Sehemu ya sasa:
Somo Nyakati ambazo swala za kujitolea zimekatazwa
Nyakati ambazo swala za kujitolea zimekatazwa.
Nyakati zote zinaruhusiwa kwa Mwislamu kuswali swala ya Nafila (hiari) yoyote ile, isipokuwa katika nyakati zilizokatazwa, ambazo Uislamu umekataza kuswali muda huo kwa sababu nyingi. Baadhi yake ni wakati wa ibada za makafiri, na baadhi yake ni wakati Jahannamu inapokuwa imetiwa moto mkubwa sana, na baadhi yake ni wakati ambapo jua huchomoza ndani yake kati ya pembe mbili za Shetani, na sababu zinginezo. Kwa hivyo haiswaliwi wakati huo isipokuwa katika hali ya kulipa swala za lazima zilizopita, au swala za Nafila (hiari) ambazo zina sababu maalumu, kama vile Tahiyyatul Masjid (yaani, swala ya kuingia msikitini). Katazo hili linahusiana na swala peke yake, lakini kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kumuomba dua ni halali katika nyakati zote .
Kuanzia baada ya swala ya alfajiri hadi jua linapochomoza na kuinuka angani kuinuka kudogo kunakoweza kupimwa kisheria kwa urefu wa mkuki. Katika nchi za wastani kuinuka juu huku hutokea takriban dakika ishirini baada ya jua kuchomoza.
Ni wakati jua linapokaribia kufika katikati ya mbingu. Nao ni muda mfupi kabla ya wakati wa adhuhuri kuingia.
Ni baada ya swala ya alasiri hadi jua linapozama.