Endelea kujifunza

Umeshaingia
Jisajili sasa kwenye jukwaa la Taa ili uanze kujifunza, na fuatialia maendeleo yako, na kukusanya pointi, na uingie kwenye mashindano.Baada ya kujisajili, utapata cheti cha kielektroniki katika mada ambazo utajifunza.

Sehemu ya sasa:

Somo Kuamini Malaika

Kuamini katika Malaika ni nguzo katika nguzo za imani. Katika somo hili, utajifunza kuhusu uhakika wao, na sifa zao, na baadhi ya matendo yao, na maana ya kuamini katika hao.

  • Kujua kuhusu maana ya kuamini katika Malaika na umuhimu wake.
  • Kujua kuhusu baadhi ya sifa zao na kazi zao.
  • Kujua kuhusu matunda ya imani katika wao.

Maana ya kuamini katika Malaika:

Ni Imani madhubuti juu ya uwepo wa Malaika, na kwamba wao ni ulimwengu wa ghaibu usiokuwa ulimwengu wa wanadamu na ulimwengu wa majini. Nao ni watukufu na wachamungu, wanamwabudu Mwenyezi Mungu haki ya kumuabudu, na wanatekeleza anayowaamrisha, na kamwe hawamuasi Mwenyezi Mungu. Kama alivyosema Yeye Mtukufu: "Bali hao ni waja waliotukuzwa. Hawamtangulii kwa neno, nao wanafanya amri zake." (Al-Anbiya’: 26-27).

Umuhimu wa kuamini katika Malaika

Kuamini katika Malaika ni moja ya nguzo sita za imani. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: "Mtume ameamini yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa Mola Mlezi wake, na Waumini vile vile. Wote wamemuamini Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na Vitabu vyake na Mitume wake." (Al-Baqarah: 285). Na amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani ziwe juu yake: “Ni kwamba umwamini Mwenyezi Mungu, na Malaika Wake, na Vitabu vyake, na Mitume wake, na Siku ya Mwisho, na kuamini katika majaaliwa , heri yake na shari yake.” (Muslim 8) )

Kuamini katika Malaika ni wajibu kwa kila Muislamu, na mwenye kuwakufuru, basi yeye kwa hakika atapotea, na atateleza. Yeye Mtukufu alisema, "Na mwenye kumkufuru Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na Vitabu vyake, na Mitume wake, na Siku ya Akhera, basi yeye kwa hakika amekwisha potea kupotea kwa mbali." [An-Nisaa: 136] Basi atatumia neno ukafiri kwa mwenye kukanusha nguzo hizi.

Yeye, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alijulisha kwamba mbingu ilikuwa nzito kwa sababu ya wale walio ndani yake, na hapakuwa na nafasi ndani yake ya urefu wa mkono moja isipokuwa yupo malaika amesimama, au amerukuu, au amesujudu.

Kuamini katika Malaika kunajumuisha nini?

١
Kuamini kuwepo kwao: Basi aamini kwamba wao ni viumbe vya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na wapo kihakika.
٢
Kuwaamini wale tunaowajua majina yao kama Jibril, amani iwe juu yake, na wale ambao hatujui majina yao, tunawaamini kwa ujumla.
٣
Kuamini katika kile ufunuo ulijulisha juu ya sifa zao.
٤
Kuamini katika yale yaliyoelezwa na wahyi juu ya kazi zao wanazozifanya kwa amri ya Mwenyezi Mungu.

Katika sifa za malaika ambazo tunaziamini

١
Kwamba hao ni ulimwengu wa ghaibu, na wameumbwa na kuwa wanamuabudu Mwenyezi Mungu, kwa hivyo hawana sifa za umola wala uungu hata kidogo, bali wao ni waja wa Mwenyezi Mungu wanaofuata kabisa katika kumtii Mwenyezi Mungu. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu kuwahusu: "Hawamuasi Mwenyezi Mungu kama anavyowaamrisha na wanafanya wanayoamrishwa." (Al-Tahrim: 6).
٢
Kwamba waliumbwa kutokana na nuru. Amesema, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: “Malaika wameumbwa kutokana na nuru.” (Muslim 2996).
٣
Kwamba wana mbawa zinazotofautiana katika idadi zake. Kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu alijulisha kuwa amewafanya Malaika kuwa na mbawa zinazotofautiana idadi zake. Akasema Yeye Mtukufu: "Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, Muumba wa mbingu na ardhi, aliyewafanya Malaika kuwa wajumbe wenye mbawa, mbili mbili, na tatu tatu, na nne nne. Huzidisha katika kuumba apendavyo. Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza juu ya kila kitu." (Fatir: 1)

Mwenyezi Mungu aliwapa malaika kazi mbalimbali. Miongoni mwake ni:

١
Kufikisha wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwenda kwa Mitume wake, amani iwe juu yao, na aliyekabidhiwa hili ni Jibril.
٢
Kuchukua roho, na aliyekabidhiwa hili ni Malaika wa mauti na wasaidizi wake.
٣
Kuhifadhi matendo ya waja na kuyaandika sawa, yawe ni nzuri au mbaya, na waliokabidhiwa hili ni waandishi watukufu.

Mara nyingi tunastaajabishwa na mtu kuepuka kutokana na ajali fulani iliyokuwa na uhakika kutokea kwake ... na hatupaswi kusahau kwamba kati ya kazi za malaika ni kulinda wanadamu kutokana na mambo ya uharibifu kwa amri ya Mwenyezi Mungu.

Kuamini katika Malaika kuna matunda makubwa katika maisha ya Muumini, miongoni mwake ni:

١
Kuujua ukuu wa Mwenyezi Mungu, na nguvu zake, na ukamilifu wa uwezo wake, kwani ukuu wa viumbe ni katika ukuu wa Muumba. Kwa hivyo Muumini anazidi kumuamini Mwenyezi Mungu na kumtukuza, kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu huwaumba malaika wenye mbawa kutoka kwenye nuru.
٢
Kunyooka katika kumtii Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kwani mwenye kuamini kuwa Malaika huandika matendo yake yote, hili litamsababishia kumhofu Mwenyezi Mungu Mtukufu, hivyo hamuasi hadharani wala kwa siri.
٣
Kuwa na subira katika kumtii Mwenyezi Mungu, na kuhisi hali ya amani na utulivu kwa sababu ya yakini ya Muumini kwamba pamoja naye katika ulimwengu huu mpana, kuna maelfu ya malaika wanaomtii Mwenyezi Mungu kwa namna nzuri zaidi na hali kamilifu zaidi.
٤
Kumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa sababu ya kuwatunza kwake wanadamu, kwa kuwa alifanya katika malaika, wale ambao wanawahifadhi na kuwakinga.

Umemaliza somo kwa ufanisi


Anza mtihani