Endelea kujifunza

Umeshaingia
Jisajili sasa kwenye jukwaa la Taa ili uanze kujifunza, na fuatialia maendeleo yako, na kukusanya pointi, na uingie kwenye mashindano.Baada ya kujisajili, utapata cheti cha kielektroniki katika mada ambazo utajifunza.

Sehemu ya sasa:

Somo Talaka

Katika somo hili, tutajifunza kuhusu maana ya talaka na baadhi ya hukumu zinazohusiana nayo.

  • Kujua maana ya talaka.
  • Kujua baadhi ya mambo mazuri ya Uislamu kuhusiana na hukumu za talaka.
  • Kubainisha faida na madhara ya talaka.
  • Kujua aina za talaka.
  • Kujua maana ya eda na baadhi ya yale yanayohusiana nayo.

Agano zito

Uislamu umejibidiisha kuhifadhi maisha ya kifamilia, na kuhifadhi uhusiano wa kindoa kwa agano ambalo Qur-ani Tukufu imelielezea kuwa ni zito. Agano hili ni mkataba wa ndoa.

Kwa sababu ya kusisitiza juu ya kuhifadhi uhusiano wa kindoa, Uislamu umewaelekeza waume kuwashikilia wake zao na kutowapa talaka, hata kama wanawachukia au kuchukia mambo fulani katika wao. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema, "Na kaeni nao kwa wema. Na ikiwa mmewachukia, basi huenda mkakichukia kitu, na Mwenyezi Mungu ametia heri nyingi ndani yake." [An-Nisa: 19] Ili agano hili nzito lisivunjike, Uislamu ulionya onyo kali zaidi dhidi ya kujaribu kuleta mfarakano baina ya wanandoa kwa kumharibia mume mkewe. Abu Huraira, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, alisimulia kuwa: Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, alisema, "Si miongoni mwetu mwenye kumharibia mume mkewe." (Abu Dawud 2175)

Uhalisia wa Uislamu

Ingawa dini ya Uislamu inawania kuendelea kwa uhusiano wa kindoa, pia ni dini ya uhalisia ambayo haiji na mambo yaliyo kinyume na maumbile ya asili ya watu na kukandamiza matamanio yao na kuwafanyia ugumu. Badala yake, inazingatia hali zao, hisia zao na mahitaji yao. Mwenyezi Mungu Mtukufu anajua kwamba kuendelea kwa maisha ya kindoa katika hali nyingi kunaweza kuwa na madhara zaidi kuliko kuvunjika kwake. Na anajua kwamba talaka inaweza kuhitajika na hata inaweza kuwa ni lazima wakati mwingine. Kwa hivyo, kuna hekima kubwa katika kuhalalisha talaka na pia kuna kuwapanulia watu mambo yao licha ya ukali na madhara yanayoweza kutokana na hilo.

Uhalali wa Talaka

Uhalali wa talaka umekuja katika maandiko mengi katika Qur-ani Tukufu na Sunna za Mtume. Aya na hadithi mbalimbali zilikuja kudhibiti hukumu zake na kufafanua adabu zake, mpaka moja ya sura za Qur-ani ikaitwa Surat Talaq.

Maana ya Talaka katika lugha ya Kiarabu

Ni kuvunja kizuizi na kukiachilia.

Maana ya Talaka kisheria

Ni kuvunjika muungano wa ndoa papo hapo au katika siku zijazo kwa maneno maalumu. Maneno maalumu huwa kwa njia ya waziwazi; kama vile neno talaka. Nayo maneno ya sitiari ni kama vile neno kujitenga mbali, haramu, kuachiliwa, na mfano wake. Takala pia inaweza kuwa kwa njia ya ishara inayofahamika au kwa njia ya kuandika. Neno 'khulu' pia linaweza kutumika badala ya talaka. Na hakimu akisema wakati anatenganisha kati ya wanandoa, "nimetenganisha" basi hilo pia linachukuliwa kwamba ni talaka sahihi.

Miongoni mwa faida za talaka

١
Katika takala kuna kufungua njia ya kujenga familia mbili mpya zilizojengeka juu ya misingi mizuri ambayo haikuwepo katika ile familia ya kwanza, na neema ya Mwenyezi Mungu ni pana. Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema, "Na wakitengana, basi Mwenyezi Mungu atamtosheleza kila mmoja wao kwa ukunjufu wake. Na Mwenyezi Mungu ni Mkunjufu, Mwenye hekima." [An-Nisaa: 130]
٢
Kuzuia maovu makubwa ambayo yanaweza tokea kutokana na kuendelea kwa maisha yaliyojaa chuki na kutopendana, ambayo yanaweza kumsababishia mwanandoa kuingia katika uchafu - Mwenyezi Mungu aepushe hilo.
٣
Kujifunza kutoka kwa masomo ya ndoa ya kwanza, na kufikiria tena mambo mengi, na mtu kuwa mkweli juu ya nafsi yake kuhusiana na kasoro zake, na kujaribu kuzishinda, mambo ambayo husaidia katika kufanikisha ndoa ya pili.
٤
Kukomesha migongano, makabiliano, chuki, kutopendana, kufanyiana ubaya na kuharibika kwa mahusiano yao.
٥
Kuhifadhi wanafamilia, saikolojia zao na hata wao wenyewe kutokana na kuharibika, kama matokeo ya kuishi katika nyumba ambayo haina utulivu, mambo ambayo yana madhara zaidi kwa watoto.

Miongoni mwa madhara ya talaka

١
Kutawanyika kwa familia na kuharibika kwa nyumba ambayo ilipaswa kujengwa juu ya msingi wa upendo na huruma.
٢
Ikiwa wazazi hawatakuwa na mwenendo mzuri baada ya talaka, ima kwa kuendelea na uhasama na kukatika kwa uhusiano wa watoto na kila mmoja wao, au kuwafanya watoto kuwa ndiyo njia ambayo kila mmoja wao anatumia kumshinikiza mwenzake, au mengineyo, basi watoto huwa wako katika hatari ya kupata shida za kinafsi, na kupotoka kiakili na kimaadili, na athari mbaya za hayo zinakuwa pamoja nao hadi mwisho wa maisha yao.
٣
Uadui na utengano kati ya mume na mke. Hili linaweza kuenea hadi kufikia familia zao, kwa hivyo duara la utengano huu likawa limepanuka. Na hili ni kinyume na kile ambacho Uislamu unataka kwamba jamii iungane na ishikamane.

Aina za Talaka

١
Talaka ya kurudiana bila ya nikaa mpya
٢
Talaka ya kurudiana lakini kwa nikaa mpya
٣
Talaka ya kutorudiana isipokuwa kwa nikaa na talaka mpya.

Talaka ya kurudiana bila ya nikaa mpya

Ni talaka ambayo mwanamume anampa mkewe mara ya kwanza na ya pili, na anakuwa na haki ya kumrudisha mkewe huyo maadamu bado yuko ndani ya eda, bila ya kumuomba idhini, na bila ya kufunga nikaa mpya.

Talaka ya kurudiana lakini kwa nikaa mpya

Ni ile inayokuwa katika mara ya kwanza au ya pili, lakini baada ya kumalizika kwa kipindi cha eda. Hapa mkewe hawi halali kwake kwa kurudiana tu, lakini lazima iwe kwa kufunga nikaa mpya.

Talaka ya kutorudiana isipokuwa kwa nikaa na takala mpya

Ni talaka ya tatu, na hapo mume huwa hana haki ya kumrudisha mkewe isipokuwa kwa kufunga nikaa mpya na mahari mpya baada ya mke huyo kuolewa na mume mwingine, kisha amtaliki - bila ya wao kulipanga hili kabla kwa nia ya kurudiana - au kutokana na kufa kwa mume wa pili.

Hukumu zinazohusiana na talaka ya kurudiana bila nikaa mpya na kurudiana kwa nikaa mpya ambayo mke hapaswi kuidhinisha, na kurudiana kwa nikaa mpya baada ya kutalikiwa na mume mwingine zina udhihirisho wazi wa sifa za sheria ya Kiislamu, kwamba talaka siyo mwisho wa mambo. Katika wakati wa kurudiana kila mmoja wa hao wanandoa hupata fursa na nafasi ya kutosha ili kutafakari tena, na kufikiria juu ya matokeo ya vitendo vyao kwa utulivu na wakiwa mbali na shinikizo la shida iliyokuwa kati yao. Pia baada ya talaka ya mwanamke huyo kutoka kwa mumewe wa pili huenda pande zote mbili zikaweza kugundua kuwa kurudiana kunawezekana na kwamba ni chaguo zuri. Bali mara nyingi inakuwa tajriba hii ni sababu nzuri ya kujenga tena ndoa yao juu kwa misingi wenye nguvu na ulio thabiti.

Eda

Ni kipindi kilichowekwa na Sheria baada ya kuachana kwa mume na mke - kwa kifo au talaka - ambapo inamlazimu mwanamke kukaa bila ya kuolewa mpaka eda yake hiyo iishe.

Mke ana haki ya kukaa eda yake katika nyumba ya mumewe, na inamlazimu mumewe kumpa matumizi, kama vile anastahiki pia kumrithi mumewe ikiwa atakufa ilhali bado yuko katika eda.

Hekima ya kuweka eda katika sheria

١
Ni ibada: Mwanamume wa Kiislamu na mwanamke wa Kiislamu wamesalimisha mambo yao kwa Mwenyezi Mungu, na anapoamrisha jambo, wanaharakisha kulitekeleza, ili kuonyesha uja wao kwake.
٢
Ili kuwa na uhakika kwamba tumbo la uzazi la mwanamke halina mimba.
٣
Kumpa mume nafasi ya kutosha baada ya talaka ili kumrudisha mke wake aliyetalikiwa.
٤
Ili kumuomboleza mumewe aliyekufa.

Umemaliza somo kwa ufanisi


Anza mtihani