Endelea kujifunza

Umeshaingia
Jisajili sasa kwenye jukwaa la Taa ili uanze kujifunza, na fuatialia maendeleo yako, na kukusanya pointi, na uingie kwenye mashindano.Baada ya kujisajili, utapata cheti cha kielektroniki katika mada ambazo utajifunza.

Sehemu ya sasa:

Somo Nguzo za Swala, wajibu zake, yenye kuibatilisha, na yachukizayo ndani yake

Swala ina nguzo na wajibu ambazo haiwezi kufanywa bila ya hizo, na pia inaweza ingiliwa na mambo ambayo yanaibatilisha. Katika somo hili, utajifunza kuhusu nguzo za swala, wajibu zake, mambo yanayoibatilisha, na mambo yanayochukiza ndani yake.

  • Kujua nguzo za swala.
  • Kujua wajibu za swala.
  • Kujua yanayobatilisha swala.
  • Kujua sijda ya kusahau.
  • Kujua yachukizayo katika swala.

Nguzo za swala

Hizi ni sehemu kuu za swala ambazo swala inabatilika ikiwa zitaachwa makusudi, na ambazo ni lazima zifanywe ikiwa zitaachwa bila kukusudia, vinginevyo swala hiyo inabatilika.

Nguzo za swala

١
Takbira ya kufungua swala.
٢
Kisimama ikiwa una uwezo
٣
Kusoma suratul-fatiha
٤
Kurukuu
٥
Kuinuka kutoka kwa rukuu na kusimama wima sawasawa kwa mwenye uwezo wa hilo
٦
Kusujudu
٧
Kukaa baina ya sijda mbili
٨
Tashahud ya mwisho na kukaa kwa ajili yake
٩
Kuwa mtulivu
١٠
Kutoa salamu
١١
Kufanya mpangilio wa sawasawa katika nguzo

Wajibu za swala

Hizi ni sehemu za faradhi za Swala ambazo Swala hubatilika ikiwa mtu ataziacha kukusudia. Lakini akiziacha kwa kusahau, basi ataikamilisha swala yake, kisha atasujudu sijda ya kusahau mwishoni mwa Swala yake.

Wajibu za swala

١
Takbira zote isipokuwa takbira ya kuanza nayo swala (Takbiratul-Ihram)
٢
Kusema: "Ametakasika Mola wangu Mlezi, Mkuu" mara moja huku ukirukuu.
٣
Kusema: "Mwenyezi Mungu amewasikia wanaomsifu." Hayo, mtu atayasema akiwa anaswali peke yake, au ikiwa ni imamu.
٤
Kusema: "Mola wetu Mlezi, sifa njema ni zako" kwa imamu na maamuma.
٥
Kusema: "Ametakasika Mola wangu Mlezi, aliye juu zaidi" mara moja katika sijda.
٦
Akisema: "Mola wangu Mlezi, nisamehe" mara moja katika kikao cha baina ya sijda mbili.
٧
Tashahud ya kwanza na kukaa kwa ajili yake.

Wajibu hizi zinaondolewa ikiwa mtu atazisahau, lakini ataswali sijda mbili kwa sababu ya kusahau huku.

Sunna za swala

Maneno na vitendo vyote ambavyo si miongoni mwa nguzo na wajibu za swala, vilivyojumuishwa katika jinsi ya kuswali ni Sunna zinazokamilisha swala na ni lazima zidumishwe, lakini swala haibatiliki kwa kuziacha.

Sijda ya kusahau

Ni sijda mbili ambazo Mwenyezi Mungu ameziweka ili kufidia mapungufu na kasoro zilizotokea katika swala.

Ni wakati gani sijda ya kusahau inafanywa?

١
Ikiwa aliongeza kurukuu, sijda, kusimama, au kukaa katika Swala kwa sababu ya kusahau au kukosea, basi anatakiwa kusujudu sijda mbili za kusahau.
٢
Ikiwa atapunguza nguzo yoyote ile, ni atalazimika kuifanya nguzo hiyo aliyoiacha, kisha atasujudu sijda mbili kwa sababu ya upungufu huu mwishoni mwa swala yake.
٣
Ikiwa ataacha wajibu miongoni mwa wajibu za swala, kama vile tashahud ya kwanza, kwa kukosea na kusahau, basi anatakiwa kusujudu sijda mbili kwa sababu ya kusahau huku.
٤
Akitilia shaka idadi ya rakaa alizoswali, basi ataijenga hukumu yake juu ya idadi ambayo ana yakini nayo, ambayo ni idadi ndogo zaidi, kisha atasujudu sijda ya kusahau.

Jinsi ya kufanya sijda ya kusahau

Kuna nyakati mbili za sijda ya kusahau, kwa hivyo anaweza kuchukua moja ya nyakati hizi:

١
Kabla ya salamu na baada ya tashahhud ya mwisho. Atasujudu kisha atatoa salamu.
٢
Baada ya kutoa salamu ya kumaliza swala. Atasujudu sijda mbili za kusahau, kisha atatoa salamu tena.

Yenye kuharibu swala

Haya ni mambo yanayobatilisha swala na inalazimu kuirudia.

Yenye kuharibu swala

١
Kuacha kwa makusudi nguzo au sharti huku una uwezo wa kuifanya; au kwa kusahau katika hali ya kuiacha hata baada ya kutahadharishwa.
٢
Kuacha wajibu miongoni mwa wajibu za swala.
٣
Kuzungumza kimakusudi.
٤
Kucheka kwa sauti kubwa.
٥
Kufanya harakati ikiwa ni nyingi kwa mtawalia bila ya kuwepo haja kuzifanya.

Maombi yanayochukiza katika swala.

Haya ni matendo ambayo yanapunguza malipo ya swala na yanaondoa unyenyekevu na heshima yake.

Kuangalia huku na huku katika swala

Hili haliruhusiki, kwa sababu Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu ya yake, aliulizwa kuhusu kugeukageuka katika Swala, na akasema, “Ni njia ya kuiba ambayo Shetani anachukua (sehemu) kutoka katika swala ya mja.” (Al-Bukhari 751)

Kuchezea mikono, uso na mengineyo

Kuweka mkono kwenye ubavu, kuingiza vidole kwa vingine na kuvivunjavunja.

Kuingia kwenye swala huku moyo wake umeshughulika mbali nayo

Hili ni kwa sababu anahitaji kwenda chooni au anahitaji chakula ikiwa kimeshawasilishwa mbele yake. Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alisema: “Hakuna swala yoyote (inayoruhusiwa) wakati chakula kimeshawekwa mbele, wala ilhali amekazwa na vile vichafu viwili (yaani, haja ndogo na haja kubwa).” (Muslim 560)

Umemaliza somo kwa ufanisi


Anza mtihani