٢
Kutumia manukato sawa iwe kwenye nguo au mwili wake.
٣
Kujamiiana baina ya mume na mke wake, pamoja na kugusana na kupapasana kwa matamanio.
٤
Kufunga ndoa, sawa awe aliye katika ihram ni mwanamume au mwanamke.
٥
Amekatazwa aliye katika ihram kuwinda, kwa hivyo haruhusiwi kuwinda ndege na wanyama wa porini.

Miongoni mwa makatazo ya ihram kwa wanaume

١
Kuvaa nguo za kawaida zilizoshonwa, kama vile shati, nguo, suruali na mfano wa hizo.
٢
Kufunika kichwa kwa kitu kinachoshikana nacho. Ama chochote kinachofunika kichwa kama vile paa za majengo, vipando na mwavuli hivyo havina neno kuvitumia.

Miongoni mwa makatazo ya ihram kwa wanawake

١
Nikabu na kufunika uso. Imefaradhishwa kwake kufunua uso wake isipokuwa ikiwa wanaume wasiokuwa Mahrim wake watapita karibu naye, hapo anaweza kufunika uso wake na wala haitamdhuru ikiwa alichojifunika kwacho kitamgusa uso wake.
٢
Kuvaa glavu

Mwenye kufanya mojawapo ya makatazo haya kwa kusahau, kutojua au kulazimishwa, basi hakuna chochote kitakuwa juu yake. Hii ni kwa sababu ya kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Wala si lawama juu yenu kwa mlivyokosea. Lakini ipo lawama katika yale ziliyofanya nyoyo zenu kwa makusudi." (Al-Ahzab: 5) Lakini akikumbuka au akijua, basi itamlazimu aache katazo hilo papo hapo.

Yeyote atakayefanya kwa makusudi kitu ambacho kimekatazwa kwa udhuru anaoruhusiwa, basi inamlazimu kulipa fidia na wala hakuna dhambi juu yake.

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Wala msinyoe vichwa vyenu mpaka wanyama hao wafike machinjoni mwao. Na atakayekuwa mgonjwa au ana vya kumuudhi kichwani mwake, basi atoe fidia kwa kufunga au kwa kutoa sadaka au kuchinja wanyama. Na mtakapokuwa salama, basi mwenye kujistarehesha kwa kufanya Umra kisha ndio akahiji, basi achinje mnyama aliye mwepesi kumpata. Na asiyepata, afunge siku tatu katika Hija na siku saba mtakaporudi; hizi ni kumi kamili. Hayo ni kwa ajili ya yule ambaye watu wake hawako karibu na Msikiti Mtakatifu. Na mcheni Mwenyezi Mungu, na jueni Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu." (Al-baqara 196).

Mwenye kufanya kwa makusudi kitu ambacho kimekatazwa bila udhuru, basi analazimika kufidia na atapata dhambi kwa kosa lake.

Makatazo ya ihram, kwa kuzingatia fidia, yamegawanyika katika makundi manne:

١
Kwanza: Ni mambo yasiyokuwa na fidia, nalo ni kufunga ndoa.
٢
Pili: Mambo ambayo fidia yake ni ngamia, ambayo ni kujamiiana wakati wa Hija kabla ya kutoka kwa kwanza katika makatazo ya Hija.
٣
Tatu: Mambo ambayo fidia yake ni mfano wake au mbadala wake, ambayo ni kuua windo.
٤
Nne: Mambo ambayo fidia yake ni kufunga saumu, kutoa sadaka au kuchinja mnyama, ambayo ni kunyoa kichwa na vitu vingine vilivyoharamishwa isipokuwa vitatu vilivyotangulia hapo juu.

Umemaliza somo kwa ufanisi


Anza mtihani