Sehemu ya sasa:
Somo Siku kuu ya Iddi
Sikukuu ni miongoni mwa ishara za dhahiri za Dini:
Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie alipofika Madina, aliwakuta Ansari ambao ni Waislamu miongoni mwa watu wa Madina wakicheza na kufurahi katika siku mbili za mwaka. Akasema: "Siku hizi mbili ni zipi?" Wakasema: Tulikuwa tukisherehekea katika siku hizo katika zama za kabla ya Uislamu. Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, akasema: "Mwenyezi Mungu amekubadilishieni na kuwapa bora kuliko hizo: Siku ya Iddul-Adha na siku ya Iddul-Fitr." (Abu Dawud 1134) Na Mtume, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, pia alisema akibainisha kwamba siku kuu ni katika ishara za Dini: "Hakika kila umma una sikukuu yao. Na hii ndiyo siku kuu yetu."(Al-Bukhari 952, Muslim 892)
Siku ya Iddi katika Uislamu ni siku ambayo Waislamu huonyesha furaha kwa kukamilisha ibada fulani ili kushukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwaongoza waja wake na kuwawezesha kumuabudu. Inaruhusika katika siku hiyo kuingiza furaha katika nyoyo za watu kwa ujumla, kuvaa mavazi mazuri zaidi, kufanya hisani kwa wale wanaohitaji, na kuburudisha roho kwa njia zote zinazoruhusiwa kama vile sherehe na matukio ambayo huingiza furaha katika moyo wa kila mtu, na yanayowakumbusha neema ya Mwenyezi Mungu juu yao.
Waislamu wana Iddi mbili katika mwaka wanazozisherehekea, na hairuhusiwi kuteua siku miongoni mwa siku za mwaka na kuifanya kuwa sikukuu (Iddi). Iddi mbili hizi ni:
Ni swala ambayo Uislamu umeisisitiza na kuwahimiza Waislamu wanaume, wanawake na watoto kwamba kwenda kuitekeleza. Wakati wake huwa kuanzia jua linapoinuka juu kiasi cha mkuki kwenye upeo wa macho baada ya kuchomoza kwake siku ya Iddi hadi jua linapopita katikati ya mbingu.
Swala ya Iddi ni rakaa mbili ambamo imamu atasoma kwa sauti kubwa, na atatoa khutba mbili baada ya swala. Inaruhusika katika swala ya Iddi kuzidisha idadi ya takbira mwanzoni mwa kila rakaa. Kwa hivyo katika rakaa ya kwanza atatoa takbira sita kando na takbira ya kufungua swala, na katika rakaa ya pili atatoa takbira tano kando na takbira ya kunyanyuka kutoka kwenye sijda.
Hili linawajumuisha vijana na wazee, wanaume na wanawake, kwa kila njia inayoruhusiwa, wakiwa wamevaa nguo nzuri zaidi, na kumwabudu Mwenyezi Mungu kwa kutofungua saumu, bali kula katika mchana wa siku hiyo. Hii ni kwa sababu ni haramu kufunga katika siku ya Iddi.
Takbir imeamrishwa siku ya Iddul-Fitr ili kuonyesha furaha katika Iddi, na kukamilisha funga iliyobarikiwa ya Ramadhani, na kumshukuru Mwenyezi Mungu juu ya neema yake kwetu, na kutuongoza kwake kufunga saumu. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: "Na mtimize hiyo hesabu, na mumtukuze Mwenyezi Mungu kwa kuwa amekuongoeni ili mpate kushukuru." (Al-Baqarah: 185) Takbir pia imeruhusiwa siku ya Iddul-Adha; ili kuonyesha furaha katika Iddi, na kwa kufanya Hija kwa mahujaji, na kutuwezesha kufanya matendo mema katika siku kumi za Dhul-Hijja kwa mahujaji na kwa Waislamu wote. Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema alipotaja dhabihu: "Nyama zao hazimfikii Mwenyezi Mungu wala damu zao, lakini unamfikia ucha Mungu wenu. Namna hivi tumewadhalilisha kwenu ili mumtukuze Mwenyezi Mungu kwa alivyokuongoeni. Na wabashirie wafanyao mema." (Al-Hajj: 37)
Jinsi ya kufanya Takbira za Iddi
Mwenyezi Mungu ni mkubwa, Mwenyezi Mungu ni mkubwa, hakuna mungu ila Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu ni mkubwa, Mwenyezi Mungu ni mkubwa, sifa nzuri zote ni za Mwenyezi Mungu. Pia atasema: Mwenyezi Mungu ni mkubwa sana, na sifa njema nyingi ni za Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ametakasika asubuhi na jioni.
Imeamriwa kwa wanaume kuinua juu sauti zao wanapofanya Takbira kwa njia ambayo haiudhi watu au kuwashawishi, lakini wanawake wanapaswa kupunguza sauti zao wanapofanya Takbira.