Sehemu ya sasa:
Somo Swala ya Jamaa (mkusanyiko)
Mwenyezi Mungu aliwaamrisha watu kuswalia katika mkusanyiko katika swala tano, na yametajwa malipo makubwa katika hilo. Amesema Nabii - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, "Swala ya mkusanyiko ni bora zaidi kuliko swala ya mtu mmoja kwa daraja ishirini na saba." (Al-Bukhari 645, Muslim 650)
Mkusanyiko wa chini zaidi ni watu wawili: Imamu na anayemfuata. Kila mkusanyiko unapokuwa mkubwa, basi hilo linapendeza zaidi kwa Mwenyezi Mungu.
Maana ya kumfuata imamu katika swala
Maana yake ni mtu anayemfuata imamu katika swala kuifungamanisha swala yake na imamu wake, kwa kumfuata katika kurukuu na kusujudu, na kusikiliza kisomo chake, wala asimtangulie au kumhalifu katika lolote kati ya hayo, bali anapaswa kufanya kila kitendo baada ya imamu wake mara moja.
Kumfuata Imamu
Nabii - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - alisema, "Hakika Imamu aliwekwa ili afuatwe. Kwa hivyo, anapotoa takbira, basi toeni takbira, wala msitoe takbira hadi atoe takbira. Na anaporukuu, basi rukuuni, wala msirukuu hadi arukuu. Na anaposema: Mwenyezi Mungu amemsikia mwenye kumsifu, semeni, 'Ewe Mwenyezi Mungu, Mola wetu Mlezi, sifa njema zote ni zako.' Na anaposujudu, basi sujuduni, wala msisujudu mpaka asujudu." (Al-Bukhari 734, Muslim 411, Abu Dawud 603, na lafudhi hii ni yake)
Mtu anayefaa kutangulizwa kuwa imamu ni yule ambaye amehifadhi zaidi Kitabu cha Mwenyezi Mungu na mwenye usomaji bora zaidi, kisha aliye bora zaidi, kisha aliye bora zaidi. Kama alivyosema Mtume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie: "Anapaswa kuwa imamu wa watu yule ambaye ndiye msomi wao zaidi wa Kitabu cha Mwenyezi Mungu. Na ikiwa wako sawa katika usomaji, basi ni yule wao ajuaye zaidi Sunna." (Muslim 673)
Imamu anapaswa kusonga mbele, nao maamuma wasimame kwa safu sawasawa nyuma yake. Wanapaswa kukamilisha safu ya kwanza kisha inayofuata. Ikiwa maamuma ni mmoja, basi atasimama upande wa kulia wa imamu.
Mwenye kujiunga na Imamu baada ya kupitwa na baadhi ya swala, atajiunga tu naye mpaka Imamu atoe salamu ya kumaliza swala, kisha huyo atanyanyuka na akamilishe swala yake iliyobakia.
Mwenye kupata rukuu pamoja na imamu, basi atakuwa amepata rakaa hiyo kikamilifu. Na mwenye kupitwa na rukuu, basi atakuwa amepitwa na rakaa hiyo na rakaa zote za kabla yake, lakini inamlazimu ajiunge pamoja na imamu katika swala hiyo hivyo. Imamu atakapotoa salamu ya kumaliza swala, aliyepitwa huyo atanyanyuka na aswali kile alichokosa katika swala pamoja na Imamu.
Mifano ya yule aliyekosa mwanzo wa swala pamoja na Imamu
Mwenye kupata imamu katika swala ya alfajiri katika rakaa ya pili, itamlazimu baada ya imamu kutoa salamu anyanyuke ili akamilishe rakaa iliyobakia juu yake, na wala asitoe salamu mpaka aimalize; kwa sababu swala ya alfajiri ni rakaa mbili, naye hakupata isipokuwa rakaa moja tu.
Mwenye kumpata imamu ilhali yuko katika Tashahhud ya mwisho katika swala ya Maghrib, basi inamlazimu baada ya imamu kutoa salamu aswali rakaa tatu kamili; kwa sababu alimkuta Imamu katika Tashahhud ya mwisho, lakini rakaa inapatwa kwa kupata kurukuu pamoja na Imamu.
Mwenye kumkuta Imamu wakati yuko katika rukuu ya rakaa ya tatu ya swala ya Dhuhr, basi atakuwa amepata rakaa mbili pamoja na Imamu (ambazo kwa imamu ni rakaa mbili za kwanza za Dhuhr). Na Imamu atakapotoa salamu, basi itamlazimu huyu anyanyuke na atimize kilichobakia juu yake, ambacho ni rakaa ya tatu na ya nne; kwa sababu Dhuhr ni swala ya rakaa nne.