Sehemu ya sasa:
Somo Mambo ya kiimani na Safari
Safari zinazomaanishwa hapa ni zile ambazo mwanadamu husafiri na kutembea katika maeneo ya maumbile ya asili na mfano wake.
Neno safari limetajwa katika Qur-ani katika maneno ya Mwenyezi Mungu: "Kwa walivyozoea Maquraish. Kuzoea kwao safari za siku za baridi na siku za joto." [Quraish: 1-2] Safari ya majira ya baridi ni safari ya biashara ya Maquraishi wakati wa baridi, na walikuwa wakielekea Yemen, nayo ya kwenda Yemen ilikuwa katika msimu wa joto.
Maisha ya Mwislamu yanafungamana na Mwenyezi Mungu na sheria yake katika hali zake zote. Nazo safari zimejaa hukumu mbalimbali za kisheria ambazo Mwenyezi Mungu ametuamuru. Kwa sababu ndani yake kuna masilahi makubwa katika dunia hii na Akhera, na hayo ni ikiwa mwanadamu atazitumia vizuri.
Muumini anaweza kufanya safari yake kuwa ibada kwa kwenda mahali ambapo ibada hupatikana, kama vile Hija na Umra, au kutafuta elimu. Na anaweza kufanya nia yake kuwa nzuri akikusudia kumuunga jamaa yake, au kuwafurahisha familia zake, au kujiondolea machofu yeye mwenyewe na hata wao kwa kitu kinachoweza kumsaidia kumtii Mwenyezi Mungu, au kumuweka mbali na kile ambacho Mwenyezi Mungu ameharamisha.
"Sema: Hakika Swala yangu, na ibada zangu, na uhai wangu, na kufa kwangu, ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote." [Al-An'am: 162]
Ulimwengu umejaa ishara za Mwenyezi Mungu zenye kuonyesha ukuu wake, rehema yake na hekima yake. Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: "Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi na kuhitalifiana usiku na mchana, ziko Ishara kwa wenye akili." [Al-Imran: 190] Hii ndiyo sababu aliamuru sana kuziangalia kwa kuzingatia, na siyo kuangalia tu kwa njia ya kujifurahisha. Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: "Je, hawatazami ufalme wa mbingu na ardhi, na vitu alivyoviumba Mwenyezi Mungu." (Al-A'raf: 185)
Pia, katika hali ya upweke wakati mwingine kuna fursa ya mtu kuihesabu nafsi yake, na kufikiria juu ya yale aliyotanguliza kwa ajili ya kesho. Hili ni wakati yuko peke yake na hana mwangalizi yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu tu.
Yeyote anayefika mahali alipokusudia katika safari yake; iwe yuko jangwani au mahali pengine, basi ameekewa katika sheria kusema dua ifuatayo.
Ilisimuliwa kutoka kwa Khaulah bint Hakim As-Sulamiyya, Mwenyezi Mungu amridhie, kuwa; Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, akisema: "Atakayeshukia mahali fulani, kisha akasema, "A'udhu bikalimatillahit-tammati min sharri ma khalaq (Ninajilinda kwa maneno ya Mwenyezi Mungu yaliyotimia kutokana na shari ya alichokiumba"), hakitamdhuri kitu chochote mpaka aondoke kutoka hapo mahali aliposhukia." (Muslim 2708)