Endelea kujifunza

Umeshaingia
Jisajili sasa kwenye jukwaa la Taa ili uanze kujifunza, na fuatialia maendeleo yako, na kukusanya pointi, na uingie kwenye mashindano.Baada ya kujisajili, utapata cheti cha kielektroniki katika mada ambazo utajifunza.

Sehemu ya sasa:

Somo Kuamini uwepo wa Mwenyezi Mungu

Uwepo wa Mwenyezi Mungu ndio uhakika ulio dhihiri kabisa. Kwa sababu, kila tunachokiona miongoni mwa viumbe vyake visingekuwepo bila uwepo wake Yeye Mtukufu, Aliye juu. Katika somo hili, utajifunza kuhusu idadi ya ushahidi wa kuwepo kwa Mwenyezi Mungu, Mtakatifu, Mtukufu.

  • Kufikia uthibitisho thabiti wa uwepo wa Mwenyezi Mungu

Maana ya kumuamini Mwenyezi Mungu, Mwenye Nguvu, Mtukufu

Ni uthibitisho thabiti juu ya kuwepo kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kuukiri Umola wake, na Uungu wake, na majina yake na sifa zake.

Kusujudu ni mojawapo ya dalili kuu za kumnyenyekea Yeye Muumba, Mtakatifu, Mtukufu.

Umbile la asili alilioumba Mwenyezi Mungu

Kukiri kuwepo kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ni jambo la umbile la asili ndani ya mwanadamu ambalo halihitaji kujisumbua ili kulitumia kama ushahidi juu ya hilo. Na kwa sababu hii, wengi wa watu wanakiri kuwepo kwa Mwenyezi Mungu licha ya dini na madhehebu zao tofauti tofauti.

Tunahisi kutoka ndani kabisa ya mioyo yetu kwamba yupo, na tunamkimbilia wakati wa shida na mitihani, kwa silika yetu ya kuamini, na silika ya kuwa na dini ambayo Mwenyezi Mungu aliiweka katika nafsi ya kila mwanadamu, hata kama baadhi ya watu watajaribu kuifuta na kuipuuza.

Na sisi hapa tunasikia na kuona jawabu kwa waombaji, na kupewa kwa waombaji, na kujibiwa kwa wenye haja kubwa, jambo ambalo linaashiria ushahidi wa yakini juu ya kuwepo kwa Mola Mtukufu.

Ushahidi wa kuwepo kwa Mwenyezi Mungu uko wazi zaidi na hauhitaji kutajwa na kuwekewa mipaka. Miongoni mwake ni:

Inajulikana kwa kila mtu kwamba kiumbe tukio (nalo ni kile kilichotokea baada ya kutokuwepo), lazima liwe na mwenye kulitokeza (yaani, aliyelifanya). Na viumbe hivi vingi na ambavyo tunavyoviona kila wakati lazima vina muumba aliyevifanya kuwepo. Naye ni Mwenyezi Mungu, Mwenye Nguvu, Mtukufu. Kwa sababu, haiwezekani kwamba viliumbwa bila ya muumba aliyeviumba, kama vile haiwezekani kwamba vilijiumba vyenyewe. Kwa sababu, kitu hakijiumbi. Kama alivyosema Yeye Mtukufu, "Au hawakuumbwa na chochote, au ni wao ndio waumbaji?" (At-Tur: 35) Na maana ya Aya ni kwamba wao hawakuumbwa bila ya muumba, wala wao sio waliojiumba wenyewe, basi inabakia tu kwamba ni lazima muumba wao ni Mwenyezi Mungu, Mwingi wa baraka, Mtukufu.

Hakika, mpangilo mzuri wa ulimwengu huu pamoja na mbingu yake na ardhi yake, pamoja na galaksi zake, nyota zake, sayari zake, pamoja na bahari zake ndogo, bahari zake kuu, na mito yake, pamoja na milima yake, na tambarare zake, na miti yake, pamoja na viumbe vyake vyote vya ajabu, vinaonyesha kuonyesha kwa hakika kwamba ulimwengu huu una muumba mmoja. Naye ni Mwenyezi Mungu, Mtakatifu, Mtukufu, "Huo ndio ufundi wa Mwenyezi Mungu aliyetengeneza vilivyo kila kitu."(Al-Naml: 88)

Kwa hivyo, sayari hizi na nyota - kwa mfano - husoga kwenye mfumo uliowekwa imara ambao hauharibiki. Na kila sayari inasonga katika mzunguko ambao haiukiuki wala haiuzidi. Yeye Mtukufu anasema, "Haliwi jua lenye kuufikia mwezi, wala usiku kuupita mchana. Na vyote vinaogelea katika njia zao." (Yasin: 40)

Umemaliza somo kwa ufanisi


Anza mtihani