Sehemu ya sasa:
Somo Maisha ya Nabii Muhammad, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake
Inamlazimu Muislamu kujua kwa kina maisha ya Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, ili aweze kumuiga katika mambo yote ya maisha yake, kwani maisha yake yalikuwa ni utekelezaji wa hukumu za Uislamu na sheria zake. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Hakika nyinyi mnayo ruwaza njema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa anayemtaraji Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho." (Al-Ahzab: 21)
1. Nasaba ya Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake
Nasaba ya Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, ndiyo nasaba bora zaidi na tukufu zaidi. Yeye ni Muhammad ibn 'Abdillah, ibn 'Abdul-Muttalib ibn Hashim, ibn 'Abd Manaf, ibn Qusay, ibn Kilab, ibn Murra, ibn Ka'b, ibn Lu'ay, ibn Ghalib, ibn Fihr, ibn Malik, ibn an-Nadhr, ibn Kinana, ibn Khuzayma, ibn Mudarika, ibn Ilyas, ibn Mudhar, ibn Nizar, ibn Ma'd ibn Adnan. Naye Adnan ni katika wana wa Ismail, amani iwe juu yake.
2. Wazazi wake
Baba yake ni Abdullah bin Abdul Muttalib bin Hashim. Alifariki hali ya kuwa Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, bado yuko tumboni mwa mama yake.
3. Kuzaliwa kwake
Alizaliwa Jumatatu katika mwezi wa Rabi 'al-Awwal, mwaka wa tembo, unaolingana na 571 miladiya.
4. Kunyonyeshwa kwake
Alinyonyeshwa siku kadhaa na Thuwaiba, kijakazi wa Abu Lahab, kisha akanyonyeshwa na Halima as-Saadiya kutoka kwa Bani Sa'd, na akaishi naye huko katika Bani Sa'd kwa miaka minne takriban. Moyo wake ulipasuliwa huko, na fungu la shetani likatolewa katika nafsi yake, kisha Halima akamrudisha kwa mama yake baada tu ya hilo kufanyika.
5. Malezi na ujana wake
Kazi yake kabla ya kupewa utume
Maisha ya Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, kabla ya utume yalikuwa maisha mema na matukufu ambayo hayakuwa na mapungufu yoyote wala makosa. Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, aliinukia hali ya kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu amemzunguka na ulezi wake akimlinda kutokana na uchafu wa zama za ujinga, mpaka akawa mbora zaidi wa watu wake katika mwenendo, tabia na mtukufu zaidi wa hadhi, ujirani, ustahamilivu, mkweli wao zaidi katika mazungumzo, mwenye amana kubwa zaidi, wa mbali wao zaidi na machafu na tabia zenye kuchafua wanaume, mpaka akajulikana kwao kwamba yeye ni “mkweli na mwaminifu."
6. Wake wa Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake
Mtume, rehema na amani zimshukie, alimwoa Khadija, Mwenyezi Mungu amuwie radhi, alipofikia umri wa miaka ishirini na tano, alipotoka kwenda huko Sham kufanya biashara pamoja na mtumishi wake Khadija aitwaye Maysara. Basi Maysara akaona cha kumshangaza mno kuhusiana na mambo yake, kama vile ukweli na uaminifu. Aliporudi, akamjulisha bibi yake yale aliyoyaona. Basi Khadija akataka amuoe. Na yeye ndiye aliyekuwa mwanamke wa kwanza ambaye Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake alioa, na hakuwahi kumuoa mwengine mpaka Khadija alipokufa. Naye Khadija, radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake alikuwa ndiye mama wa watoto wake wote isipokuwa Ibrahim. Na alifariki miaka mitatu kabla ya Hijra.
Majina ya wake za Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake
7. Watoto wa Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake
Watoto wake ni saba kulingana na kauli iliyo sahihi: watatu wa kiume na wanne wa kike.
Watoto wake wa kiume ni watatu: Al-Qasim, na Nabii aliitwa jina lake la utani kwa huyu mwanawe, lakini aliishi siku chache tu kisha akafa. Na Abdullah ambaye alipewa jina la utani la At-Twahir (aliye safi), At-Tayyib (mzuri). Na katika watoto wake pia ni Ibrahim.
Binti zake ni wanne: Zainab, ambaye ndiye binti yake mkubwa, Ruqayya, Umm Kulthum na Fatima. Kwa hivyo, watoto wa kiume na wa kike wa Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, wote walikuwa kutoka kwa mkewe, mama wa waumini, Khadija, Mwenyezi Mungu amridhie, isipokuwa Ibrahim. Kwani yeye alikuwa kutoka kwa suria wa Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, anayeitwa Mariya, mwanamke wa Kikoptiki, ambaye Muqawqas alimpa Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake.