Sehemu ya sasa:
Somo Iddul-Fitr na Iddul-Adha
Iddul-Fitr
Ni siku ya kwanza ya mwezi wa Shawwal; mwezi wa kumi katika kalenda ya Kiislamu, na inakuja baada ya mwisho wa siku ya mwisho ya mwezi wa Ramadhani, ndiyo sababu inaitwa Eid al-Fitr, kwa sababu watu wanamwabudu Mwenyezi Mungu kwa Iftar ya siku hii kama walivyomwabudu Mwenyezi Mungu kwa funga ya Ramadhani. Wanasherehekea Eid shukrani kwa ukamilifu wa fadhila na neema ya Mwenyezi Mungu kwa kuwafanya iwe rahisi kwao kukamilisha funga ya mwezi mtakatifu wa Ramadhani, Mwenyezi Mungu alisema: "Na kukamilisha maandalizi na kujivunia Mungu kwa kile ulichokifanya na kukushukuru." (Al-Baqarah: 185)
Ni mambo gani yanayotakiwa kisheria siku ya Iddul-Fitr?
Mwenyezi Mungu amemuwajibishia mwenye chakula kilicho zaidi ya anachohitaji mchana na usiku wa Iddi kutoa kiwango cha Swaa moja, (kilo mbili na nusu) katika chakula cha watu wa mji huo, sawa iwe ni mchele, ngano au tende, awape Waislamu mafukara na masikini, ili asibaki mtu yeyote hali ya kuwa ana mahitaji siku ya Iddi.
Wakati wake unaanzia magharibi ya siku ya mwisho ya Ramadhani hadi swala ya Iddi. Pia inaruhusiwa kuitoa usiku mmoja au mbili kabla ya Iddi.
Ni Swaa (kilo mbili na nusu au tatu) ya chakula cha watu wa mji huo kama vile ngano, mchele, tende na mfano wake.
Zakatul-Fitr ni lazima kwa wale ambao wana zaidi ya kile wanachohitaji - wao wenyewe na wategemezi wake kama vile mkewe na watoto wake - siku ya Idi na usiku wake. Inapendekezwa kuwatolea viumbe walio matumboni mwa mama. Kwa hivyo atajitolea na amtolee kila mtegemezi wake Swaa moja (kilo mbili na nusu au tatu) katika chakula cha mji huo.
Hekima katika kutozwa Zakatul-Fitr
Ilifaradhishwa na mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, ili kumtakasa mfungaji saumu kutokana na maneno ya upuuzi na machafu, na kukamilisha mapungufu yaliyotokea katika kufunga kwake.
Hii ndiyo siku kuu ya pili kwa Waislamu na inakuja katika siku ya kumi ya mwezi wa Dhul-Hijja (mwezi wa kumi na mbili katika kalenda ya Kiislamu). Ina fadhila nyingi sana ikiwa ni pamoja na:
1. Ni mojawapo ya siku bora zaidi za mwaka
Siku bora za mwaka ni kumi za mwanzo za mwezi wa Dhul-Hijja. Amesema Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: “Hakuna siku ambazo kufanya matendo ndani yake humpendeza zaidi Mwenyezi Mungu kuliko hizi siku kumi.” Wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, hata jihadi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu? Mtume wa Mwenyezi Mungu (rehema na amani ziwe juu yake) amesema: "Hakuna jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, isipokuwa mtu aliyetoka mwenyewe na fedha zake na hakurudi kutoka huko na kitu chochote." (Al-Bukhari 969, Al-Tirmidhi 757)
Ndani yake kuna matendo makuu ya Hija na ya umuhimu mkubwa na matukufu kama vile kuzunguka Al-Qaaba, kuchinja wanyama wa dhabihu na kuzitupia Jamaraat vijiwe.
Ni nini kinachoruhusika katika siku ya Idul-Adha?
Katika siku ya Idul-Adha, inaruhusika kwa wasiokuwa mahujaji kufanya kila kitu ambacho kimefaradhishwa siku ya Idul-Fitri, isipokuwa Zakatul-Fitr, ambayo ni mahususi kwa Idul-Fitr pekee. Nayo Idul-Adh'ha ni tofauti kwa sababu imependekezwa kumchinja mnyama wa dhabihu kama njia ya kujiweka karibu na Mwenyezi Mungu.
Ni kile kinachochinjwa miongoni mwa wanyama kama vile ngamia, ng'ombe, mbuzi au kondoo kwa ajili ya kujiweka karibu na Mwenyezi Mungi siku ya Idul-Adh'ha baada ya swala ya Iddi hadi jioni ya siku ya kumi na tatu ya mwezi wa Dhul-Hijja. Mwenyezi Mungu amesema: "Basi Swali na uchinje kwa ajili ya Mola wako Mlezi." (Al-Kawthar: 2) Aya hii ilifasiriwa kuwa ni mahususi kwa Swala ya Idul-fitri na Idul-Adh'ha.
Hukumu zake
Ni Sunna iliyokokotezwa kwa mwenye uwezo. Muislamu atajichinjia yeye mwenyewe na kwa niaba ya wana familia yake.
Ni katika sheria kwamba yule ambaye anataka kuchinja dhabihu asikate chochote katika nywele zake, wala kucha zae, wala ngozi yake, kutokea unapoonekana mwezi mwandamo wa Dhul-Hijja hadi atakapomchinja dhabihu wake.
Masharti ya mnyama wa dhabihu (Udh-hiya) anayechinjwa.
Nao ni kondoo, mbuzi, ng'ombe au ngamia, na dhabihu hiyo hairuhusiki kutoka kwa wanyama wengineo au ndege. Kondoo au mbuzi anamtosheleza mtu mmoja na wana familia yake, na inaruhusika kwa watu saba kushirikiana katika ng'ombe ama ngamia mmoja.
Mnyama huyo anafaa awe amefikisha umri unaohitajika.
Umri unaohitajika kwa kondoo ni miezi sita, na kwa mbuzi ni mwaka mmoja, na kwa ng'ombe ni miaka miwili, na kwa ngamia ni miaka mitano.
Usalama wa wanyama hao kutokana na kasoro zinazoonekana
Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alisema: "Wanne hawaruhusiki kuchinjwa kama dhabihu: Mnyama mwenye jicho moja ambaye dosari yake hiyo ni dhahiri, mnyama mgonjwa ambaye maradhi yake ni dhahiri, mnyama kilema ambaye ulemavu wake uko dhahiri, na mnyama ambaye ni dhaifu (aliyekonda) sana.” (An-Nasai 4370, Tirmidhi 1497)