Endelea kujifunza

Umeshaingia
Jisajili sasa kwenye jukwaa la Taa ili uanze kujifunza, na fuatialia maendeleo yako, na kukusanya pointi, na uingie kwenye mashindano.Baada ya kujisajili, utapata cheti cha kielektroniki katika mada ambazo utajifunza.

Sehemu ya sasa:

Somo Kuna hukumu za jumla ambazo zinahitajika sana wakati wa majira ya baridi.

Kuna hukumu za jumla ambazo zinahitajika sana wakati wa majira ya baridi. Somo hili litabainisha baadhi yake.

  • Kujifunza kuhusu baadhi ya hukumu na adabu ambazo zinahitajika sana katika msimu wa baridi

Kuzima moto wakati wa kulala

Moto ambao mara nyingi huwashwa wakati wa msimu wa baridi unapaswa kuzimwa kabla ya kulala, na vile vile vipasha joto vinavyoweza kusababisha moto. Imesimuliwa kutoka kwa Abu Musa Al-Ash'ari, Mwenyezi Mungu amridhie, kuwa alisema: Usiku mmoja, nyumba moja huko Madina ilichomeka pamoja na wakazi wake. Nabii, rehema na Amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, akaambiwa juu yao na akasema: "Hakika moto huu ni adui yenu. Kwa hivyo, mnapolala, basi uzimisheni." (Al-Bukhari 6294, Muslim 2016) Na katika Hadithi nyingine: "Msiache moto katika nyumba zenu mnapoenda kulala." (Al-Bukhari 6293, Muslim 2015)

Muislamu anafaa kufanya nini wakati upepo unapovuma?

1. Anafaa kukumbuka uwezo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu wa kuendesha upepo; akaleta upepo moto na baridi, laini na mkali, akaupeleka kaskazini na kusini, mwingine ukawa ni wa kupandishia mvua na mwingine ni tasa, na kadhalika. Amesema Mtukufu: "Hakika katika kuumbwa kwa mbingu na ardhi, na kuhitalifiana usiku na mchana, na merikebu ambazo hupita baharini kwa viwafaavyo watu, na maji anayoyateremsha Mwenyezi Mungu kutoka mbinguni, na kwa hayo akaihuisha ardhi baada ya kufa kwake, na akaeneza humo kila aina ya wanyama; na katika mabadiliko ya pepo, na mawingu yanayoamrishwa kupita baina ya mbingu na ardhi, bila shaka zimo Ishara kwa watu wanaozingatia." (Al-Baqara 164)

2. Anafaa kuogopa kuwa huenda ni adhabu itokayo kwa Mwenyezi Mungu. Aisha, mke wa Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alisema: Kamwe, sikuwahi kumwona Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, akicheka sana mpaka niweze kuona kidakatonge chake. Lakini alikuwa akitabasamu tu. Na alikuwa anapoona mawingu yaliyotanda au upepo mkali, linajulikana hilo (yaani wasiwasi) kwenye uso wake. ('Aisha) Alisema, "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Ninawaona watu wanapoyaona mawingu yakiwa yametanda, wanafurahia wakitumaini kwamba kunawezakuwa na mvua ndani yake. Lakini ninakuona wewe unapoyaona (mawingu yaliyotanda), kunajulikana kuchukia (hilo) katika uso wako?" Akasema, "Ewe 'Aisha! Ni nini kinaweza kunifanya kuwa katika amani kwamba hakuna adhabu ndani yake. Kwa hakika, walikwisha adhibiwa kaumu fulani kwa upepo. Na kaumu fulani waliiona adhabu na wakasema, 'Hili ni wingu la kutunyeshea mvua!" (Qur-ani 46:24). (Muslim 899)

3. Amuombe Mwenyezi Mungu heri yake. Imesimuliwa kutoka kwa Aisha, Mwenyezi Mungu amridhie, kuwa alisema: Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alikuwa unapopiga upepo mkali, anasema, "Allahumma! Inni as-aluka khayraha, wa khayra maa fiiha, wa khayra maa ursilat bihii. Wa a'udhu bika min sharrihaa, wa sharri maa fiiha, wa sharri maa ursilat bihii (Ee Mwenyezi Mungu! Hakika mimi ninakuomba heri yake, na heri ya kilicho ndani yake, na heri ya uliyoituma ndani yake. Na ninajikinga kwako kutokana na shari yake, na shari iliyoko ndani yake, na shari iliyotumwa nao)." (Muslim 899)

4. Anajiepusha na suala la kuutukana. Ibn Abbas, Mwenyezi Mungu amridhie, alisema kwamba mwanamume mmoja aliulaani upepo mbele ya Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, na Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, akasema: "Usilaani upepo kwani umeamrishwa. Na hakika, mwenye kulaani kitu ambacho hakistahiki kulaaniwa, laana hiyo inamrudia yeye mwenyewe." (Tirmidhi 1978) Na katika hadithi nyingine: "Msiutukane upepo." (Tirmidhi 2252) Imam Shaafi'i alisema: "Mtu yeyote hafai kuutukana upepo kwani ni kiumbe cha Mwenyezi Mungu Mtukufu, ambacho ni kitiifu (kwake), na ni askari miongoni mwa askari wake, ambao anaufanya kuwa ni rehema na laana akipenda."

Muislamu anafaa kufanya nini anaposikia ngurumo za radi?

ʻAbdallāh bin Zubair alisema: Alikuwa anaposikia ngurumo za radi, anaacha kuzungumza, na anasema: “Ametakasika yule ambaye radi inamtakasa kumsifu, na Malaika pia, kwa kumhofu." Na maneno haya pia yako ndani ya Qur-ani: "Na radi inamtakasa Mwenyezi Mungu kwa kumhimidi, na Malaika pia, kwa kumhofu. Naye hupeleka mapigo ya radi yakampata amtakaye. Nao wanabishana juu ya Mwenyezi Mungu. Na Yeye ni Mwenye adhabu kali!" (Ar-Ra'd: 13)

Muislamu anafaa kufanya nini wakati mvua inanyesha?

Mwenyezi Mungu Mtukufu aliielezea mvua kwamba ni yenye baraka, akasema: "Na tumeteremsha kutoka mbinguni maji yaliyobarikiwa." (Surat Qaf: 9) Na miongoni mwa mambo yanayofanywa inaponyesha ni: 1. Mtu kudhihirisha kitu katika mwili wake ili mvua ikinyeshee. Anas, Mwenyezi Mungu amridhie, alisema: Tulinyeshewa na mvua hali ya kuwa tuko pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. Kwa hivyo, Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, akaikunja nguo yake mpaka akanyeshewa na mvua (kwenye ngozi yake). Tukasema:"Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Kwa nini umefanya hivyo?" Akasema: "Kwa sababu, ndiyo (yaani, mvua) imetoka tu kwa Mola wake Mlezi Aliyetukuka." (Muslim 898)

2. Kuomba dua. Imeelezwa katika simulizi kadhaa kwamba huo ni wakati ambao dua hujibiwa.

Dua za wakati mvua inaponyesha na baada yake

Imesimuliwa kutoka kwa Aisha, Mwenyezi Mungu awe radhi naye kuwa, Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alikuwa anapoona mvua, anasema: "Allahumma, swayyiban naafi-'an (Ewe Mwenyezi Mungu! Na iwe mvua yenye manufaa)." (Al-Bukhari 1032) Neno As-swayyib katika hadithi linamaanisha mvua inayonyesha kwa wingi.

Na pia aombe kwamba mvua hiyo iwe ni yenye manufaa; kwa sababu mvua inaweza kuwa nyingi, lakini haina manufaa ndani yake. Imesimuliwa katika Hadithi kuwa: "Ukame si kwamba kutonyeshewa na mvua. Lakini, ukame ni mnyeshewe na mvua lakini ardhi isioteshe kitu." (Muslim 2904) Na neno As-Sanna katika hadithi hii linamaanisha Ukame mkali.

3. Ni sunna kusema neno "rehema" wakati mvua inaponyesha. Imesimuliwa kutoka kwa 'Aisha, mke wa Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, kuwa alisema: "Alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, inapokuwa ni siku ya upepo mkali na yenye kutanda mawingu, linajulikana hilo (yaani, athari ya hofu yake) juu ya uso wake, kisha anakwenda mbele na nyuma (kwa sababu ya wasiwasi). Na wakati mvua inapomaliza kunyesha, anafurahishwa na hilo; kwa hivyo wasiwasi wake ukamwisha." Aisha alisema: "Kwa hivyo, nilimwuliza (sababu ya hali hiyo ya hofu)," naye akasema: "Hakika mimi nilihofia kuwa inaweza kuwa ni adhabu iliyotumwa juu ya Umma wangu." Na alikuwa anapoona mvua, anasema, "Ni rehema." (Muslim 899)

4. Ni sunna kusema wakati mvua inaponyesha na baada yake: "Tumenyeshewa kwa fadhila na rehema ya Mwenyezi Mungu." Imesimuliwa kutoka kwa Zaid bin Khalid Al-Juhani, kuwa alisema; "Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alituswalisha katika swala ya Fajr katika sehemu iitwayo Hudaibiya baada ya usiku wa mvua. Baada ya kukamilisha swala, aliwaelekea watu na akasema: "Je, mnajua Mola wenu Mlezi amesema nini?" Watu wakamjibu: "Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndio wanaojua zaidi." Akasema: "Mwenyezi Mungu amesema, 'Asubuhi ya leo, baadhi ya waja wangu bado ni waumini wa kweli, nao wengine wamenikufuru. Ama yule aliyesema: "Tumenyeshewa kutokana na fadhila na rehema ya Mwenyezi Mungu," basi huyo ndiye aliyeniamini Mimi na akaikufuru nyota. Na ama aliyesema: "Tumenyeshewa kwa sababu ya nyota fulani na fulani," basi huyo amenikufuru Mimi na akaamini katika nyota hiyo." (Al-Bukhari 846, Muslim 71)

Mtu atafanya nini ikiwa kuna hofu ya mvua nyingi?

Ikiwa kuna mvua nyingi sana na mtu akahofia kudhurika nayo, basi inapendekezwa kwamba aombe huku ameinua juu mikono yake kwa dua zilizosimuliwa kutoka kwa Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Ewe Mwenyezi Mungu! Kandoni mwetu na si juu yetu. Ewe Mwenyezi Mungu! Kwenye sehemu tambarare zilizoinuka, kwenye milima, kwenye vilima, kwenye mabonde, sehemu zenye kumea miti." (Bukhari 1014, Muslim 897)

Umemaliza somo kwa ufanisi


Anza mtihani