Endelea kujifunza

Umeshaingia
Jisajili sasa kwenye jukwaa la Taa ili uanze kujifunza, na fuatialia maendeleo yako, na kukusanya pointi, na uingie kwenye mashindano.Baada ya kujisajili, utapata cheti cha kielektroniki katika mada ambazo utajifunza.

Sehemu ya sasa:

Somo Kuamini Majina ya Mwenyezi Mungu na Sifa zake

Kumjua Mwenyezi Mungu, Mwenye Nguvu, Mtukufu kwa Majina yake mazuri mazuri na Sifa zake zilizotukuka, na kumwabudu Mwenyezi Mungu Mtakatifu kwa matakwa yake ni katika matendo makubwa zaidi yanayoongeza imani. Katika somo hili, utajifunza kuhusu baadhi ya hayo.

  • Kuijua Tauhid ya majina na sifa.
  • Kuijua itikadi ya Ahlus-Sunnah wal-Jamaa katika majina na sifa.
  • Kuzijua maana za baadhi ya majina ya Mwenyezi Mungu, Mwenye Nguvu, Mtukufu.

Kuamini katika majina ya Mwenyezi Mungu na sifa zake

Qur-ani imesisitiza juu ya kuwabainishia waja Mola wao Mlezi na Muumba wao, na ikarudia haya katika nyingi ya Aya. Kwa sababu, ni lazima kwa Muislamu kumjua Mola wake Mlezi kwa Majina yake Mazuri zaidi na sifa za utukufu na uzuri ambazo Yeye Mtakatifu anasifika kwazo ili amwabudu Mwenyezi Mungu kwa elimu, na atekeleze matakwa ya majina hayo na sifa, na athari zake katika maisha yake na ibada zake.

Basi, Muislamu anaamini yale aliyojithibitishia Mwenyezi Mungu katika Kitabu chake au Sunna za Mtume wake - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, - miongoni mwa majina na sifa kwa namna inayomfaa Mwenyezi Mungu, Mtukufu.

Na Mwenyezi Mungu, Mtakatifu ana majina mazuri kabisa, na sifa kamilifu zaidi, na wala hana mfano wake katika majina yake na sifa zake. Kama alivyosema Yeye Mtukufu, "Hakuna kitu kama mfano wake. Naye ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona." (Al-Shura: 11) Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu ametakasika kutoka na kufanana na yeyote katika viumbe vyake katika majina yake yote na sifa zake.

"Sema: Mwombeni Mwenyezi Mungu, au mwombeni Ar-Rahman (Mwingi wa Rehema). Kwa jina lolote mnalomwita, kwani Yeye ana majina mazuri mazuri." (Al-Isra: 110)

Na hapa tunawasilisha baadhi ya majina ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Ar-Rahman (Mwingi wa rehema), Ar-Rahim (Mwenye kurehemu)

Na majina haya mawili ni yale ambayo Mwenyezi Mungu alianzisha kwayo ufunguzi wa Kitabu chake, na jambo la kwanza ambalo Mwenyezi Mungu Mtukufu alijitambulisha kwalo kwa waja wake, na kwa hayo sura zote za Qur-ani Tukufu zilianza kwa kauli yake, "Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu," isipokuwa Surat At-Tawba.

Na Mola wetu Mlezi alijitolea kujiandikia rehema juu ya nafsi yake. Na rehema zake Yeye Mtakatifu zimeenea kila kitu, kiasi kwamba rehema ya viumbe wao kwa wao, na rehema ya mama kwa mtoto wake, na kuwafikishia chakula viumbe si isipokuwa athari katika athari za rehema ya Mwenyezi Mungu kwa viumbe vyake. Kama alivyosema Yeye Mtukufu, "Basi ziangalie athari za rehema ya Mwenyezi Mungu, jinsi anavyoihuisha ardhi baada ya kufa kwake." (Ar-Rum: 50).

Na imesimuliwa kutoka kwa 'Umar Ibn Al-Khattab, Mwenyezi Mungu amuwie radhi, “Mateka fulani walimjia Nabii - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, - na tazama, mwanamke mmoja katika mateka hao alikuwa anakama matiti yake akimnywesha. Na akimkuta mtoto katika mateka, anamchukua na kumshikanisha na tumbo lake na anamnyonyesha. Nabii - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - akatuambia: "Je, mnamuona huyu anaweza kumtupa mtoto wake katika Moto?" Tukasema: Hapana, na hali ya kuwa anaweza kutomtupa." Akasema, "Hakika, Mwenyezi Mungu ni mwenye huruma zaidi kwa waja wake kuliko huyu kwa mtoto wake.” (Bukhari 5999, Muslim 2754).

Basi, rehema yake Muumba Mtakatifu, Mtukufu ni kitu kingine kikubwa zaidi na kitukufu zaidi. Nayo iko juu zaidi ya kila makadirio, na dhana, au kufikiria. Na lau kuwa waja wangejua thamani ya rehema ya Mwenyezi Mungu, Mwenye Nguvu, Mtukufu, basi hangekata tamaa yeyote katika rehema yake.

Na rehema za Mwenyezi Mungu ni aina mbili:

١
Ni rehema kwa viumbe vyote, na binadamu, na wanyama na viumbe visivyo na uhai, wanapata kwayo wepesi wa kidunia. Kama alivyosema Yeye Mtukufu akijulisha kuhusu dua ya Malaika wake, "Mola wetu Mlezi! Umekienea kila kitu kwa rehema na elimu." (Ghafir: 7)
٢
Ni rehema maalumu kwa waja wake Waumini. Kwa hivyo, anawawezesha kwenye utiifu, anawasahilishia heri, na anawaweka imara juu yake kwa rehema yake, na anawakamilishia rehema yake kwa kuwasamehe na kuwafutia dhambi, na kuwaingiza Peponi na kuwaokoa na Moto. Kama alivyosema Yeye Mtukufu, "Naye ni Mwenye kuwarehemu Waumini. Maamkizi yao siku watakayokutana naye yatakuwa Salama! Na amewaandalia malipo ya ukarimu." (Al-Ahzab: 43-44)

Na alisema Nabii - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, “Hayatamwingiza Peponi yeyote matendo yake mema.” Wakasema, “Hata wewe ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?" Akasema, “Hata mimi, isipokuwa ikiwa Mwenyezi Mungu atanigubika kwa rehema yake.” (Bukhari 6467, Muslim 2818)

Na mja kila utiifu wake unavyokuwa mkubwa na ukaribu wake na kukazidi kunyenyekea kwake kwa Mola wake Mlezi, ndivyo linazidi fungu lake katika kustahiki rehema hizi. Kama alivyosema Yeye Mtukufu, "Hakika, rehema ya Mwenyezi Mungu iko karibu na walio wema." (Al-A'raf: 56)

Mwenye kusikia yote, Mwenye kuona vyema:

Mwenyezi Mungu, Mtakatifu anasikia sauti zote, pamoja na utofauti wa lugha mbalimbali na mahitaji tofauti tofauti, kwake ni sawa siri ya usemi au uwazi wake. Na baadhi ya watu wajinga walipodhania kuwa Mwenyezi Mungu Mtakatifu hasikii siri zao na mazungumzo yao yaliyofichikana, akateremsha maneno ya Mwenyezi Mungu, Mwenyez baraka, Mtukufu akiwarudi na kuwakemea:, "Au wanadhani kwamba hatusikii siri zao na minong'ono yao? Sivyo hivyo! Na wajumbe wetu wapo karibu nao, wanayaandika maneno yao yaliyofichika." (Az-Zukhruf: 80)

Na Mwenyezi Mungu, Mtakatifu anakiona kila kitu, hata kiwe kidogo vipi, haifichiki kwake chenye kufichika Yeye aliyetakasika. Na hakika Ibrahim, amani iwe juu yake, alimpinga baba yake kuabudu sanamu ambalo halisikii wala halioni. Hivyo akasema kama ilivyo katika Qur-ani Tukufu: "Ewe baba yangu! Kwa nini unaabudu vile ambavyo havisikii, wala havioni, wala havikufai chochote?" (Maryam: 42)

Mja anapojua kwamba Mwenyezi Mungu Mtakatifu ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona, hakuna uzito wa chembe unaofichika kwake katika mbingu wala katika ardhi, na kwamba anajua siri na kilichofichika zaidi, basi hilo litamsababishia kumchunga Mwenyezi Mungu Mtakatifu. Basi anakuwa mwenye kuuchunga ulimi wake usije ukaanguka katika uongo na kashfa, na akavilinda viungo vyake na mielekeo ya moyo wake kutokana na kila kinachomkasirisha Mwenyezi Mungu, na akazitia neema hizo na uwezo katika yale anayoyapenda Mwenyezi Mungu na anayaridhia. Kwa sababu Yeye anaijua siri yake na uwazi wake, na dhahiri yake na ndani yake. Na kwa sababu ya hilo, ndiyo maana akasema yeye, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, “Ihsan ni kwamba umwabudu Mwenyezi Mungu kana kwamba unamuona, na ikiwa haumwoni. basi Yeye kwa hakika anakuona.” (Bukhari 4777, Muslim 9)

Aliye hai, msimamia yote.

Mwenyezi Mungu, Mwenye Nguvu, Mtukufu ana uhai mkamilifu ambao haukutanguliwa na kutokuwepo, wala hautafuatiwa na kutoweka au kuisha, wala haupatwi na upungufu au dosari. Ametukuka Mola wetu Mlezi na ametakasika kutokana na yote hayo. Uhai unaolazimu ukamilifu wa sifa zake kama vile elimu, na kusikia, na kuona, na uwezo, na kutaka, na zisizokuwa hizo miongoni mwa sifa zake Yeye Mtukufu. Na yule ambaye ni wa namna hii, anastahiki kuabudiwa, kufanyiwa rukuu, na kumtegemea Yeye. Kama alivyosema Yeye Mtukufu, "Na mtegemee aliye hai ambaye hafi." (Al-Furqan: 58).

Na maana ya jina la Mwenyezi Mungu "Msimamia yote," linaashiria mambo mawili:

١
Ukamilifu wa kutohitajia kwake Yeye Mtakatifu. Yeye ndiye anayejisimamia mwenyewe, asiyewahitajia viumbe vyake, kama alivyosema Yeye Mtukufu, "Enyi watu! Nyinyi ndio wenye haja kwa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujitosha, Msifiwa." (Fatir: 15) Basi Yeye, Mtakatifu hawahitajii viumbe wake, kwa kila namna. Kwa hivyo hakumnufaishi kutii kwa mtiifu, wala kuuasi kwa muasi hakumdhuru. Kama alivyosema Yeye Mtukufu, "Na anayefanya juhudi basi bila ya shaka anafanya juhudi kwa ajili ya nafsi yake. Hakika Mwenyezi Mungu si mhitaji wa walimwengu." (Ankabut 6) Na alisema juu ya ulimi wa Musa amani iwe juu yake, "Mkikufuru nyinyi na wote waliomo duniani, hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujitosha, Msifiwa.” (Ibrahim: 8)
٢
Ukamilifu wa uwezo wake na uendeshaji wake wa viumbe. Kwani Yeye ndiye anayevisimamia kwa uwezo wake, Yeye Mtakatifu. Na viumbe vyote ni mafakiri, wanamhitajia Yeye, hawawezi kutomhitajia kwa kiasi cha kupepesa jicho. Na kile tunachokiona katika mpangilio mzuri wa ulimwengu na mwendo wa maisha siyo isipokuwa katika athari za usimamizi wake, Yeye Mtakatifu. Kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema akimkanusha yeyote mwenye kumshirikisha asiyekuwa Yeye pamoja na Mwenyezi Mungu, "Je, anayeisimamia kila nafsi kwa yale iliyoyachuma...? (Ar-Ra'd 33). Naye Mtukufu alisema, "Hakika, Mwenyezi Mungu ndiye anayezuilia mbingu na ardhi zisiondoke. Na zikiondoka, hapana yeyote wa kuzizuia isipokuwa Yeye." (Fatir 41)

Na ndiyo maana kujumuika kwa majina mawili haya makuu kulikuwa na nafasi maalumu katika dua na kunyenyekea. Na ilikuwa katika dua zake yeye - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, - “Ewe uliye hai, ewe Msimamia yote, kwa rehema zako ninaomba msaada.” (Al-Tirmidhiy 3524)

Matunda ya kuamini katika majina ya Mwenyezi Mungu na sifa zake

١
Kumjua Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kwa hivyo, mwenye kuamini majina ya Mwenyezi Mungu na sifa zake, atazidisha kumjua Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwa hivyo inaongezeka imani yake kwa Mwenyezi Mungu kwa yakini, na unaimarika upwekeshaji wake wa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na ni haki kwa mwenye kujua majina ya Mwenyezi Mungu na sifa zake kwamba moyo wake ujazwe na utukuzaji wa Yeye Mtukufu, Mtakatifu na upendo, na kumnyenyekea kwake.
٢
Kumsifu Mwenyezi Mungu kwa Majina yake mazuri. Na huu ni miongoni mwa aina bora zaidi za kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema, "Enyi mlioamini, mkumbukeni Mwenyezi Mungu kukumbuka kwingi." (Al-Ahzab: 41)
٣
Kumuuliza Mwenyezi Mungu na kumwomba kwa majina yake na sifa zake, kama alivyosema Yeye Mtakatifu, "Na Mwenyezi Mungu ana majina mazuri kabisa, basi muombeni kwayo." (Al-A'raf: 180) Na mfano wa hayo ni aseme, "Ewe Mwenye kuruzuku, niruzuku. Na ewe Mwingi wa kukubali toba, nikubalie toba yangu. Na ewe Mwingi wa Rehema, nirehemu."

Umemaliza somo kwa ufanisi


Anza mtihani