Sehemu ya sasa:
Somo Mbinu za kujikingia za kisheria
Pamoja na kuongezeka kwa wimbi la hofu kati ya watu kutokana na maradhi na magonjwa ya milipuko, Muislamu, pamoja na kuzingatia sababu za kihisia, pia anajikinga kwa kufanya visababishi vya kisheria.
Jambo la kwanza na muhimu zaidi ambalo muumini anajikinga kwalo katika majanga na misiba ni kumkimbilia Mwenyezi Mungu na kujikinga kwake katika kuzuia dhiki hizo. Yusuf, amani iwe juu yake, wakati mke wa Mheshimiwa yule wa Misiri alipomtamani kinyume cha nafsi yake: "(Yusuf) akasema: Audhubillahi (Najikinga na Mwenyezi Mungu)." (Yusuf: 23) Na Mariam, amani iwe juu yake, wakati Jibril alipojifananisha kwake sawa na mtu: (Maryamu) akasema: "Hakika mimi ninajikinga kwa Mwingi wa rehema aniepushe nawe." (Maryam: 18)
Kuomba Mwenyezi Mungu dua kwa unyenyekevu, kujidhalilisha na kuonyesha kuhitaji kwake, ili aondoe balaa na wasiwasi hiyo. Kwani dua ndiyo ngome na silaha ya Mwislamu. Kwa maana balaa hiyo ilitokana na mipangilio ya Mwenyezi Mungu, basi hakuna kinachoweza kuizuia isipokuwa dua. Amesema Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Hakuna kinachoweza kuzuia mipangilio ya Mwenyezi Mungu isipokuwa dua." (Tirmidhi 2139)
Mtu anapaswa kutafuta ponya kwayo, kwani ndiyo dawa ya magonjwa yote ya kihisia na yasiyokuwa ya kihisia. (Al-Israa: 82) Kwa imani, yakini na ukweli, sababu za uponyaji huongezeka kwa sababu ya maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Sema: Hii Qur-ani ni uwongofu na poza kwa wenye kuamini." (Fussilat: 44)
Qur-ani yote ni uponyaji. Lakini baadhi ya sura na aya zina fadhila maalumu kuliko zingine; kama vile Suratul-Fatiha, suratul-Falaq, Suratun-Nas, na Ayatul-Kursi. Ibn Al-Qayyim, Mwenyezi Mungu amrehemu, alisema: "Kama mja angejitibu vizuri na Al-Fatiha, basi angeona athari yake ya ajabu katika uponyaji. Nilikaa Makka kwa muda na nikagonjeka, na sikuweza kupata daktari wala dawa. Kwa hivyo nilikuwa nikijitibu kwa Al-Fatiha, na ninaiona ikiwa na athari ya ajabu, kwa hivyo nikawa ninamwelezea hivyo mtu ambaye anaumwa; na wengi wao walikuwa wakipona haraka."
Hasa, swala ya Fajr, kwa kauli ya Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Mwenye kuswali (swala ya) Subhi, basi atakuwa katika ulinzi wa Mwenyezi Mungu." (Muslim 657)
Miongoni mwa ngome muhimu ni kuomba dua wakati unawaona wagonjwa na watu wenye balaa. Katika hadithi, Nabii alisema: "Yeyote anayemwona mtu anayeteseka, na akasema: 'Sifa njema ni za Mwenyezi Mungu ambaye ameniepusha na kile alichokupa mtihani, na akaniboresha mimi kuliko wengi miongoni mwa aliowaumba,' basi hatapatwa na balaa hiyo." (Tirmidhi 3432).
Katika kudumisha kumdhukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu kuna heri nyingi katika maisha haya na malipo makubwa katika Akhera. Na nyiradi za asubuhi na jioni ni miongoni mwa nyiradi muhimu zaidi ambazo Muislamu anapaswa kuzidumisha. Miongoni mwa faida zake ni: kukunjuka kwa kifua, utulivu wa moyo, kuwa pamoja na Mwenyezi Mungu Mtukufu, na Mwenyezi Mungu kumtaja mja huyo mbele ya waja watukufu wa juu.
Miongoni mwa dua, nyiradi na kinga za kisheria ni kama ifuatavyo:
Kusoma Ayatul-Kursi kabla ya kulala:
Imekuja katika Hadithi kwamba msemaji mmoja alimwambia Abu Huraira, Mwenyezi Mungu amridhie: "Kila wakati unapoenda kwenye malazi yako (kulala), soma Ayatul-Kursi; Mwenyezi Mungu atakuekea mlinzi ambaye ataendelea kuwa pamoja nawe, na hakuna shetani yeyote atakayekukaribia mpaka ufike asubuhi." Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, akasema: "Hakika yeye amekwambia ukweli, ingawa yeye ni mwongo wa waongo. Huyo alikuwa Shetani." (Al-Bukhari 3275)
Kusoma aya mbili za mwisho za Surat Al-Baqara:
Imesimuliwa kutoka kwa Abu Mas'ud, Mwenyezi Mungu amridhie, kuwa: Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alisema: "Mwenye kusoma zile aya mbili za mwisho za Suratul Baqara usiku, basi zitakuwa ni zenye kumtosheleza." (Bukhari 5008, Muslim 808)
Kumsifu Mwenyezi Mungu kwa wingi, na kuomba msamaha:
Ikiwa mja atadumu katika kumsifu Mwenyezi Mungu na kumuomba msamaha, basi Mwenyezi Mungu atamwondolea shari na balaa. Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: "Na Mwenyezi Mungu hakuwa wa kuwaadhibu nawe umo pamoja nao, wala Mwenyezi Mungu si wa kuwaadhibu na hali ya kuwa wanaomba msamaha." (Al-Anfal: 33)