Endelea kujifunza

Umeshaingia
Jisajili sasa kwenye jukwaa la Taa ili uanze kujifunza, na fuatialia maendeleo yako, na kukusanya pointi, na uingie kwenye mashindano.Baada ya kujisajili, utapata cheti cha kielektroniki katika mada ambazo utajifunza.

Sehemu ya sasa:

Somo Sunna za maumbile ya asili

Mwenyezi Mungu, Mwenye Nguvu, Mtukufu alimuumba mwanadamu akiwa na sifa mbalimbali kamilifu zinazomfanya aonekane bora zaidi ikiwa atazifanyia kazi. Katika somo hili, utajifunza kuhusu Sunnah za maumbile ya asili na hukumu zake.

  • Kujua Sunna za maumbile ya asili.
  • Kujua hukumu za Sunna za maumbile ya asili.

Sunna za maumbile ya asili

Ni sifa ambazo Mwenyezi Mungu amewaumba nazo watu, na ambazo kwa kuzifanya Muislamu anakamilika na anakuwa katika sifa bora zaidi na sura nzuri zaidi. Hilo ni kwa sababu Uislamu ulizingatia mambo mazuri yanayomkamilisha Muislamu ili ajumuishe uzuri wa sura ya nje na ya ndani.

Amesema Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: “Mambo ya maumbile ya asili ni matano: kutahiri, kunyoa sehemu za siri, kupunguza masharubu, kukata kucha, na kunyoa makwapa.” (Al-Bukhari 5891, Muslim 257) Na amesema: “Mambo kumi ni sehemu ya maumbile ya asili: kupunguza masharubu, kufuga ndevu, kutumia mswaki, kuvuta maji puani, kukata kucha, kuosha viungo vya vidole, kunyoa makwapa,kunyoa nywele za sehemu ya siri na kujisafisha kwa maji msalani. [Msimuliaji alisema]: Na nilisahau jambo la kumi na huenda likawa kusuuza mdomo." (Muslim 261)

Kutahiri

Kutahiri kwa wanaume ni kuondolewa ngozi kwenye sehemu ya mbele ya uume, na kwa kawaida hilo huwa katika siku za kwanza za kuzaliwa kwa mtoto. Na hili ni miongoni mwa mambo ya maumbile ya asili ya mwanadamu ambayo ni wajibu kwa wanaume, na lina faida nyingi za kiafya.

Kunyoa nywele za sehemu za siri

Na hili ni kuondoa nywele ngumu za sehemu ya siri kwa kuzinyoa au kwa njia nyingine yoyote ile.

Kupunguza masharubu

Kuachilia masharubu ni katika mambo yanayoruhusika, lakini halipendekezwi. Na iwapo Muislamu atayaacha, basi asiyarefushe kupita kiasi, na atafanya hima kuyapunguza au kufupisha mara kwa mara.

Kuachilia ndevu kumea

Uislamu unahimiza kukuza ndevu, nazo ni nywele zinazoota kwenye mashavu na kidevu. Na maana ya kukuza ndevu ni kuziachilia na kutozinyoa, kwa kufuata Sunnah za Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake.

Kupiga mswaki

Maana yake ni kutumia kijiti cha mti wa Arak au kitu kinginecho katika kusafisha meno, na hilo ni katika yale yanayopendekezwa.

Kukata kucha

Muislamu anafaa kuzichunga kucha zake na kuzifupisha ili zisiwe mahali pa kuweka uchafu.

Kunyoa kwapa

Muislamu anapaswa kuondoa nywele za kwapa kwa kunyoa au kuiondoa kwa chochote chenye kuondoa, ili kuhakikisha kwamba harufu mbaya haitoki ndani yake.

Kuosha viunganishi vya vidole

Viunganishi vya vidole ni mafundo yanayopatikana kwenye vidole, na inapendekezwa kuyaosha.

Kuchamba, kusukutua mdomo, na kuvuta maji ndani ya pua

Kuchamba ni kujisafisha kwa maji baada ya kukidhi haja ya asili. Na haya matatu tumeshayazungumzia hapo awali katika somo la adabu za kujisafisha na kukidhi haja ya asili, na katika somo la kutawadha.

Umemaliza somo kwa ufanisi


Anza mtihani