Sehemu ya sasa:
Somo Hali maalumu za twahara
Kupangusa khuff na soksi
Miongoni mwa wepesi wa dini ya Uislamu ni kwamba inamuwezesha Mwislamu wakati wa kutawadha, kupangusa kwa mkono wake wenye majimaji juu ya soksi au kiatu chake ambacho kinafunika mguu mzima badala ya kuosha mguu wake, na hili ni kulingana na masharti mbalimbali.
Imehalalishwa kupangusa juu ya khuff na soksi wakati wa kutawadha ikiwa Muislamu atazivaa katika hali ya usafi kutokana na hadathi kubwa na ndogo.
Muda wa kupangusa juu ya Khuff na soksi
Inaruhusiwa kupangusa juu ya Khuff wakati wa kutawadha. Ama wakati wa kuoga kutokana na janaba, itamlazimu Mwislamu kuiosha miguu yake kwa hali zote.
Ataanza kuhesabu muda wa kupangusa juu ya Khuff na soksi kuanzia wakati wa kupangusa kwa kwanza baada ya kupata hadathi.
Bendeji ni kitu kinachowekwa juu ya kiungo kinapovunjika au kinapopata majeraha ili isaidie kuharakisha kupona na kupunguza maumivu.
Inatosha tu kupangusa kwa mkono ulioloa maji juu ya bendeji inapohitajika, sawa iwe ni wakati wa kutawadha au kuoga kutokana na janaba.
Inamlazimu aoshe sehemu yoyote ya kiungo hicho inayoonekana. Atapangusa kwa mkono wake ulioloa kwa maji sehemu iliyofunikwa kwa bendeji.
Muda wa kupangusa kwenye bendeji
Ataendelea kupangusa juu ya bendeji hata kama itachukua muda mrefu ilimradi anaihitaji. Na itamlazimu kuiondoa bendeji hiyo na akioshe kiungo hicho pindi haja ya bendeji hiyo inapoisha.
Tayammam
Muislamu asipoweza kutumia maji katika kutawadha au kuoga kwa sababu ya maradhi au ukosefu wa maji, au kwa sababu maji hayapatikani isipokuwa ya kunywa tu, basi inaruhusika kwake kutayammam kwa vumbi mpaka aweze kupata maji na kuweza kuyatumia.
Namna ya kufanya tayammam
Mwislamu atapiga kwa mikono yake mara moja juu ya vumbi.
Atapangusa uso wake kwa vumbi inayoshikilia kwenye mikono.
Atapangusa juu ya kiganja chake cha kulia kwa kiganja chake cha kushoto na kinyume chake.