Endelea kujifunza

Umeshaingia
Jisajili sasa kwenye jukwaa la Taa ili uanze kujifunza, na fuatialia maendeleo yako, na kukusanya pointi, na uingie kwenye mashindano.Baada ya kujisajili, utapata cheti cha kielektroniki katika mada ambazo utajifunza.

Sehemu ya sasa:

Somo Majira ya baridi na usafi

Usafi una hukumu maalum katika msimu wa baridi. Katika somo hili, utajifunza kuhusu baadhi ya hukumu hizo.

  • Kujifunza jinsi ya kujisafisha katika msimu wa baridi.
  • Kujua hukumu za kufuta juu ya Khuff (viatu vya ngozi nyepesi).
  • Kujua jinsi ya kutayammam.

Usafi wa maji ya mvua:

Maji ya mvua ni safi na ni yenye kusafisha. Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: "Na tunayateremsha kutoka mbinguni maji safi." (Al-Furqan: 48) Vile vile, athari za maji hayo yanayorukia nguo, mchanga na lami ya barabarani ni safi.

Kutawadha sawasawa katika msimu wa baridi kali:

Kutawadha sawasawa - licha ya ubaridi wa maji au joto lake - ni ibada miongoni mwa ibada. Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alisema: "Je, nisiwaonyeshe kile ambacho Mwenyezi Mungu hufuta kwacho madhambi na kunyanyua kwacho daraja?" Wakasema, "Ndiyo, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu." Akasema, "Kutawadha kikamilifu katika nyakati za kuchukiza, na kufanya hatua nyingi kwenda msikitini, na kungoja swala (inayofuata) baada ya swala (iliyoisha), na huko ndiko kujizuia kwenyewe." (Muslim 251)

Mojawapo ya makosa ni uzembe katika kuosha viungo kwa sababu ya kuepuka ubaridi wa maji. Kwa mfano utawakuta baadhi ya watu hawajakamilisha kuosha uso wao au hata wanaupangusa tu, au hawajakamilisha kuosha mkono au mguu, na hili haliruhusiki. La wajibu ni kukamilisha ikiwa mtu anaweza kufanya hivyo, vinginevyo na atumie maji ya moto au mfano wake.

Inaruhusiwa kupasha maji joto kwa ajili ya kutawadha wakati wa msimu wa baridi, na hilo halipunguzi malipo. Inaruhusika pia kukausha viungo baada ya kutawadha, na hilo pia halipunguzi malipo. Ikiwa mtu atadhurika kwa kuacha kufanya hivyo au ikiwa hatatawadha vyema kwa sababu ya ubaridi wa maji, basi asiache kupasha maji joto.

Tayammam:

Ni mtu kupiga mavumbi ya ardhi kwa viganja vyake, kisha apanguse uso wake kwavyo, kisha apanguse kiganja chake cha kulia kwa kiganja chake cha kushoto, kisha apanguse kiganja chake cha kushoto kwa kiganja chake cha kulia.

Je, tayammam huruhusika wakati gani?

Tayammam inaruhusika wakati maji hayapo kabisa, au ikiwa yapo kwa uchache na pia yanahitajika katika mambo mengine, au kwa sababu ya kuwepo shida kubwa zaidi katika kutawadha kwayo; kwa sababu ya ukali wa baridi au ugonjwa.

Kupangusa juu ya Khuff (viatu vya ngozi nyepesi):

Kupangusa juu ya Khuff ni wakati mtu amevalia viatu vya ngozi nyepesi ambavyo vinafunika miguu, au amevalia soksi au mfano wake miongoni mwa vitu ambavyo vinafunika miguu yote, kwa sharti kwamba alivivaa hali ya kuwa yeye mwenyewe ni safi kutokana na hadathi kubwa na ndogo. Kwa hivyo, anapopangusa kichwa chake na masikio yake anapotawadha, haimlazimu kuvua Khuff zake ili aoshe miguu yake, badala yake atapangusa tu juu ya miguu yake kwa juu ya Khuff hizo.

Ili kupangusa juu ya Khuff kuwe sahihi, yafuatayo ndiyo masharti yake:

١
Khuff zenyewe ziwe safi.
٢
Khuff hizo zifunike miguu.
٣
Na kwamba Muislamu azivae baada ya kutawadha vikamilifu pamoja na kuosha miguu vizuri.

Muda wa kupangusa juu ya Khuff

Mkazi atapangusa kwa muda wa mchana mmoja na usiku mmoja (masaa 24)
Naye msafiri atapangusa kwa muda wa michana mitatu na usiku wake (masaa 72)

Kuhesabu muda wa kupangusa juu ya Khuff kutaanza kutokea mara ya kwanza alipopangusa baada ya kupatwa na hadathi.

Hairuhusiwi kufuta juu ya Khuff kwa yule ambaye alizivaa bila ya kutawadha kikamilifu, wala kwa yule ambaye kipindi cha kufuta juu yake kimeisha, wala kwa yule ambaye anapaswa kuoga - kwa sababu ya janaba au mfano wake. Huyu analazimika kuzivua, na kujisafisha pamoja na kuosha miguu.

Umemaliza somo kwa ufanisi


Anza mtihani