Sehemu ya sasa:
Somo Shirki
Maana ya shirki
Ushirikina ni kumfanyia Mwenyezi Mungu Mtukufu mshirika katika umola wake, uungu wake, au majina na sifa zake.
Mifano ya ushirikina
Hatari ya ushirikina
Ushirikina unapingana na imani ya uungu wa Mwenyezi Mungu peke yake. Ikiwa kuamini uungu wa Mwenyezi Mungu peke yake na kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika ibada ndiyo wajibu muhimu na kubwa zaidi, basi ushirikina ndiyo dhambi kubwa zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu. Nao ndiyo dhambi moja tu ambayo Mwenyezi Mungu haisamehe isipokuwa kwa toba. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu: "Hakika Mwenyezi Mungu hasamehe kushirikishwa, na husamehe yaliyo duni ya hilo kwa amtakaye.” (An-Nisa: 48) Na alipoulizwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: Ni dhambi ipi iliyo kubwa zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu? Akasema: “Ni kumfanyia Mwenyezi Mungu mwenza ilhali yeye ndiye aliyekuumba.” (Al-Bukhari 4477, Muslim 86)
Ushirikina unaharibu utiifu wote na unaubatilisha. Kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema: "Na lau wangelimshirikisha, yangeliwaharibikia waliyokuwa wakiyatenda." (Al-An’am: 88)
Ushirikina unamlazimu mwenye ushirikina huo kudumu milele katika moto wa Jahannam. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Kwani anayemshirikisha Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu atamharimishia Pepo, na mahala pake ni Motoni." (Al-Maida: 72)
Aina za shirki
Ni mja kuelekeza ibada yake kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Kila neno au tendo miongoni mwa ibada miongoni mwa mambo anayoyapenda Mwenyezi Mungu, ikiwa litaelekezwa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu, basi huo ni ushirikina na ukafiri. Mfano wa shirki kubwa ni pale mtu anapomuomba asiyekuwa Mwenyezi Mungu; akamwomba amponye maradhi yake, au amkunjulie riziki yake, na vile vile ikiwa mtu atamtegemea asiyekuwa Mwenyezi Mungu, au kumswalia asiyekuwa Mwenyezi Mungu, au akachinja kwa ajili ya asiyekuwa Mwenyezi Mungu.
Kwa hivyo, kuelekeza dua hizi, matendo haya na mfano wa haya kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu ni ushirikina na ukafiri. Kwa sababu uponyaji na riziki ni miongoni mwa sifa za umola. Na kumtegemea Mwenyezi Mungu, kuswali kwa ajili yake, na kumchinjia ni katika kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika uungu wake.
2- Shirki Ndogo
Ni kila neno au kitendo ambacho ni njia ya kufikia ushirikina mkubwa, na njia ya kuingia humo.
Mifano ya shirki ndogo
Je, kuwauliza watu na kuwaomba ni shirki?
Uislamu ulikuja kuikomboa akili ya mwanadamu kutokana na ushirikina, itikadi potofu na udanganyifu, na mwanadamu kujikomboa kutokana na kumnyenyekea asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, hairuhusiki kumuomba maiti au kitu kisicho na uhai, na kukinyenyekea na kujidhalilisha kwake hata kidogo. Hilo ni katika ushirikina na itikadi potofu. Ama kumuomba mtu aliye hai, aliyepo kitu anachoweza, kama vile kumsaidia au kumuokoa kutokana na kuzama, au kumuomba amuombee Mwenyezi Mungu, basi hayo yanaruhusika.
Kuomba na kuitisha kitu kutoka kwa kitu kisicho na uhai au maiti kunachukuliwa kuwa ni shirki inayokiuka akili, Uislamu na imani. Kwa sababu vitu vilivyokufa na visivyo na uhai haviwezi kusikia ombi hilo wala kuliitikia. Hii ni kwa sababu dua ni ibada, na kuielekeza kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu ni shirki. Na shirki ya Waarabu wakati Mtume alipopewa utume ilikuwa kuomba vitu visivyo na uhai na vilivyokufa.