Sehemu ya sasa:
Somo Kumuosha maiti na kumvalisha sanda
:idadi wanafunzi wengine walimaliza somo hili
Ni nini kinapendekezwa kufanya Muislamu anapokufa?
Mtume, rehema na amani za Mweneyzi Mungu zimshukie, alipoingia alimokuwa Abu Salama huku macho yake yako wazi, alimfumba macho na akasema: “Mnapowahudhuria maiti wenu, basi wafumbeni macho.” (Ibn Majah 1455)
2. Uvumilivu na kujidhibiti nafsi
Kama Mtume, rehema na amani zimshukie alivyomfanyia Abu Salama, mmoja wa maswahaba wake watukufu alipofariki, na akasema: “Hakika, roho inapochukuliwa, macho yanaifuata." Kisha akasema, "Ewe Mwenyezi Mungu! Msamehe Abu Salama, na ipandishe daraja yake katika waongofu, na uweke badili yake kwa aliyowacha nyuma, na utusamehe sisi na yeye, ewe Mola Mlezi wa walimwengu wote, na umkunjulie katika kaburi lake, na umtilie mwangaza ndani yake.” (Muslim 920)
Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za mwenyezi Mungu zimshukie: “Iharakisheni jeneza. Ikiwa ni mtu mwema, basi ni heri mnayoitanguliza kwake. Na ikiwa ni kinyume chake, basi hiyo ni shari (mliyoibeba, na ambayo mnatakiwa kwa haraka) muishushe kutoka kwenye shingo zenu." (Al-Bukhari 1315, Muslim 944)
5. Kuwasaidia wana familia ya maiti
Ni lazima maiti aoshwe kabla ya kuvikwa sanda na kuzikwa. Ataoshwa na mmoja wa familia yake, jamaa yake, au Waislamu wengineo. Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, alioshwa alipofariki, ilhali yeye ndiye safi zaidi aliyesafishwa na Mwenyezi Mungu.
Katika kuosha maiti, inafaa kueneza maji kwenye mwili mzima, kumuondolea uchafu wowote ikiwa utapatikana, pamoja na kujali sana suala la kusitiri sehemu zake za siri wakati wa kumuosha. Inapendekezwa kuzingatia mambo yafuatayo:
1. Kufunika sehemu zake za siri: kati ya kitovu chake na magoti yake, baada ya kumvua nguo zake.
2. Muoshaji atavaa glavu au kitambaa kwenye mkono wake wakati wa kuosha sehemu za siri za maiti.
3. Kuanza kwa kuondoa uchafu na najisi kutoka kwenye mwili wa maiti.
4. Kisha huosha viungo vya wudhuu kwa utaratibu wake sahihi unaojulikana.
5. Kisha kuosha kichwa chake na mwili wote. Inapendekezwa kuuosha kwa mkunazi au kwa sabuni, na kisha atamiminiwa maji baada ya hayo.
6. Inapendekezwa kuosha kwanza upande wa kulia, kisha upande wa kushoto.
7. Inapendekezwa kumuosha mara tatu au zaidi ikiwa kuna haja ya kufanya hivyo.
8. Kumuwekea kitambaa au pamba
Inapendekezwa kumpaka maiti manukato wakati wa kumwosha na baada ya kumwosha. Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, aliwaamrisha wale waliokuwa wanamuosha binti yake, Zainab kwamba watie kafuri katika muosho wa mwisho. (Al-Bukhari 1253, Muslim 939)
Ni nani anayefaa kumwosha maiti?
Aisha radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake alisema: “Lau ningeweza kujua hali yangu ya mbeleni, yale ambayo nimeshajua, basi Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, asingeoshwa na yeyote isipokuwa wake zake.” (Abu Dawud 3141 Ibn Majah 1464)
Kumkafini maiti kwa vazi linalomsitiri ni katika ya haki za wajibu kwake juu ya familia yake na waislamu wote. Nayo ni faradhi ya kutoshelezana, kwa kauli ya Mtume, rehema na amani zimshukie: "Vaeni katika nguo zenu ambazo ni nyeupe. Kwani hizo ndizo bora katika nguo zenu, na wakafinini kwazo maiti wenu." (Abu Dawud 3878)