Endelea kujifunza

Umeshaingia
Jisajili sasa kwenye jukwaa la Taa ili uanze kujifunza, na fuatialia maendeleo yako, na kukusanya pointi, na uingie kwenye mashindano.Baada ya kujisajili, utapata cheti cha kielektroniki katika mada ambazo utajifunza.

Sehemu ya sasa:

Somo Kuamini Mitume

Kuamini Mitume ni miongoni mwa nguzo sita za imani. Katika somo hili, utajifunza kuhusu maana ya kuamini katika mitume, na umuhimu wake, na tabia zao, na baadhi ya miujiza yao.

  • Kujua maana ya kuamini Mitume.
  • Kujua  sifa za Manabii na Mitume.
  • Kujua baadhi ya miujiza yao.
  • Kujua matunda ya kuamini katika wao.

Maana ya kuamini Mitume

Ni kusadiki kwa uhakika kwamba Mwenyezi Mungu alituma katika kila umma Mtume kutoka miongoni mwao anayewaita wamuabudu Mwenyezi Mungu peke yake, pasi na washirika. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu: "Na kwa hakika kwa kila umma tuliutumia Mtume kwamba: Muabuduni Mwenyezi Mungu, na muepukeni Shetani.” [An-Nahl: 36]

Tunaamini kuwa Mitume wote ni wakweli, wanaosadikiwa, wachamungu, waaminifu, waongofu na walioongolewa, na kwamba walifikisha kila alichowatuma nacho Mwenyezi Mungu, wala hawakukificha wala hawakukibadilisha, wala hawakuongeza ndani yake hata herufi moja kutoka kwa nafsi zao wenyewe wala hawakuyapunguza. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "(Hao wa zamani) waliokuwa wakifikisha risala za Mwenyezi Mungu na wanamwogopa Yeye, na wala hawamwogopi yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ndiye atoshaye kuhesabu." (Al-Ahzab: 39)

Haja ya watu kwa ujumbe:

Watu lazima wawe na ujumbe wa kimungu unaowafafanulia sheria na kuwaongoa kwenye yale yaliyo sahihi na ya haki. Na Ujumbe ndio roho ya ulimwengu, na nuru yake, na uhai wake. Basi Ulimwengu utatengenea vipi ikiwa hakutakuwepo roho, uhai, na nuru?

Ndiyo maana Mwenyezi Mungu akauita ujumbe wake kuwa ni roho, na roho ikipotea, basi uhai unapotea. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: "Na namna hivi tumekufunulia Qur-ani kwa amri yetu. Ulikuwa hujui Kitabu ni nini, wala Imani. Lakini tumekifanya kuwa ni Nuru ambayo kwayo tunammwongoa tumtakaye katika waja wetu." (Al-Shura: 52). Hii ni kwa sababu, ingawa akili inajua mema na mabaya kwa ujumla, lakini haiwezi kujua maelezo yake ya kina. Na utekelezaji matendo ya ibada na namna zake huuwezi kujulikana isipokuwa kupitia ufunuo na ujumbe.

Kwa hivyo, hakuna njia ya kupata furaha na mafanikio katika ulimwengu wote wawili isipokuwa kwa mikono ya Mitume, na hakuna njia ya kujua mema na mabaya kwa usahihi isipokuwa kupitia kwao, na yeyote anayeuepuka ujumbe atapata misukosuko, wasiwasi na taabu kwa kadiri anavyoipinga na kujiepusha nayo. Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: “Tukasema: Shukeni nyote kutoka humo; na kama ukikufikieni uwongofu utokao kwangu, basi watakaofuata uwongofu wangu huo, haitakuwa hofu juu yao wala hawatahuzunika. Na wenye kukufuru na kukadhibisha ishara zetu, hao ndio watakaokuwa watu wa Motoni, humo watadumu.” (Al-Baqara: 38:39).

Moja ya nguzo za Imani

Kuamini Mitume ni miongoni mwa nguzo sita za imani. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: "Mtume ameamini yale yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa Mola Mlezi wake, na Waumini vile vile. Wote wamemuamini Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na Vitabu vyake na Mitume wake. Hatutafautishi baina ya yeyote katika Mitume wake." (Al-Baqara: 285). Aya hii inaashiria ulazima wa kuwaamini Mitume wote, rehema na amani ziwe juu yao bila ya kutofautisha kati yao. Kwa hivyo, hatufai kuwaamini baadhi ya Mitume na kuwakufuru wengine kama walivyo Mayahudi na Wakristo.

Amesema Mwenyezi Mungu, rehema na amani ziwe juu yake: “Kwamba umwamini Mwenyezi Mungu, Malaika Wake, Vitabu vyake, Mitume wake, Siku ya Mwisho, na kuamini hatima ya heri na ya shari.” (Muslim 8)

Ishara na miujiza ya Mitume‭

Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwaunga mkono Mitume wake, amani iwe juu yao, kwa ishara na ushahidi mbali mbali unaoonyesha ukweli wao na unabii wao, ikiwa ni pamoja na kuwaunga mkono kwa miujiza na ishaha dhahiri ambazo haziko ndani ya uwezo wa wanadamu. Ili kubainisha ukweli wao na kuthibitisha unabii wao. Na maana ya miujiza ni: mambo ya ajabu ambayo Mwenyezi Mungu Mtukufu huyadhihirisha kupitia mikono ya manabii na mitume wake kwa njia ambayo wanadamu hawawezi kuleta mfano wake.

Miongoni mwa miujiza ya Manabii, amani iwe juu yao:

١
Kugeuka kwa fimbo ya Musa, amani iwe juu yake, kuwa nyoka.
٢
Isa, amani iwe juu yake, kuwaambia watu wake kile watakachokula na watakachoweka akiba katika nyumba zao.
٣
Kupasuliwa mwezi kwa ajili ya Mtume wetu Muhammad, rehema na amani ziwe juu yake.

Kuamini Mitume kunajumuisha nini?

1- Kuamini kwamba ujumbe wao ni wa kweli kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na kwamba ujumbe huo unaafikiana katika kulingania kumwabudu Mwenyezi Mungu peke yake pasi na mshirika yeyote.

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Na kwa hakika kwa kila umma tuliutumia Mtume kwamba: Muabuduni Mwenyezi Mungu, na muepukeni Taghut (Shetani na wengineo).” (An-Nahl: 36)

Huenda sheria za Mitume zikahitalifiana katika matawi ya halali na haramu kulingana na kile kinachofaana na umma huo. Kama Mwenyezi Mungu alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Kila mmoja katika nyinyi tumemwekea sheria yake na njia yake." (Al-Maida: 48)

2- Kuamini Manabii na Mitume wote

Tunawaamini wale ambao Mwenyezi Mungu amewataja miongoni mwa Mitume kama vile: Muhammad, Ibrahim, Musa, Isa, Nuh, Yakub, Yusuf, Yunus, na wengineo rehema na amani iwe juu yao. Na ama wale ambao hatujui majina yao, tunawaamini kwa ujumla wao, na anayekufuru ujumbe wa mmoja wao; amewakadhibisha wote.

3- Kusadiki yaliyo sahihi katika habari na miujiza yao

Kwa hivyo tunazisadiki habari sahihi za Mitume na miujiza yao katika Qur-ani na Sunnah, kama vile kisa cha kupasua bahari cha Musa, amani iwe juu yake.

4- Kuitendea kazi sheria ya Mtume aliyetumwa kwetu, na yeye ndiye mbora zaid wao na wa mwisho wao: Muhammad, rehema na amani ziwe juu yake.

Katika sifa za Mitume:

1- Kwamba wao ni wanadamu

Na tofauti baina yao na watu wengineo ni kuwa Mwenyezi Mungu aliwateua kwa ajili ya wahyi na ujumbe. Mwenyezi Mungu amesema: "Na hatukuwatuma Mitume kabla yako isipokuwa wanaume tuliowafunulia wahyi." (Al-Anbiya: 7) Na akasema Mwenyezi Mungu: "Sema: Mimi ni mwanadamu kama nyinyi. Ninaletewa Wahyi kwamba Mungu wenu ni Mungu Mmoja.” (Al-Kahf: 110). Siyo kuwa wao wana baadhi ya sifa za ubwana na uungu, bali wao ni wanaadamu ambao wamefikia ukamilifu katika tabia ya dhahiri, na pia wamefikia kilele cha ukamilifu katika maadili. Pia ni watu bora kwa nasaba, na wana akili safi na ulimi ulio wazi unaowastahiki kubeba matokeo ya ujumbe na kutekeleza mizigo ya unabii. Bali Mwenyezi Mungu amewaumba Mitume kutokana na wanadamu ili wawe ni viigizo kutoka katika aina zao, na katika hali hiyo kumfuata Mtume na kumuiga, na itakuwa ndani ya uwezo wao na ndani ya mipaka ya uwezo wao.

2- Mwenyezi Mungu tu ndiye aliyewateua kwa ajili ya ujumbe.

Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwateuua kwa wahyi kando na watu wengine. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu: "Mwenyezi Mungu huteua Wajumbe miongoni mwa Malaika na miongoni mwa watu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona." (Al-Hajj: 75) Utume na ujumbe haupatikani kwa usafi wa kiroho, akili, au mantiki ya akili, bali ni chaguo na uteuzi wa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu aliwachagua Mitume na akawateua miongoni mwa watu wote. Kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema: "Mwenyezi Mungu ndiye Mjuzi kuliko wote kujua wapi anaweka ujumbe wake." (Al-An'am: 124).

3- Wao wamehifadhiwa kutokana na kukosea katika yale wanayowasilisha kuhusu Mwenyezi Mungu.

Kwa hivyo hawafanyi makosa katika kufikisha habari za Mwenyezi Mungu, na hawafanyi makosa katika kutekeleza yale ambayo Mungu amewafunulia.

4- Ukweli

Kwa hivyo Mitume, amani iwe juu yao, ni wakweli katika kauli zao na vitendo vyao. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Haya ndiyo aliyoyaahidi Mwingi wa Rehema na wakasema kweli Mitume." (Yasin: 52)

5. Subira

Nao walilingania kwenye dini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu wakileta bishara njema na maonyo. Na kwa sababu hiyo walipatwa na kila aina ya madhara na kila aina ya taabu, lakini wakawa na subira na ustahimilivu ili kuinua neno la Mwenyezi Mungu. Amesema Mwenyezi Mungu: "Basi subiri, kama walivyosubiri Mitume wenye stahamala kubwa." (Al-Ahqaf: 35)

Kuamini Mitume kuna matunda makubwa, ikiwa ni pamoja na:

١
Kuwa na elimu kuhusu rehema na utunzaji wa Mwenyezi Mungu kwa waja wake, kwani aliwatuma mitume kwao ili kuwaongoa kwenye njia iliyo sawa, na kuwaonyesha jinsi ya kumwabudu Mwenyezi Mungu. Kwa sababu akili ya mwanadamu haijitegemei katika kuyajua haya, Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema kuhusu Nabii wetu Muhammad, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Nasi hatukukutuma ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote." (Al-Anbiya’: 107)
٢
Kumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa neema hii kubwa.
٣
Kuwapenda Mitume, rehema na amani ziwe juu yao, na kuwatukuza, na kuwasifu kwa namna inayowafailia. Kwa sababu walimwabudu Mwenyezi Mungu, na wakafikisha ujumbe wake, na wakawausia waja wake.
٤
Kufuata ujumbe waliouleta Mitume kutoka kwa Mwenyezi Mungu, ambao ni kumwabudu Mwenyezi Mungu peke yake, bila washirika, na kuufanyia kazi, ili muumini apate heri, na uongofu, na furaha katika nyumba zote mbili.

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Basi atakayeufuata uwongofu wangu, hatapotea wala hatataabika. Na atakayejiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki." (Twaha: 123-124)

Umemaliza somo kwa ufanisi


Anza mtihani