Endelea kujifunza

Umeshaingia
Jisajili sasa kwenye jukwaa la Taa ili uanze kujifunza, na fuatialia maendeleo yako, na kukusanya pointi, na uingie kwenye mashindano.Baada ya kujisajili, utapata cheti cha kielektroniki katika mada ambazo utajifunza.

Sehemu ya sasa:

Somo Riba

Katika somo hili, tutajifunza kuhusu maana ya riba na baadhi ya hukumu zinazohusiana nayo katika sheria ya Kiislamu.

  • Kujifunza kuhusu riba na hukumu yake katika sheria ya Kiislamu.
  • Kujua hekima ya kuharamishwa riba.
  • Kubainisha madhara ya riba.
  • Kubainisha jinsi ya kutubia kutokana na riba.

Hekima ya Mwenyezi Mungu ilitaka kwamba riba iwe ni miongoni mwa mambo makubwa yaliyoharamishwa katika sheria ya Kiislamu. Na pia ilikuwa imeharamishwa kwa umma waliotutangulia, kwa sababu ya uharibifu wake mkubwa na balaa yake kwa jamii na watu binafsi. Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: "Basi kwa dhuluma yao Mayahudi tuliwaharimishia vitu vizuri walivyohalalishiwa. Na kwa sababu ya kuwazuilia kwao watu wengi njia ya Mwenyezi Mungu. Na kuchukua kwao riba, nao walikwisha katazwa hilo..." [An-Nisaa: 160, 161]

Miongoni mwa yale yanayobainisha hatari za riba ni tishio kali lililokuja kuhusiana nayo. Mwenyezi Mungu aliyetakasika, Mtukufu alisema: "Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na acheni riba zilizobakia, ikiwa nyinyi ni Waumini. Basi mkitofanya, jitangazieni vita na Mwenyezi Mungu na Mtume wake." [Al-Baqarah: 278, 279] Kwa hivyo aliyetakasika, Mtukufu akawa amekataza riba, akaiharamisha na akamuahidi adhabu anayejihusisha nayo.

Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alisisitiza kuhusu uharamu wake, na juu ya tishio kubwa lililokuja kuhusiana nayo. Imesimuliwa kutoka kwa Jabir, radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, kuwa alisema: "Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alimlaani mwenye kula riba (yani mwenye kuichukua), na mwenye kuilisha (riba) wengine (yani mwenye kuitoa), na mwandishi wake, na mashahidi wake wawili, na akasema, "Wao (wote) ni sawa (katika kupata dhambi)." (Muslim 1598)

Maana ya riba katika lugha ya Kiarabu

Maana ya riba kilugha ni: Kuongezeka na kukua. Miongoni mwa maana hizo ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Kwa kuwa ati taifa moja lina nguvu zaidi (ni jingi) kuliko jingine?" [An-Nahl: 92]. Yaani, wengi katika idadi.

Maana ya riba kisheria

Ama maana ya riba kisheria ni: vitu kushindana (kwa idadi au kipimo) na kuwepo muda katika vitu maalumu ambavyo Sheria iliviharamisha.

Aina za riba

١
Riba Al-Fadhl (Riba inayotokana na kuzidisha kipimo)
٢
Riba An-Nasia (Riba inayotokana na kuzidishwa muda wa kulipa deni)

Riba Al-Fadhl

Ni kuzidisha kipimo katika vitu ambavyo vilitajwa kwa jina, na vitu vinavyoweza kufungamanishwa na hivyo. Nayo nyogeza hiyo hutokea katika kubadilishana mali inayoingia katika hukumu ya riba kwa mali nyingine inayoingia katika hukumu ya riba. Kama vile kuuza pishi moja ya tende nzuri kwa pishi mbili za tende mbaya.

Riba An-Nasia

Hutokea kwa kuongeza muda ambao ubadilishanaji wa bidhaa ni lazima utimie ndani yake. Nayo ni kuchelewesha kupokea bidhaa au hela katika uuzaji wa vitu vya aina moja vyenye sababu moja ya kuvifanya kuwa riba Al-Fadhl. Kama vile kuuza Swaa’ (pishi) moja ya ngano kwa Swaa’ (pishi) moja ya shayiri na kuchelewesha kupokezana pishi hizo.

Hukumu ya riba

Riba imeharamishwa na Qur-ani, Sunna na makubaliano ya wanazuoni. An-Nawawi, Mwenyezi Mungu amrehemu, alisema: “Waislamu kwa pamoja walikubaliana kwamba riba imeharamishwa na kwamba ni miongoni mwa madhambi makubwa.” (Al-Majmuu' 9/391)

Hekima ya kuharamishwa riba

1- Kuhimiza shughuli za kiuchumi za kiuhakika: Hii ni kwa sababu mwenye kula riba hawekezi fedha zake katika kazi ya uzalishaji mali yenye manufaa kwake au kwa jamii; katika kilimo, viwanda, biashara au mengineyo.

2- Kuzuia kuchuma bila ya badili: Uislamu unadhibiti miamala ya kimali kwa njia ambayo inafanikisha kuwepo masilahi ya pande zote mbili. Kwani, kila mmoja wao hutoa kitu na anapokea kitu kama malipo kwake; na hili si kweli katika riba.

3- Kwamba riba inakata mambo mema miongoni mwa watu: Hili ni kinyume na madhumuni ya Uislamu ya kueneza wema na hisani miongoni mwao.

4- Kuzuia unyanyasaji: Mkopeshaji kwa kawaida hutumia hitaji la mkopaji kama fursa kwake; ili amkopeshe kwa riba.

5- Kuzuia dhuluma: Riba ni dhuluma kwa mmoja wa wahusika, na Mwenyezi Mungu ameharamisha aina zote za dhuluma.

Madhara ya riba

Madhara na hatari za riba ni makubwa, na yanaenea katika nyanja zote za maisha ya watu binafsi na jamii.

1- Madhara ya kimaadili na ya kiroho

Riba humfanya anayeamiliana nayo kuwa na mazoea ya ulafi, na kuwa na moyo mgumu, na kuwa mtumwa wa mali. Kwa hivyo, akawa anaruhusu kuwadhulumu wengine, na kuchukua fursa hiyo kuwanyanyasa watu kwa sababu ya mahitaji yao, udhaifu wao na ufukara wao. Kwa upande mwingine, huvunja moyo wa mtu anayehitaji mali, na kuikunja nafsi yake na ardhi pamoja na upana wake wote.

2- Madhara ya kijamii

Riba husababisha kuvunja jamii, kwani inazifanya kuvunjika na kugawanyika; wenye nguvu wakala vya walio dhaifu. Na hakuna mtu anayekubali kuwasaidia wengine isipokuwa kwa faida inayotarajiwa.

3. Madhara ya kiuchumi

Riba husababisha kuharibika kwa mfumo wa kiuchumi katika ngazi zote; watu wakalimbikiziwa madeni, na uzalishaji wa kweli na wenye manufaa katika jamii ukapunguka.

Masharti ya kutubia riba

١
Kukomesha shughuli zote zinazohusiana na riba.
٢
Kujutia kile kilichopatwa kutokana na shughuli za riba.
٣
Kuazimia sawasawa kutorudi kwenye dhambi hili.
٤
Kurudisha mali za ziada kwa mmiliki wake ikiwezekana. Lakini ikiwa hili haliwezekani, basi atoe sadaka na ampe masikini kutoka katika mali hii na pia anaweza kuitumia katika njia za heri.

Umemaliza somo kwa ufanisi


Anza mtihani