Sehemu ya sasa:
Somo Mambo yanayovunja saumu
Mambo yanayovunja saumu
Ni mambo ambayo mtu anayefunga anapaswa kujiepusha nayo kwa sababu huharibu funga yake.
Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: "Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa alfajiri katika weusi wa usiku." (Al-Baqara: 187)
Mwenye kula au kunywa kwa kusahau; saumu yake ni sahihi na hakuna dhambi juu yake. Kama alivyosema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: “Mwenye kusahau akiwa amefunga na akala au akanywa, basi akamilishe funga yake, kwani hakika Mwenyezi Mungu ndiye aliyemlisha na kumnywesha.” (Al-Bukhari 1933, Muslim 1155)
2. Vitu vyenye maana ya kula na kunywa
3. Kujamiana kwa kuingiza kichwa cha uume kwenye uke wa mwanamke, sawa mwanamume huyu alitoa manii au la.
4. Mwanaume kujitoa manii kwa hiari yake; kwa kutizama kwa matamanio au kwa kupiga punyeto, na mifano yake.
Ama ndoto inayotokea usingizini, hiyo sio katika mambo yanayoharibu saumu. Mwanamume anaweza kumbusu mkewe ikiwa anaweza kujizuia, vinginevyo haruhusiwi kufanya hivyo ili asiharibu funga yake.
5.Kutapika kwa makusudi
Mwenye kutapika bila hiari, hakutakuwa na chochote juu yao. Amesema Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: “Mwenye kushindwa na akatapika huku amefunga saumu, basi hatalazimika kulipa. Lakini akijitapikisha, basi na alipe.” (Tirmidhi 720, Abu Dawud 2380)
6. Kutokwa kwa damu ya hedhi na ya baada ya kuzaa (nifaas)
Kila inapopatikana damu ya hedhi au damu ya baada ya kuzaa katika sehemu yoyote ya mchana, basi mwanamke huyo atakuwa ameshafungua saumu yake. Na kama alikuwa katika hedhi, kisha akasafika baada ya alfajiri kutokea, basi saumu yake haitakuwa sahihi siku hiyo. Kwa sababu ya kauli yake Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Je, si kweli kwamba anapokuwa katika hedhi, haswali wala hafungi saumu?"(Al-Bukhari 1951)
Ama damu inayotoka kwa mwanamke kutokana na ugonjwa, ambayo ni tofauti na hedhi ya kawaida katika siku maalumu za mwezi na damu ya nifasi inayotoka baada ya kujifungua, hiyo haizuii kufunga saumu.