Sehemu ya sasa:
Somo Mapato machafu na miamala inayohusiana na mali iliyoharamishwa
Kuna kuchuma ambako ni kuzuri na halali, lakini pia kuna kuchuma ambako ni kuchafu na haramu. Mwenyezi Mungu amesema: "Enyi mlioamini! Toeni katika vile vizuri mlivyovichuma, na katika vile tulivyokutoleeni katika ardhi. Wala msikusudie kutoa vilivyo vibaya." [Al-Baqarah: 267]
Katika Hadith ya Abu Huraira, radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, Mtume rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, alisema: "Hakika zama zitawajia watu ambapo mtu hatajali ni wapi anapata (anachuma) mali yake; je, ni kwa njia ya halali au ya haramu?" (Al-Bukhari 2083)
Ni kula mali za watu kwa batili, au kuchuma kupitia njia ambayo imeharamishwa na Sheria.
Njia mbaya za kuchuma mali
Sababu za kujihusisha na mapato mabaya
Madhara ya mapato mabaya
Aina za vitu vilivyoharamishwa katika Miamala inayohusiana na mali
Vitu vyenyewe vilivyoharamishwa
Ni kila kitu kilichoharamishwa chenyewe, kama vile nyamafu, damu, nyama ya nguruwe, vitu vichafu na najisi na vinginevyo. Hivyo ni miongoni mwa mambo ambayo nafsi yenyewe haivipendi. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Sema: Sioni katika yale niliyofunuliwa mimi kitu kilichoharamishwa kwa mlaji kukila isipokuwa kiwe ni nyamafu, au damu inayomwagika, au nyama ya nguruwe, kwani hiyo ni uchafu; au kwa upotofu kimechinjwa kwa jina la asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Lakini mwenye kushikwa na dharura, bila ya kutamani wala kuvuka mipaka, basi hakika Mola wako Mlezi ni Mwenye kusamehe, Mwingi wa kurehemu." [Al-An'am: 145]
Ni kila shughuli inayokiuka Sheria, kama vile riba, kamari, bahati nasibu, ulaghai, udanganyifu, kuhodhi mali na mengineyo ambayo yanajumuisha kuwadhulumu waja, na kula mali za watu kwa batili. Aina hii ndiyo ambayo inatamaniwa sana na nafsi. Ndiyo maana ilihitaji kukemewa na kuiwekea adhabu ambayo inazuia kujiingiza ndani yake. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hakika wale wanaokula mali ya mayatima kwa dhuluma, hapana shaka yoyote wanakula matumboni mwao moto, na wataingia katika Moto wenye mwako mkali." Na Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: "Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na acheni riba zilizobakia, ikiwa nyinyi ni Waumini. Basi msipofanya, jitangazieni vita na Mwenyezi Mungu na Mtume wake." [Al-Baqarah: 278, 279]