Sehemu ya sasa:
Somo Maadili ya Kiislamu katika Miamala inayohusiana na mali
Maadili yanahusiana kwa ukaribu na mambo yote ya maisha. Miongoni mwa mambo muhimu zaidi yanayoutofautisha mfumo wa kifedha wa Kiislamu na mifumo mingineyo ni maadili yaliyo ndani yake na ambayo inayatunza. Hili ndilo linaloufanya mfumo wa kifedha wa Kiislamu kuwa wa kipekee kuliko mifumo mingineyo.
Ni ambayo yote ambayo Sheria ya Kiislamu inaruhusu kufanya ili kuchuma mapato halali. Yanajumuisha shughuli zinazohusiana na mali zinazojumuisha mikataba yote ambayo inategemea mali au haki za kimali zinatokana nazo. Kama vile uuzaji, ununuzi, kukodisha, kampuni, na mikataba mingineyo. Hukumu zinazohusiana na miamala ya Kiislamu ni hukumu za kisheria zinazodhibiti miamala ya watu ya kimali na kiuchumi.
Malengo ya miamala ya kimali ya Kiislamu
Uislamu ndiyo dini ya haki. Dini hii ilileta mambo yaliyo sawa kwa watu na yenye kuwaboresha; kwa sababu ilitoka kwa Muumba wa watu, Mtukufu, aliye juu, anayewajua zaidi na anayajua yenye kuwanufaisha. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: "Je, aliyeumba hajui, naye ndiye Mjua siri, Mwenye habari?" [Al-Mulk: 14] Tofauti na sheria na mifumo mingine, Uislamu umekuja na mfumo unaohusiana na mali ambao unazingatia mahitaji ya mwili na mambo ya kidunia, na pia unazingatia mahitaji ya kiroho na mambo ya akhera.
Kwanza: Upande wa kidunia: Sheria ya Kiislamu ilidhibiti miamala ya watu inayohusiana na mali kwa njia ambayo inafanikisha uadilifu kati ya hao wanaoamiliana, na kwa njia ambayo inampa kila mwenye haki haki yake, na kuwapa wote utoshelevu. Vile vile ilipanua mlango wa halali katika miamala, na ikaharamisha kila kitu ambacho kinamdhuru mmoja wa hao wanaoamiliana.
Pili- Upande wa kidini: Lengo kuu la hukumu zote za kisheria ni kufikia ridha ya Mwenyezi Mungu na kupata Pepo. Kwa kuongezea, hukumu za miamala ya Kiislamu kunaleta udugu miongoni mwa waumini kwa kueneza uadilifu na kuhimiza hisani, kama vile kumpa muhula mwenye ugumu wa kulipa deni, na kuharamisha kila yenye kuleta chuki katika vifua, kama vile riba na kamari.
Kwanza - Uadilifu: Hili ndilo huhakikisha kwamba kila mmoja wa pande mbili ziinazoamiliana zinapata haki yake bila kuongezewa wala kupunguziwa, kama vile kuuza au kukodisha kwa bei inayofaa. Mwenyezi Mungu alisema: "Lakini Mwenyezi Mungu ameihalalisha biashara." (Al-Baqarah: 275). Pili - Fadhila: Nayo ni hisani; kama vile kumpa muhula mwenye ugumu katika kulipa deni au hata kumuondolea deni lote. Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: "Na akiwa (mdaiwa) ana shida, basi (mdai) angoje mpaka afarijike. Na mkiifanya deni kuwa ni sadaka, basi ni bora kwenu, ikiwa mnajua." [Al-Baqarah: 280] Na kama vile kukubaliana na mfanyakazi juu ya mshahara na kisha ukampa zaidi yake. Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: "Na fanyeni wema. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao wema." [Al-Baqarah: 195]
Tatu - Dhuluma: Ni mtu kupata zaidi ya haki yake, na kula mali za watu kwa batili; kama vile riba, kamari, kumnyima mfanyakazi haki yake na mengineyo. Mwenyezi Mungu alisema: "Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na acheni riba zilizobakia, ikiwa nyinyi ni Waumini. Basi msipofanya, jitangazieni vita na Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na mkitubu, basi haki yenu ni rasilmali zenu. Msidhulumu wala msidhulumiwe." (Al-Baqara: 278-279) Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alisema: "Mwenyezi Mungu amesema: "Nitakuwa hasimu dhidi ya watu watatu Siku ya Kiyama: 1. Mtu anayefanya agano kwa Jina langu, kisha akalivunja (akasaliti). 2. Mtu aliyemuuza mtu huru (kama mtumwa) na akala thamani yake 3. Mtu aliyeajiri mfanyakazi, na akamfanyia kazi kikamilifu, lakini yeye hakumlipa mshahara wake." (Al-Bukhari 2227)