Endelea kujifunza

Umeshaingia
Jisajili sasa kwenye jukwaa la Taa ili uanze kujifunza, na fuatialia maendeleo yako, na kukusanya pointi, na uingie kwenye mashindano.Baada ya kujisajili, utapata cheti cha kielektroniki katika mada ambazo utajifunza.

Sehemu ya sasa:

Somo Haki za wanandoa

Katika somo hili, tutajifunza kuhusu haki za kila mwanandoa juu ya mwenzake.

  • Kujifunza kuhusu kanuni ya haki na wajibu katika maisha ya ndoa.
  • Kubainisha baadhi ya haki za mume juu ya mke wake.
  • Kubainisha baadhi ya haki za mke juu ya mumewe.

Haki na majukumu ya maisha ya ndoa

Uislamu uliwapa wanandoa wote wawili haki kadhaa zinazofailiana na majukumu yao. Kwa kutekeleza majukumu haya, na kutokataa kumpa mwenye haki yake, uhusiano kati yao unadhibitiwa, heshima yao inahifadhiwa, na familia yenye mafanikio inaanzishwa, yenye uwezo wa kufikia kusudio ambalo Mwenyezi Mungu alimuumba Adam na uzao wake kwa ajili yake.

Haki za mume juu ya mke wake

١
Kutambua usimamizi wake juu ya familia
٢
Kuhifadhi mali yake
٣
Kumhifadhi wakati hayupo
٤
Kumhifadhia watoto wake
٥
Kumsaidia kutenda heri na mema
٦
Kuitanguliza haki yake juu ya haki ya ndugu zake wengine wote, hata wazazi
٧
Kutekeleza mambo ya nyumbani na kuwatunza watoto

Kutambua usimamizi wake juu ya familia

Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema, "Wanaume ni wasimamizi madhubuti wa wanawake, kwa kufadhiliwa na Mwenyezi Mungu baadhi yao juu ya baadhi, na kwa mali yao wanazozitoa." [An-Nisaa: 34] Hii linahitaji kwamba mwanamume atimize majukumu yake ya usimamizi wake kwa njia bora kabisa, bila ya ugumu na udhalimu, na kwamba ni lazima juu ya mke amtii kwa wema, na asipingane naye kwa sababu ya cheo ambacho Mwenyezi Mungu alimpa kwa uadilifu wake na hekima yake.

Kuhifadhi mali yake na kutozipuuza

Hafai kuzitumia mali zake isipokuwa kwa ruhusa yake; waziwazi au kwa ishara. Lakini, ikiwa mume atashindwa kutoa matumizi ya kutosha juu ya nyumba yake ilhali anao uwezo wa kufanya hivyo, basi mkewe ana haki ya kuchukua kutoka kwa mali zake kile kinachomtosha yeye na watoto wao bila idhini yake, lakini asiiharibu wala kupitiliza kiwango.

Kumhifadhi wakati hayupo

Haruhusiwi kumruhusu mwanaume ambaye si mahramu wake kuingia kwake wakati mumewe hayupo, na hakuna tofauti katika hili kati ya jamaa za mke huyu, wala jamaa za mumewe, wala wengineo.

Kumlinda katika watoto wake

Hilo ni kwa kushirikiana naye katika jukumu la kuwalea vizuri, haswa katika miaka ya mwanzo ya maisha yao. Hii ni kwa sababu watoto wanaishi pamoja naye wakati mwingi, na wanajifunza kwake zaidi kuliko kutoka kwa baba yao.

Mke kusimamia kufanya mambo ya nyumbani na kuwatunza watoto

Hilo ni kwa kuyaendesha, kupanga mambo yake, na kufanya kila huduma katika nyumba awezavyo.

Haki za mke juu ya mumewe

١
Mahari
٢
Kumfundisha kile anachohitaji miongoni mwa mambo ya dini yake.
٣
Kumpa matumizi na pia kutoa matumizi ya nyumba na familia yake.
٤
Kuishi pamoja kwa wema.
٥
Kuonyesha upendo na rehema, na kuzingatia udhaifu wake.
٦
Kufanya uadilifu katika hali ya kuwa na zaidi ya mke mmoja.

Mahari

Ni haki ya mke, ambayo mume anampa kama kipawa na zawadi; ili kuufanya moyo wake kumzoea, na kumfanya ahisi upendo wake kwake, na kwamba kweli anamtaka. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema, "Na wapeni wanawake mahari yao hali ya kuwa ni kipawa." [An-Nisaa: 4]

Kumpa mke matumizi yake, na kutoa matumizi ya nyumba na familia yake

Hilo ni katika kila kitu wanachohitaji, kama vile chakula, kinywaji, mavazi, na makazi, kulingana na inavyohitaji kila hali, na kama awezevyo, bila ya kupitiliza mipaka wala kuwakunjia sana. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Mwenye wasaa, na atoe kulingana na wasaa wake. Na mwenye dhiki, basi na atoe katika alichompa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu hamtwiki mtu isipokuwa kwa kiasi cha alichompa. Mwenyezi Mungu atajalia baada ya dhiki faraji." [At-Talaq: 7]

Kuishi pamoja kwa wema

Anapaswa kuwa na tabia nzuri, mpole kwake kwa kauli na matendo, na asiwe mkali wala mgumu. Pia anafaa kumvumilia mkewe, wala asifuate nyuma ya kila dosari kwa kujitenga mbali naye au kumchukia. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Na kaeni nao kwa wema, na ikiwa mmewachukia, basi huenda mkakichukia kitu, na Mwenyezi Mungu ametia kheri nyingi ndani yake." [An-Nisaa: 19] Naye Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimfikie, alisema, “Muumini asimchukie muumini. Ikiwa anachukia kwake tabia fulani, basi ataridhia kwake nyingine.” (Muslim 1469)

Umemaliza somo kwa ufanisi


Anza mtihani