Sehemu ya sasa:
Somo Kufunga saumu kwa hiari
Mwenyezi Mungu alilazimisha kufunga saumu mwezi mmoja katika mwaka, lakini alihimiza kufunga saumu katika siku nyinginezo kwa mwenye uwezo na hamu ya kufanya hivyo ili kutafuta malipo zaidi, na miongoni mwa siku hizo ni:
Ni siku ya kumi ya mwezi wa Muharram; mwezi wa kwanza katika kalenda ya Kiislamu. Hii ni siku ambayo Mwenyezi Mungu alimwokoa Nabii wake Musa, amani iwe juu yake, kutoka kwa Firauni. Kwa hivyo Muislamu anaifunga ili kumshukuru Mwenyezi Mungu juu ya kumuokoa Musa, amani iwe juu yake, na kumfuata Mtume wetu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, kwa sababu aliifunga. Alipoulizwa juu ya kufunga saumu siku ya Ashura, alisema: "Inasamehe dhambi za mwaka uliopita." (Muslim 1162). Inapendekezwa kufunga saumu siku moja kabla yake, siku ya tisa. Imesimuliwa kutoka kwa Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, kwamba alisema: "Ikiwa nitabakia mpaka mwaka ujao, basi hakika nitafunga saumu siku ya tisa." (Muslim 1134)
Ni siku ya tisa ya mwezi wa Dhul-Hijja, mwezi wa kumi na mbili wa kalenda ya Kiislamu. Siku hii ni wakati ambapo mahujaji waliohiji Nyumba ya Mwenyezi Mungu hukusanyika Arafa na kumuomba Mwenyezi Mungu, na ndiyo siku bora ya mwaka. Anaruhusiwa kufunga siku hii mtu asiyekuwa hujaji. Mtume rehema na amani ziwe juu yake, alipoulizwa juu ya kufunga siku ya Arafa, alisema: "Ni kafara ya madhambi ya mwaka uliopita na mwaka uliopo." (Muslim 1162)
Shawwal ni mwezi wa kumi wa kalenda ya Kiislamu. Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alisema: "Atakayefunga Ramadhani kisha akaifuatisha siku sita katika mwezi wa Shawwal, huwa ni kama amefunga mwaka mzima." (Muslim 1164)
Imesimuliwa kutoka kwa Abu Huraira, Mwenyezi Mungu amridhie, kuwa alisema: "Rafiki yangu mwandani aliniusia mambo matatu ambayo sitaacha mpaka nitakapokufa: kufunga siku tatu katika kila mwezi, swala ya dhuha, na kulala hali ya kuwa nimeswali witri." (Al-Bukhari 1178, Muslim 721)