Endelea kujifunza

Umeshaingia
Jisajili sasa kwenye jukwaa la Taa ili uanze kujifunza, na fuatialia maendeleo yako, na kukusanya pointi, na uingie kwenye mashindano.Baada ya kujisajili, utapata cheti cha kielektroniki katika mada ambazo utajifunza.

Sehemu ya sasa:

Somo Cheo cha familia katika Uislamu

Katika somo hili, tutajifunza kuhusu maana ya familia na cheo chake katika Uislamu.

  • Kujua maana ya familia katika Uislamu.
  • Kubainisha cheo cha familia katika Uislamu.
  • Kujua nguzo za kujenga familia katika Uislamu.

Maana ya umma

Umma unaundwa kwa makundi ya watu ambao wana mambo wanayofanana ndani yake; kama vile asili yao, lugha, historia, na zaidi ya hayo yote ni dini. Watu hawa walitoka katika nyumba za ndoa zenye waume na wake, na wao pia watakuja unda familia mpya zitakazozaa wana wa kiume na mabinti ambao wataendeleza safari hii. Kwa hili, umma unabakia na kuendelea.

Maisha mazuri ya ndoa ndiyo asili katika maisha ya umma, na kutokea hapa ilikuwa hakuna budi kuzingatia asili hii, ambayo ni familia.

Ingawa mwanadamu ni kiumbe wa kijamii kulingana na maumbile yake ya asili, na hatulii isipokuwa anapoishi katika jamii ambayo ina wanajamii wanaofungamana kwa uhusiano mwingi, lakini anahitaji awatengee idadi fulani ya watu ya baadhi ya hisia, ambao ni wanafamilia yake. Familia katika Uislamu ndiyo sehemu ya jamii inayojumuisha mwanamume na mwanamke waliounganishwa kwa ndoa halali, na uzao unaotokana na hilo.

Uislamu umechukua dhamana ya kutunza sehemu hii ya jamii, kuanzia katika kumhimiza mtu kuoa, kisha kutunza haki za watoto wadogo, na kuishia kupangilia uhusiano kati ya watu wote wa familia moja. Mjengo huu wa kifamilia ndio mwonekano angavu wa ubinadamu wa mwanadamu kama vile Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyokusudia.

Cheo cha familia katika Uislamu

١
Familia katika Uislamu ndiyo nguzo ya asasi ya kujenga jamii ya kibinadamu iliyo salama na yenye uwiano.
٢
Familia ndio mwonekano safi angavu ambamo watu huibuka, na ambayo mahusiano yanaundwa kutoka humo.
٣
Katika Uislamu, familia ndiyo chembe ya kwanza ambamo aina mbalimbali za tabia salama za kijamii hujengeka katika mwanadamu, na ambamo hujua haki zake na wajibu wake.
٤
Katika Uislamu, familia ndiyo hutunza maumbile asili ya baba katika kuelekea kwake kwenye suala la kupanua ukoo wake, kwa hivyo linafikiwa lengo lililokusudiwa la kuhifadhi binadamu wote.
٥
Katika yale yanayobainisha nafasi kubwa ya familia katika Uislamu, ni kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu ameihesabu miongoni mwa neema nyingi alizompa mwanadamu. Mwenyezi Mungu Mtukufu, alisema, "Enyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi aliyewaumba kutokana na nafsi moja, na akamuumba mkewe kutoka nafsi ile ile. Na akaeneza kutokana na wawili hao wanaume wengi na wanawake." [An-Nisaa: 1]

Kuoa katika Uislamu

Mwenyezi Mungu Mtukufu alitia ndani ya kila mwanamume na mwanamke kumuelekea mwingine kwa muelekeo mkubwa wa kimaumbile, na akafanya kuoa kuwa njia halali ya kukidhi mwelekeo huu, na kuzaa wanadamu na kuhifadhi aina hii ya kibinadamu. Uislamu umehimiza katika Qur-ani Tukufu na Sunna za Mtume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - suala la kuoa.

Mjengo wa familia ya Kiislamu unategemea nguzo mbili kuu:

Nguzo ya kisaikolojia

Inajumuisha utulivu wa kisaikolojia, upendo na rehema zilizotajwa katika kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Na katika Ishara zake ni kuwa amewaumbia wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye amejaalia mapenzi na rehema baina yenu. Hakika katika haya, bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanaotafakari." [Ar-Rum: 21]

Nguzo ya kimali

Inajumuisha kutimiza masharti ya mkataba, na kila mmoja wa wanandoa kushikamana na majukumu yake, kama vile kutoa matumizi, utunzaji, kuyasimamia masuala ya nyumba na masilahi ya watoto.

Uislamu unawataka wanandoa wote wawili kutunza mjengo huu na kuuhifadhi, ili usianguke na wakatawanyika watu wanaokaa katika kivuli chake. Kwa sababu ya hilo, unahimiza uvumilivu, na kuendelea kwa uhusiano wa kindoa hata kama upendo kati ya pande hizo mbili utakatika. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Na kaeni nao kwa wema. Na ikiwa mmewachukia, basi huenda mkakichukia kitu, na Mwenyezi Mungu akatia heri nyingi ndani yake." [An-Nisaa: 19]

Umemaliza somo kwa ufanisi


Anza mtihani