Endelea kujifunza

Umeshaingia
Jisajili sasa kwenye jukwaa la Taa ili uanze kujifunza, na fuatialia maendeleo yako, na kukusanya pointi, na uingie kwenye mashindano.Baada ya kujisajili, utapata cheti cha kielektroniki katika mada ambazo utajifunza.

Sehemu ya sasa:

Somo Adabu za kuchamba na kukidhi haja ya asili

Sheria haikuacha jambo analokabiliana nalo Muislamu isipokuwa ilimwekea adabu na vidhibiti. Miongoni mwa mambo haya ni adabu zinazohusiana na kukidhi haja ya asili. Katika somo hili, utajifunza kuhusu adabu za kukidhi haja ya asili na kuchamba, aina za hadathi na kusafisha kila moja yake.

  • Kujua adabu za kukidhi haja ya asili na kuchamba.
  • Kujua aina za hadathi.
  • Kujua jinsi ya kujisafisha kutokana na hadathi.

Adabu za kukidhi haja ya asili

Inapendekezwa kwa mtu anayetaka kuingia mahali pa kukidhi haja ya asili (choo) kuutanguliza mguu wake wa kushoto na aseme: “Kwa jina la Mwenyezi Mungu. Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na majini wa kiume na majini wa kike."

Sikiliza dua ya kuingia chooni

Anapotoka humo, anautanguliza mguu wake wa kulia na aseme, "Ninaomba unifutie dhambi.”

Muislamu analazimika kusitiri sehemu zake za siri ili asionwe na watu anapokidhi haja ya asili.

Ni haramu kwake kukidhia haja yake ya asili mahali ambapo watu wanadhurika kwayo.

Ni haramu kwake akiwa kwenye nchi kavu kukidhia haja yake ya asili kwenye shimo, kwa sababu ya wanyama ambao wanaweza kuwa humo akawadhuru na wakamdhuru.

Anafaa kutoelekea Kibla wala kuipa mgongo wakati wa kukidhi haja yake ya asili. Lakini akiwa kwenye nchi kavu, na hakuna ukuta wa kumsitiri, basi hilo linakuwa ni lazima juu yake. Hii ni kwa kauli yake Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, “Mkiijia sehemu ya kukidhi haja ya asili kwenye nchi kavu, basi msielekee Kibla, wala msikipe mgongo kwa mkojo wala haja kubwa.” (Bukhari 394, Muslim 264)

Pia inamlazimu awe mwangalifu asiruhusu uchafu wowote kumrukia kwenye nguo au mwili wake, na ni lazima aoshe chochote kinachomrukia katika hayo.

Anapokidhi haja yake, basi linamlazimu moja ya mambo haya mawili:

١
Kuchamba (Kujisafisha kwa maji)
٢
Kujisafisha kwa mawe

Kuchamba

Ni kusafisha kwa maji mahali panapotokea mkojo na kinyesi.

Istijmaar

Ni kusafisha sehemu ambayo mkojo na kinyesi hutokea kwa karatasi ya shashi au mawe matatu au zaidi au mfano wa hivyo ambavyo vinaweza kusafisha najisi kutoka kwa mwili.

Hadathi mbalimbali

Ni hali isiyokuwa ya kihisia inayompata mtu, ambayo inamzuia kuswali kabla ya kujisafisha, nayo ni tofauti na kitu cha kihisia kama vile najisi.

Maji safi

Hadathi humuondokea Muislamu anapotawadha au kuoga kwa maji safi. Maji safi ni maji ambayo hayakuchanganyika na najisi na kuathiri rangi yake, ladha yake, au harufu yake.

Hadathi imegawanyika katika sehemu mbili:

١
Hadathi ndogo: Ni hadathi inayomlazimu Muislamu kutawadha ili kuiondoa kwenye mwili wake.
٢
Hadathi kubwa: Ni hadathi inayomlazimu Muislamu aoge na kufikisha maji kwenye mwili wake wote ili kuiondoa.

Hadathi dogo na kutawadha ili kuiondoa

Mwislamu anapopatwa na hadathi ndogo, atalazimika kutawadha kwa ajili ya swala. Mifano ya hadathi (uchafu) ndogo ni mambo yanayoharibu wudhuu:

1. Mkojo, kinyesi, na kila kitokacho katika tupu yake, kama vile upepo. ”Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kutaja kinachobatilisha usafi: "au mmoja wenu ametoka chooni." (An-Nisa: 43) Naye Nabii, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani ziwe juu yake, alisema kuhusiana na mwenye shaka kuwa ameharibu wudhuu wake wakati wa swala: “Asiondoke mpaka asikie sauti au apate harufu.” (Al-Bukhari 175, Muslim 361)

2. Kugusa sehemu za siri kwa matamanio bila kizuizi chochote. Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, alisema: “Yeyote anayegusa uume wake, basi na atawadhe.” (Abu Dawud 181)

3. Kula nyama ya ngamia. Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimfikie, aliulizwa: "Je, nitawadhe kwa sababu ya kula nyama ya ngamia? Akasema: “Ndiyo.” (Muslim 360)

4. Kupoteza akili kutokana na usingizi, wazimu, kuzimia, au kulewa.

Umemaliza somo kwa ufanisi


Anza mtihani