Sehemu ya sasa:
Somo Walioruhusiwa na Mwenyezi Mungu kutofunga katika mwezi wa Ramadhani.
Wale ambao Mwenyezi Mungu aliruhusu kutofunga saumu ya mwezi wa Ramadhani
Mwenyezi Mungu amewapa ruhusa makundi ya watu kufuturu katika mwezi wa Ramadhani; kwa sababu ya kuwahafifishia, kuwarehemu na kuwafanyia wepesi.
Kwa hivyo anaruhusiwa kutofunga, na atalipa idadi ya siku ambazo hakufunga baada ya Ramadhani kuisha akiwa ni katika wale wanaotarajiwa kupona.
Hii ni kwa sababu ya uzee au ugonjwa ambao hatarajiwi kupona. Huyu anaruhusiwa kutofunga na atalisha kila siku masikini mmoja. Atampa kiasi cha kilo moja unusu cha chakula kikuu cha mji huo.
Ni haramu kwao kufunga na hata wakifunga, saumu yao haiwi sahihi, na inawalazimu kulipa funga hiyo baada ya Ramadhani.
Mwanamke mjamzito au yule anayenyonyesha akihofia kujidhuru au kumdhuru mtoto wake, basi ataacha kufunga ila atalipa funga hio baadaye. Imesimuliwa kutoka kwa Anas bin Malik, Mwenyezi Mungu amridhie, kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, alisema: "Kaa chini nitakuelezea juu ya kufunga saumu. Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu amemuondolea msafiri nusu ya Swala, na akamuondolea kufunga saumu msafiri, mjamzito na mwanamke anayenyonyesha." (Ibn Majah 1667)
Wakati wa safari yake na anapokuwa amekaa mahali kwa muda wa chini ya siku nne, msafiri anaweza kutofunga saumu, kisha atazilipa siku hizo baada ya Ramadhani.
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi atimize hesabu katika siku nyingine. Mwenyezi Mungu anawatakia yaliyo mepesi wala hawatakii yaliyo mazito." (Al-Baqarah: 185)
Ni ipi hukumu ya yule asiyefunga bila ya udhuru?
Kila anayefungua saumu yake katika Ramadhani bila udhuru, lazima atubu kwa Mwenyezi Mungu kwa sababu amefanya dhambi kubwa na kutotii amri ya Muumba Mtukufu. Inamlazimu kulipa siku hiyo tu, isipokuwa kwa yule anayevunja funga kwa kufanya tendo la ndoa. Yeye atatubu na kulipa siku hiyo, na inamlazimu pamoja na hayo kufidia maasi hayo kwa kuachilia huru mtumwa Mwislamu. Na Uislamu unasisitiza umuhimu wa kumkomboa mwanadamu kutoka katika utumwa katika kila wakati. Lakini ikiwa hilo haliwezekani, kama ilivyo leo, basi atafunga miezi miwili mfululizo, na ikiwa hawezi, basi atawalisha masikini sitini.