Endelea kujifunza

Umeshaingia
Jisajili sasa kwenye jukwaa la Taa ili uanze kujifunza, na fuatialia maendeleo yako, na kukusanya pointi, na uingie kwenye mashindano.Baada ya kujisajili, utapata cheti cha kielektroniki katika mada ambazo utajifunza.

Sehemu ya sasa:

Somo Fadhila za Mtume Muhammad, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake.

Mwenyezi Mungu Mtukufu amempa Nabii wake, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, peke yake sifa na fadhila nyingi zinazofanya nyoyo zifungamane naye kwa kumpenda na kumpa taadhima. Katika somo hili, utajifunza kuhusu baadhi ya sifa na fadhila hizi.

  • Kujua baadhi ya sifa za Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, ili nyoyo zizidi kumpenda.

Sifa za Nabii Muhammad, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake

Mtume Muhammad, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, ndiye mwenye sifa na fadhila nzuri zaidi. Alipata sifa za hali ya juu zaidi, maadili mema, na tabia za kusifiwa. Na mwenye kutazama sifa zake, atapata kwamba yeye ndiye binadamu mkuu zaidi anayejulikana kwa wanadamu.

Yeye ndiye mja bora zaidi wa Mwenyezi Mungu na anayependeza zaidi kwa Mwenyezi Mungu, rafiki wake mwandani, mteule wake, ambaye ndiye mkamilifu zaidi miongoni mwa waja wa Mwenyezi Mungu katika ibada na mkatatifu zaidi katika tabia. Mwenye nafsi nzuri zaidi, mwenye miamala mizuri zaidi, anayemjua Mwenyezi Mungu zaidi na mwenye kutimiza zaidi uja kwake. Mwenyezi Mungu alimchagua ili awe Mtume wake na Nabii wake kwenda kwa viumbe vyake, na mpatanishi kati yake na watu katika kuelekeza kwenye heri na kulingania kwenye uwongofu.

Mwenyezi Mungu alimchagua kutoka katika nasaba bora zaidi na akampa sifa za kibinadamu kamili zaidi katika maumbile na maadili. Pia alimpa sifa kamili zaidi katika mwonekano wake mzuri, uzuri wake, maisha yake yanayong'aa, na sifa zake za juu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. Miongoni mwa sifa zake ni zifuatazo:

2. Sifa ya kimo cha Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake

١
Watu bora zaidi si wale ambao ni warefu sana au wafupi sana. Nabii alielekea upande wa urefu na hakuwa akitembea na mtu yeyote isipokuwa akikuwa mrefu kwake. Alikuwa anapoketi chini, bega lake linakuwa juu kuliko yule aliyeketi, na urefu wake na upana wake ulikuwa ukilingana sawa kabisa.
٢
Hakuwa mwembamba wala mnene. Tumbo lake lilikuwa sawa na kifua chake, na pande za kiuno chake hazikuwa zimechomoka nje wala nyembamba.
٣
Alikuwa ndiye mzuri zaidi wa watu wote kutokea mbali, na mtukufu na mzuri zaidi yao kutokea karibu.

Imesimuliwa kutoka kwa Anas ibn Malik, Mwenyezi Mungu amridhie, kwamba alimuelezea Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alisema: "Alikuwa wastani miongoni mwa watu. Hakuwa mrefu wala mfupi." (Al-Bukhari, 3547)

2. Sifa ya uso wake mtukufu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake

Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake alikuwa ndiye wa uso mzuri zaidi wa watu wote. Ulikuwa wa mviringo, lakini si mviringo sana. Bali ulikuwa na muonekano rahisi, mzuri sana, wenye mng'ao na urembo dhahiri. Ulikuwa uking'aa kama unavyong'aa mwezi usiku wa mwezi kamili. Kila mtu aliyemwona alikuwa anafarijika. Alikuwa anapofurahi, mistari ya paji la uso wake inang'aa. Na alikuwa na masikio kamilifu.

Sifa za uso wake, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake

١
Nyusi zake zilikuwa nyembamba na ndefu, zikienea hadi mwisho wa macho, huku zimejikunja na zikiungana sana kiasi kwamba hazionekani kwa mtu yeyote isipokuwa akizitazama kwa makini sana.
٢
Macho yake yalikuwa mapana, meupe sana katika sehemu yake nyeupe, meusi sana katika sehemu yake nyeusi, hayana kitu chochote kilifichikana katika weusi wake. Yalikuwa yamechanganyika na rangi nyekundu kutokana na mishipa miekundu myembamba sana iliyokuwa kwenye weupe wake. Alikuwa na kope ndefu kana kwamba amezipaka koholi.
٣
Pua yake ilikuwa wastani, yenye urefu mzuri, yenye pande zake mbili nzuri, iliyoinuka juu katika sehemu yake ya katikati, na yenye mwanga mkubwa.
٤
Mashavu yake yalikuwa madhubuti, yenye nyama chache, na ngozi nyembamba bila uvimbe wala mwinuko.
٥
Mdomo wake ulikuwa mpana, wenye midomo miwili miembamba. Meno yake yalikuwa meupe ya kung'aa, safi, na yenye umbali kati ya meno ya kukatia na machonge. Anapozungumza, nuru ingeonekana ikitokea kwenye meno yake madogo, na hakuwa akicheka ila tabasamu tu.
٦
Alikuwa mwenye shingo ndefu; na ilikuwa kama fedha katika usafi wake.

Alikuwa na ndevu nyingi nyeusi. Kulikuwa na nafasi inayoweza kuonekana kati ya kidevu chake na mdomo wake wa chini. Sehemu hiyo ilikuwa imeinuka, na ilikuwa na nywele inayotokana na ndevu zake kana kwamba ni ndevu zenyewe.

3. Rangi ya ngozi ya Mtume, rehema na amani ziwe juu yake

Imesimuliwa kutoka kwa Jubayr bin Mut’im, kutoka kwa Ali bin Abi Talib kuwa alisema akielezea namna alivyokuwa Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: “Alikuwa na umbo kubwa, mwenye rangi nyeupe iliyochanganyika na nyekundu, na mwenye ndevu nyingi.” (Musnad Ahmad 944)

4. Nywele za Nabii

Yeye, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alikuwa na nywele zenye kufikia nusu ya masikio yake wakati akizipunguza, na kama akiziachilia kurefuka zilikuwa zinnafikia kwenye mabega yake. Na hazikuwa zimekunjuka sana wala zilizokunjika, lakini zilikuwa baina ya hayo. Mara alikuwa akiziachilia juu ya paji la uso wake, na mara nyingine alikuwa akizipasua kwenye sehemu ya katikati ya kichwa chake bila ya kuacha chochote kwenye paji la uso wake.

Imesimuliwa kutoka kwa Qatada kuwa alisema: Nilimwambia Anas bin Malik, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi; "Nywele za Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake zilikuwa vipi?" Akasema: "Zilikuwa ni nywele za wastani, si zilizokunjuka wala za kujikunjakunja, na zilikuwa zikifikia baina ya masikio yake na shingo yake.” (Al-Bukhari 5905 na Muslim 2338)

Haukufikia mvi ishirini katika nywele zake na ndevu zake, nyingi yake ilikuwa kwenye ndevu zake kati ya kidevu chake na mdomo wa chini. Na mvi uliokuwa kichwani kwake ulikuwa kwenye sehemu aliyokuwa akipasulia nywele zake juu ya kichwa chake.

Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, alikuwa akizichana nywele zake, akizisafisha, na kuzifanya kuwa nzuri bila ya kuzidisha kiasi katika kujipamba na kujistarehesha kuhusiana na hilo. Alikuwa akianza na upande wa kulia.

5. Sifa za mabega yake, dhiraa yake na mikono ya Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake

١
Alikuwa na mabega mapana, kifua kipana na mgongo mpana, na kulikuwa na nywele nyingi juu ya mabega yake.
٢
Mgongo wake ulikuwa mweupe kana kwamba ni kipande cha fedha.
٣
Alikuwa na dhiraa ndefu na pana, viganja vikubwa, vidole virefu, mwenye sehemu kubwa ya kati ya kiganja na kiwiko. Sehemu hii ilikuwa ndefu bila ya uvimbe wowote, na alikuwa na nywele kwenye dhiraa yake. Viganja vyake vilikuwa vipana vilivyojaa nyama, na vilikuwa laini kuliko hariri licha ya ukubwa wake.

Imesimuliwa kutoka kwa Anas, Mwenyezi Mungu amuwie radhi, kuwa alisema: “Sikuwahi kugusa hariri wala dibaji laini zaidi kuliko kiganja cha Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake.” (Bukhari 3561, Muslim 2330)

6. Sifa za muhuri wa Unabii

Kulikuwa na muhuri wa unabii kwenye bega lake la kushoto. Nao ulikuwa ni kipande cha nyama kilichoinuka kilichofanana na rangi ya mwili wake, cha ukubwa wa yai la njiwa. Pembeni mwake kulikuwa na rangi tofauti na ya mwili wake, na juu yake kulikuwa na nywele zilizokusanywa pamoja.

Imesimuliwa kutoka kwa Jabir bin Samura, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, kuwa alisema: “Niliuona muhuri wa unabii wa Mtume kwenye bega lake kana kwamba ni yai la njiwa, na ulikuwa unafanana na mwili wake." (Muslim 2344)

7. Sifa za kifua na tumbo lake, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake

١
Alikuwa na kifua kipana.
٢
Tumbo lake lilikuwa kiwango sawa na kifua chake.
٣
Kiuno chake hakikuwa kimechomoza nje wala hakikuwa chembamba.
٤
Ilikuwa imeunganishwa kutoka chini ya koo hadi kwenye kitovu kwa nywele zinazokwenda kama mstari, na hakukuwa na nywele zingine kwenye kifua chake na tumbo lake zaidi ya hizo.
٥
Kwapa zake zilikuwa nyeupe bila nywele.

8. Sifa za miundi na miguu ya Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake

١
Alikuwa na miundi na miguu mirefu. Miundi yake ilifanana na moyo mororo wa mtende kwa sababu ya weupe wake, na ilikuwa mizuri sana na ya kung'aa.
٢
Alikuwa na miguu mikubwa, laini, isiyo na nyufa. Kidole cha shahada cha mguu wake kilikuwa kirefu zaidi kuliko vidole vingine.
٣
Ilikuwa na nyama kidogo.
٤
Miguu yake miwili ilikuwa na nafasi kwenye tumbo lake (yaani sehemu yake ya chini) na ilikuwa mbali sana na ardhi anapokanyaga.

9. Harufu ya Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake

Jasho lake lilinukia zaidi kuliko miski. Mtu angemsalimia mkononi, angeshinda siku nzima akiipata harufu hiyo. Na alikuwa akipaka manukato muda wake mwingi.

Imesimuliwa kutoka kwa Anas kuwa alisema: “Sikuwahi kunusa harufu ya miski wala manukato mazuri zaidi kuliko harufu ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. (Muslim 2330)

Maneno ya jumla katika kuelezea maadili yake adhimu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na hakika wewe una tabia tukufu." [Al-Qalam: 4] Jibril alipomjia Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, kwa mara ya kwanza, naye akapatwa na hofu, akamwambia Mama wa Waumini, Khadija, Mwenyezi Mungu amuwie radhi: “Hakika ninajihofia nafsi yangu.” Naye akamwambia: “Pata bishara njema. Wallahi! Mwenyezi Mungu hawezi kukuhizi abadani. Wallahi! Hakika wewe unaweka mahusiano mazuri na jamaa zako, na unasema kweli, na unawasaidia masikini, na unawasaidia wasiokuwa na chochote, na unawahudumia wageni wako kwa ukarimu, na unasaidia katika mambo ya haki." (Bukhari 4953, Muslim 160)

1. Uaminifu wa Mtume, rehema na amani Mwenyezi Mungu ziwe juu yake

Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alijulikana kwa uaminifu wake kiasi kwamba watu wake kabla ya utume walimwita “Mwaminifu” na licha ya uadui wao kwake baada ya utume, walikuwa wakimkabidhi amana zao.

2. Huruma na rehema zake, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake

Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alikuwa mpole mwenye huruma kwa umma wake. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: "Hakika amekwisha kujieni Mtume kutokana na nyinyi wenyewe; yanamhuzunisha yanayokutaabisheni; anakuhangaikieni sana. Kwa Waumini ni mpole na mwenye huruma." [Tawba: 128] Na amesema: "Basi ni kwa sababu ya rehema itokayo kwa Mwenyezi Mungu ndiyo umekuwa laini kwao. Na lau ungelikuwa mkali, mwenye moyo mgumu, bila ya shaka wangelikukimbia." [Al Imran: 159]

3. Msamaha wake na kuachilia kwake mbali, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake

Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alipoingia Makka akiwa amewashinda, viongozi wa Makka na watawala wake walisimama mbele yake kwa unyenyekevu, baada ya kuendelea kumfanyia uadui na kumdhuru yeye na masahaba zake kwa muda wa miaka kadhaa. Basi hakuwaambia isipokuwa: "Leo hapana lawama juu yenu. Nendeni, kwani mko huru."

4. Kukakamia kwake kuwaongoza viumbe

Alikuwa na shauku kubwa ya kuwaongoza watu kiasi kwamba alikaribia kujiangamiza kwa huzuni kwa ajili yao. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: “Huenda ukajihiliki nafsi yako kwa ajili yao, kuwasikitikia kwa kuwa hawayaamini mazungumzo haya!” [Al-Kahf: 6]

5. Ujasiri na nguvu zake, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake

Ali, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi - ambaye alikuwa mmoja wa mashujaa zaidi - alisema akielezea ushujaa wa Mtume rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: “Tulikuwa tunapokuwa katika vita na vikawa vikali zaidi, watu wakakutana na watu wengine, tungejikinga kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, kwa hivyo hawi yeyote miongoni mwetu karibu zaidi na adui hao kuliko yeye.” (Ahmad 1347)

Umemaliza somo kwa ufanisi


Anza mtihani