Sehemu ya sasa:
Somo Wudhuu
:idadi wanafunzi wengine walimaliza somo hili
Fadhila ya wudhuu
Je, ninatawadha vipi na ninaondoa vipi hadathi ndogo?
Nia
Inapendekezwa kwamba aoshe mikono yake kwa maji mara tatu.
Atasukutua mdomo wake kwa maji, nalo hili ni kuingiza maji mdomoni na kuyazungusha humo sawasawa, kisha ayatoe. Inapendekezwa afanye hivyo mara tatu, lakini mara moja tu ndio wajibu.
Atapandisha maji puani, kisha ayatoe kwa kusukuma nje hewa inayotoka puani. Na inapendekezwa azidishe katika kufanya hivyo isipokuwa ikiwa hilo litamletea madhara au ikiwa atakuwa amefunga saumu. Na inapendekezwa kwamba arudie hilo mara tatu, lakini mara moja tu ndiyo wajibu.
Ataosha uso wake kutoka juu ya paji la uso, kutokea kwenye sehemu ambayo nywele zinaishia hadi chini ya kidevu, na kutokea kwenye sikio moja hadi sikio lingine. Maskio sio kiungo katika uso. Na inapendekezwa kwamba afanye hivyo mara tatu, lakini mara moja tu ndio lazima.
Ataosha mikono yake kuanzia ncha za vidole mpaka kwenye kiwiko. Kiwiko ni pale ambapo dhiraa inaungana na mkono wa juu, na viwiko vyenyewe vinajumuishwa katika kuosha huko. Inapendekezwa aanze na sehemu ya kulia na kurudia kuosha mara tatu, lakini mara moja tu ndio wajibu.
Atapangusa kichwa chake kwa kulowesha mikono yake kwa maji, kisha atapangusa kichwa chake kuanzia sehemu ya mbele ya kichwa hadi nyuma ya kichwa kwenye sehemu iliyo karibu na shingo. Ni Sunna kupangusa kwa kurudisha mikono yake mbele ya kichwa tena. Na haipendekezwi kurudia hili mara tatu, kama ilivyo katika sehemu zingine, badala yake alifanye mara moja tu.
Baada ya kupangusa kichwa chake, atapangusa masikio yake kwa kuingiza vidole vyake viwili vya shahada kwenye masikio yake , na kupangusa sehemu ya nje ya masikio yake kwa vidole gumba.
Ataosha miguu yake pamoja na visigino, ambayo ni mifupa miwili iliyojitokeza kwenye kila upande wa mguu ambapo muundi unakutana na wayo. Ataanza na sehemu ya kulia na inapendekezwa kurudia kuosha mara tatu, lakini mara moja tu ndio wajibu. Ikiwa amevaa soksi, inaruhusika kwake kupangusa tu juu yake, lakini kwa kuzingatia masharti ya kufanya hivyo.