Endelea kujifunza

Umeshaingia
Jisajili sasa kwenye jukwaa la Taa ili uanze kujifunza, na fuatialia maendeleo yako, na kukusanya pointi, na uingie kwenye mashindano.Baada ya kujisajili, utapata cheti cha kielektroniki katika mada ambazo utajifunza.

Sehemu ya sasa:

Somo Al-Wadia' (kumwekea mtu kitu)

Katika somo hili, tutajifunza kuhusu maana ya Wadi'a katika sheria ya Kiislamu na hukumu zinazofungamana nayo.

  • Kujua maana ya Wadi'a na hekima yake.
  • Kujua hukumu za kisheria zinazohusiana na Wadi'a.

Maana ya Wadi'a

Ni mali wanazoweka watu kwa wengine ili wazihifadhi bila malipo, kama vile mtu kuweka kwa mwingine saa, gari, au pesa.

Hukumu ya Wadi'a (kuweka kitu)

Wadi'a ni mkataba unaoruhusiwa, na kila mmoja wa wana mkataba huu anaweza kuusitisha wakati wowote anapotaka. Na ikiwa mmiliki wake atataka kurudishiwa kitu hicho, basi itakuwa lazima kumrudishia. Na ikiwa aliyekuwa amekiweka atakirudisha kwa mmiliki wake, basi itamlazimu mmiliki wake kukichukua. Wadi'a inaingia katika mlango wa kusaidiana katika wema na uchamungu.

Hekima ya kuhalalisha Wadi'a

Kunaweza kuwa na hali ambazo mtu hawezi kuhifadhi mali yake - ima kwa sababu ya kutokuwa na mahali pazuri, au kwa sababu haiwezekani, kwa sababu ya kushindwa, ugonjwa, au hofu - naye mtu mwingine anaweza kuwa na uwezo wa kumhifadhia mali hiyo.

Hii ndiyo sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu akaruhusu Wadi'a, ili mali iweze kuhifadhiwa kwa upande mmoja na yule aliyekihifadhi apate malipo kwa upande mwingine. Katika hili kuna kuwarahisishia watu, na kuwasaidia kukidhi mahitaji yao.

Wadi'a imeruhusika kisheria, na msingi wa uhalali wake ni Kitabu, Sunna, makubaliano ya wanazuoni na Qiyas. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema, "Hakika Mwenyezi Mungu anawaamrisha kwamba mzirudishe amana kwa wenyewe." [An-Nisaa: 58]

Imesimuliwa kutoka kwa Abu Huraira - Mwenyezi Mungu awe radhi naye - kuwa alisema kwamba: Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - alisema, "Timiza amana kwa yule aliyekupa kuiweka, wala usimsaliti yule aliyekusaliti." (Abu Dawud, 3535)

Hukumu ya kukubali Wadi'a

Inapendekezwa kukubali Wadi'a (amana) kwa yule anayejua kwamba anaweza kuitunza, kwa sababu ya ushirikiano katika wema na uchaji Mungu ulio katika hilo, na kupata malipo kutoka kwa Mwenyezi Mungu katika kuitunza.

Nguzo za Wadi'a

١
Al-Mudi': Ni mmiliki wa amana.
٢
Al-Mustawda': Ni mlinzi wa amana.
٣
Al-Wadi'a: Ni kitu kilichohifadhiwa.
٤
Njia ya kuhitimisha mkataba: Ni kuwasilisha ofa na kukubali kuiweka kwa pande zote mbili.

Hali ambapo mweka amana atadhamini amana

١
Akipuuza kuilinda amana.
٢
Kuiweka amana hiyo kwa wengine bila udhuru wala ruhusa kutoka kwa mmiliki wake.
٣
Kuitumia amana hiyo, au kuifanyia atakavyo.

Hali ambazo Wadi'a inabadilika na kuwa yenye kudhaminiwa.

١
Kuichanganya na vitu vingine kwa njia ambayo haiwezi kutambulika.
٢
Ukiukaji katika jinsi ya kuiweka amana.
٣
Kuihamisha hadi katika mahali ambapo hapastahili kuihifadhi.

Ikiwa amana itaharibikia kwa aliyepewa kuilinda, naye hakuvuka mipaka, wala hakuipuuza, basi hapaswi kuidhamini. Lakini anapaswa kuihifadhi mahali ambapo mfano wa kitu hicho huhifadhiwa. Na ikiwa mmilki wake atamuidhinisha huyo anayeilinda kuituma, basi hiyo inabadilika na kuwa mkopo, ambao ni lazima kuurejesha.

Ikiwa kutakuwa na hofu, na huyo aliyepewa amana kuihifadhi akataka kusafiri, basi inamlazimu amrudishie amana hiyo mmiliki wake au wakili wake. Lakini ikiwa haitawezekana, basi ataipeleka kwa mtawala, ikiwa ni mwadilifu. Na ikiwa haiwezekani, basi ataiweka kwa mtu muaminifu ili airudishe kwa mmiliki wake.

Yeyote aliyepewa mali kuihifadhi, naye akaitoa katika mahali pake pa kuihifadhia, au akaichanganya na mali ya watu wengine kwa njia ambayo haitambuliki, kwa hivyo ikapotea yote au ikaharibika, basi hapo ataidhamini.

Mtu aliyepewa amana kuihifadhi anapaswa kuaminiwa, na hapaswi kudhamini isipokuwa akivuka mipaka au kuipuuza. Inafaa kuikubali kauli ya huyo aliyepewa kuweka pamoja na kiapo chake ikiwa atasema kwamba aliirudisha amana hiyo, au ikiwa atadai kwamba iliharibika, na kwamba hakuipuuza, mradi hakuna ushahidi wowote dhidi yake.

Hukumu ya kurejesha amana

Wadi'a ni amana anayopewa mtu kuihifadhi, ambayo ni lazima kuirudisha wakati mwenyewe anaitaka. Na ikiwa hatairudisha baada ya mwenyewe kumtaka airudishe bila ya udhuru, kisha ikaharibika, basi hapo analazimika kuidhamini. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema, "Hakika Mwenyezi Mungu anawaamrisha kwamba mzirudishe amana kwa wenyewe." [An-Nisaa: 58]

Ikiwa amana ni ya zaidi ya mtu mmoja, na mmoja wao akaomba sehemu yake ya kipimo, uzito au hesabu na ikawezekana kuigawanya, basi atapewa sehemu yake hiyo.

Hali mbalimbali ambazo mkataba wa amana huishia

١
Ikiwa mmiliki wake atataka arejeshewe amana yake, au ikiwa aliyekuwa anaihifadhi atairejesha.
٢
Ikiwa umiliki wa amana hiyo utahamishwa hadi kwa wengine kwa kuiuza au kupeanwa kama zawadi.
٣
Ikiwa uwezo wa mweka amana au mwenye kitu hicho utakosekana.
٤
Ikiwa mmoja wa wana mkataba hao atakufa.

Umemaliza somo kwa ufanisi


Anza mtihani