Endelea kujifunza

Umeshaingia
Jisajili sasa kwenye jukwaa la Taa ili uanze kujifunza, na fuatialia maendeleo yako, na kukusanya pointi, na uingie kwenye mashindano.Baada ya kujisajili, utapata cheti cha kielektroniki katika mada ambazo utajifunza.

Sehemu ya sasa:

Somo Hukumu za jumla zinazopatikana katika safari za mara kwa mara

Hukumu zinazohusiana na kusafiri haziishii kwenye swala na kufunga saumu tu, bali kuna hali nyinginezo ambazo zina hukumu zake. Katika somo hili utajifunza baadhi ya hizo.

Kujua hukumu za jumla ambazo watu wanazihitaji sana kuzijua katika safari.

Kuzima moto wakati wa kulala

Kabla ya kulala, mtu anafaa kuzima moto ambao mara nyingi huwashwa kwenye safari za majira ya baridi; hasa katika mahema na mfano wake.

Imesimuliwa kutoka kwa Abu Musa Al-Ash'ari, Mwenyezi Mungu amridhie, kuwa alisema: Usiku mmoja, nyumba moja huko Madina ilichomeka pamoja na wakazi wake. Nabii, rehema na Amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, akaambiwa juu yao na akasema, "Hakika moto huu ni adui yenu. Kwa hivyo, mnapolala, basi uzimisheni." (Al-Bukhari 6294, Muslim 2016) Na katika Hadithi nyingine: "Msiache moto katika nyumba zenu mnapoenda kulala." (Al-Bukhari 6293, Muslim 2015) Katika hadithi nyingine: "Kwani wanyama waharibifu wanaweza wakavuta utambi na ukateketeza watu wa nyumba hiyo." (Bukhari 3316, Muslim 2012)

Humuku za kuwinda

Hali ya asili ni kwamba uwindaji unaruhusika.Lakini uwindaji haupaswi kuwa ndiyo sababu ya moyo kufungamana nao na kughafilika na masilahi ya dini na familia, au ukawa ndiyo sababu ya kupita kufanya ubadhirifu, upuuzi na kujifahirisha. Imekuja katika hadithi kwamba: Yeyote atakayekaa jangwani, atakuwa mgumu, na mwenye kufuatana na windo, ataghafilika." (Abu Dawud 2859)

Hali ya asili ni kwamba inaruhusika kuwinda na kula wanyama wote isipokuwa kile ambacho ushahidi unaonyesha kwamba kimekatazwa. Kama vile,kila mnyama mwenye machonge kama vile mbwa mwitu na mbweha, na kila ndege mwenye kucha za kuwindia, kama vile mwewe, na vile vile wanyama wenye sumu kama vile nyoka, na wengineo.

Ni halali kuwinda wanyama wa nchi kavu na wa baharini katika mwaka wote; na hakuna tofauti kati ya Ijumaa, mwezi wa Ramadhani, au miezi mitakatifu. Lakini ni haramu kuwinda katika eneo takatifu la huko Makka au Madina, ni haramu kuwinda wanyama wanaomilikiwa na watu wengine, na ni haramu kwa mtu aliye katika Ihram ya Hija au Umra kuwinda wanyama wa nchi kavu.

Ni sharti kwamba muwindaji awe ni Mwislamu, na kwamba alitaje jina la Mwenyezi Mungu, na kwamba awinde kwa kutumia mbwa au ndege waliofundishwa kuwinda. Ikiwa ndege anayewindia atapuruka na akatoka mwenyewe au ikiwa risasi yake itatoka yenyewe bila yeye kujua, basi haifai kula windo lake isipokuwa ikiwa ataliwahi kabla ya kufa kwake, alitajie jina la Mwenyezi Mungu, na alichinje.

Pia ni sharti kwamba windo afe kwa sababu ya kuumizwa na mnyama au ndege anayetumika kuwinda; siyo kwamba afe kutokana na kunyongwa, kuzamishwa, kupigwa kwa kitu kizito, au kuanguka kutoka mahali pa juu. Ikiwa mwindaji atamkuta windo hali ya kuwa hajafa, basi itamlazimu kumchinja kwa njia inayofaa kisheria.

Ni marufuku kumuua windo kwa ajili ya kucheza tu, kama vile mtu anayewinda kisha asimle. Na vile vile hali ambayo mwindaji anatumia vifaa vya uwindaji ili kuwatishia watu. Na pia ni dhambi kumfunga ndege kwa ajili ya kufanya mazoezi ya uwindaji.

Ibn 'Umar alipita karibu na wavulana wa Kiquraishi ambao walikuwa wamemuweka mbele ndege huku wakimtupia mishale. Na walikuwa wamempa mwenye ndege huyo kila mshale waliokosa kumpiga ndege huyo kwao. Pindi walipomwona Ibn Umar, wakatawanyika. Ibn 'Umar akasema: Ni nani aliyefanya hivi? Mwenyezi Mungu amemlaani mwenye kufanya hivi. Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alimlaani mwenye kufanya hivi. (Al-Bukhari 5515, Muslim 1958)

Ni marufuku kuelekeza silaha kwa wengine, hata kama ni kwa njia ya kucheza tu. Ilikuwa katika hadithi kwamba: "Asimwashirie mmoja wenu ndugu yake kwa silaha. Kwa maana, mmoja wenu hajui, Shetani anaweza kumpokonya kutoka mkononi mwake, kwa hivyo akaanguka ndani ya shimo katika Moto." (Al-Bukhari 7072, Muslim 2617) Na katika hadithi nyingine: "Yeyote anayemuashiria ndugu yake kwa chuma, basi malaika wanamlaani mpaka awache kufanya hivyo, hata kama ni ndugu yake wa kwa baba yake na mama yake." (Muslim 2616)

Ni lazima kwa mwindaji kujua kanuni za kuwinda, na tahadhari za usalama ili ajilinde yeye mwenyewe na awalinde wengine. Na kuna hukumu maalumu zinazohusiana na namna ya kuchinja wanyama kisheria, na jinsi ya kuamiliana na mbwa wa kuwindia, na hali ambazo windo anakuwa amekufa na mengineyo. Basi na mtu awarudie wanazuoni katika hayo.

Hukumu za vyakula

Kanuni ya asili ni kwamba vyakula vyote ni halali isipokuwa vile ambavyo ushahidi ulionyesha kwamba ni haramu.

Miongoni mwa vyakula na vinywaji vilivyoharamishwa

١
Mfu na vitu vinavyotokana na mfu
٢
Nguruwe
٣
Pombe na dawa za kulevya; na kila kitu ambacho kingi chake huondoa akili, basi pia kichache chake ni haramu.
٤
Kila kitu chenye madhara kwa mwili
٥
Kila mnyama mwenye machonge ambayo anawinda kwayo, kama vile simba, mbwa, na paka au kila kitu chenye kucha za kuwindia kama vile mwewe na tai.
٦
Vyakula vilivyoibiwa na kunyang'anywa

Mimea yote na matunda yanayopatikana porini au sokoni yanaruhusiwa. Lakini Muislamu hapaswi kula kile kinachoweza kumdhuru, au kile asichojua usalama wake.

Umemaliza somo kwa ufanisi


Anza mtihani