Sehemu ya sasa:
Somo Kuamini Uungu wa Mwenyezi Mungu
Maana ya Tauhid Al-Uluhiyya (Tauhidi ya Uungu)
Ni kusadiki kithabiti kwamba Mwenyezi Mungu, Mtukufu peke yake ndiye anayestahiki kila aina ya ibada za dhahiri na za ndani. Kwa hivyo, tunampwekesha Mwenyezi Mungu katika kila aina za ibada, kama vile dua, hofu, kutegemea, kuomba msaada, Swala, Zaka na Saumu. Kwa hivyo, hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, Mtukufu. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu aliyetukuka, "Mungu wenu ni Mungu Mmoja. Kwa hivyo, mwenye kutaraji kukutana na Mola wake Mlezi, basi na atende vitendo vyema, wala asimshirikishe yeyote katika ibada ya Mola wake Mlezi." (Al-Kahf: 110)
Hapa, Yeye Mtukufu akajulisha kuwa Mungu ni Mungu mmoja; yaani, muabudiwa mmoja. Kwa hivyo, hairuhusiki kuchukuliwa mungu mwingine asiyekuwa Yeye, na asiabudiwe asiyekuwa Yeye.
Umuhimu wa Tauhid Al-Uluhiyya (kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika uungu wake):
Unadhihirika umuhimu wa Tauhid Al-Uluhiyya (kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika uungu wake) katika pande nyingi:
1. Kwamba ndiyo makusudio ya kuumbwa majini na wanadamu
Hawakuumbwa isipokuwa wamuabudu Mwenyezi Mungu peke yake, ambaye hana mshirika. Kama alivyosema Mtakatifu, "Nami sikuwaumba majini na watu isipokuwa kwamba waniabudu Mimi." (Adh-Dhariyat: 56)
2. Kwamba hilo ndilo kusudio katika kutumwa Mitume na kuteremshwa Vitabu.
Makusudio ya hilo ni kuwalingania viumbe wamwabudu Mwenyezi Mungu peke yake, na wakufuru vinavyoabudiwa badala yake. Kama alivyosema Mtakatifu, "Na kwa hakika, kwa kila umma tuliutumia Mtume kwamba: Muabuduni Mwenyezi Mungu, na muepukeni Twaghut." (An-Nahl: 36)
3. Kwamba ndio wajibu wa kwanza juu ya mwanadamu
Kama ilivyokuja katika wasia wa Nabii - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - kwa Mu’adh bin Jabal, Mwenyezi Mungu amuwie radhi, alipomtuma Yemen, akamwambia, “Hakika wewe, utawajia kaumu ya Watu wa Kitabu, basi na liwe jambo la kwanza utakalowalingania ni kumwabudu Mwenyezi Mungu, Mwenye Nguvu, Mtukufu.” (Bukhari 1458, Muslim 19)
4. Kwamba Tauhid Al-Ulihiyya (ya uungu) ndiyo maana halisi ya “Hakuna mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu.”
Kwa hivyo, Mungu ndiye muabudiwa. Na maana ya “hakuna mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu,” ni hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, tunamuabudu Yeye pekee, wala hatumfanyii asiyekuwa Yeye chochote katika aina za ibada.
5. Kwamba kuamini Uungu ndiyo matokeo ya kimantiki ya kuamini kwamba Mwenyezi Mungu pekee yake ndiye Muumba, Mmiliki, Mwendeshaji mambo.